KIUNGO YANGA ABAINISHA SABABU ZA KUCHEZA CHINI YA KIWANGO


 KIUNGO mkabaji mpya wa Yanga, Mganda, 
Khalid Aucho,amewaambia mashabiki kuwa watarajie kuona soka safi la pasi linalochezwa katika baadhi ya klabu kubwa Ulaya kwenye michezo ijayo wa Ligi Kuu Bara.


Kauli hiyo aliitoa mara baada ya mashabiki wa timu hiyo kulalamikia kiwango kibovu licha ya kupata ushindi kwenye mechi ya ufunguzi dhidi ya Kagera Sugar.


Kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Kagera Sugar ambao ulikuwa ni wa ufunguzi kwa msimu wa 2021/22 Yanga ilifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na kiungo mzawa,Feisal Salum ‘Fei Toto’ kwa shuti kali ndani ya 18 Uwanja wa Kaitaba. 

Nyota huyo alisema kuwa kwenye mechi yao dhidi ya Kagera Sugar walicheza wakiwa wamechoka baada ya kutumia nguvu mbele ya Simba lakini wana imani ya kuendelea kufanya vizuri kwenye mechi zijazo. 

"Mchezo wetu dhidi ya Kagera ulikuwa mgumu,lakini licha ya ugumu tunashukuru kuanza ligi vizuri kwa ushindi ambao umetuongezea nguvu katika michezo ijayo.


“Mchezo wa mwanzo tulicheza chini ya kiwango kutokana na miili kuchoka kwa kuwa tulitoka kwenye mchezo mgumu dhidi ya Simba hivyo tunaamini kwamba kwa mechi zijazo tutafanya vizuri na kupata matokeo chanya,hata safari ile ya Kagera Sugar nayo iliweza kutufanya tuwe wachovu, kwa mechi zijazo ni kazikazi," .

Yanga kwenye msimamo ipo nafasi ya pili ina pointi sita kwa kuwa mchezo wake wa pili ilishinda pia bao 1-0 dhidi ya Geita Gold, Uwanja wa Mkapa, mchezo wao ujao ni dhidi ya KMC, Uwanja wa Majimaji, Songea.

Chanzo:Championi



Comments

Popular posts from this blog

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA