Posts

Showing posts from September, 2021

MZUNGUKO WA KWANZA WAKUSANYA MABAO 10 BONGO

Image
  BAADA ya  Ligi Kuu Bara kuanza msimu wa 2021/22 kasi imekuwa kubwa kwa kila timu kupambana kusaka pointi tatu huku katika michezo iliyoshuhudiwa kwenye viwanja vitatu tofauti, ni Uwanja wa Karume ulikamilisha dakika 90 bila timu kupata bao. Mchezo huo ulikuwa ni wa kukata na shoka kwa wawakilishi wa kimataifa kukutana uwanjani ambapo ilikuwa ni Biashara United wenyeji wanaopeperusha bendera kwenye Kombe la Shirikisho pamoja na Simba wanaopeperusha bendera kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na ulikamilika kwa ubao kusoma Biashara United 0-0 Simba. Ni mabao 10 pekee yamekusanywa katika mzunguko wa kwanza ambapo kinara wa utupiaji kwa sasa ni Vitalis Mayanga na alifunga mabao yote mawili, Uwanja wa Karatu wakati timu yake ya Polisi Tanzania ikiwaadhibu KMC mabao 2-0 Uwanja wa Karatu. Pia mchezo ambao ulishuhudia mabao mengi yakikusanywa ukiachana na ule kati ya Polisi Tanzania na KMC ni ule wa Namungo 2-0 Geita Gold Uwanja wa Ilulu Lindi ambapo nyota wa mchezo alikuwa ni Obrey Chirwa

VIDEO: SHANGWE LA DODOMA JIJI WANAOKUTANA NA SIMBA

Image
WACHEZAJI wa Dodoma Jiji inayonolewa na Kocha Mkuu Mbwana Makata leo Oktoba Mosi wana kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri,Dodoma.  Wakiwa kambini wachezaji hao wamekuwa ni wenye furaha kabla ya kucheza mchezo wao wa pili wa Ligi Kuu Bara ambapo katika mchezo wa kwanza waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting.    Wanakutana na Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ambaye ametoka kupata pointi moja mbele ya Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.  

VIDEO:KUMBE SABABU YA SIMBA KUFUNGWA NA YANGA NI LUIS NA CHAMA

Image
SHABIKI wa Simba kutoka Dodoma ameweka wazi kuwa alikuwa anaipenda Simba tangu akiwa mdogo na alikuwa anaacha mifungo ili aweze kutazama Simba wakicheza, pia amesema kuwa walishindwa kufunga mbele ya Yanga kwa sababu viungo wawili walikuwa wameondoka ambao ni Luis Miquissone na Clatous Chama.  

KOEMAN KUPIGWA CHINI BARCELONA

Image
 IMEELEZWA kuwa maisha ya Kocha Mkuu wa Barcelona,  Ronald Koeman kwa sasa yanakaribia kufika ukingoni kwa kuwa ni suala la muda tu kwake kutimuliwa ndani ya kikosi hicho kinachoshiriki La Liga. Mwendo wa Barcelona katika Ligi ya Mabingwa Ulaya ni wa vichapo tu kwa kuwa wamepoteza mechi zote mbili ambapo wanashika mkia kwenye kundi E wakiwa bila pointi na vinara ni Bayern Munich wenye pointi sita. Kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Benfica iliyo nafasi ya pili kwenye kundi katika mchezo uliochezwa Septemba 29 huku mabao yakipachikwa na Darwin Nunez dakika ya 3 na 79 kwa penalti  na lile la tatu lilipachikwa na Rafa Silva dakika ya 69 huku nyota wa Barcelona Eric Garcia akionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 87 kimetibua mambo ndani ya Barcelona.  Mpaka sasa hata Koeman mwenyewe hajui hatma yake na anaamini kwamba atatimuliwa muda wowote kuanzia sasa na kesho ana mtihani mwingine mbele ya Atletico Madrid katika mchezo wa La Liga unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Wanda Metropolitan. Lic

MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA

Image
  MUONEKANO wa ukurasa wa nyuma gazeti la Championi Ijumaa 

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA

Image
  MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi Ijumaa 

MZUNGUKO WA KWANZA UMEACHA REKODI HIZI BONGO

Image
MZUNGUKO wa kwanza umekamilika kwa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2021/22 huku rekodi zikiandikwa katika mechi ambazo zimechezwa kwenye viwanja nane tofauti. Pazia la Ligi Kuu Bara lilifunguliwa Septemba 27 ambapo ilishuhudiwa michezo mitatu ya kukata na shoka ndani ya ligi ambayo imekuwa na ushindani mkubwa. Ilikuwa ni Septemba 27 ambapo kazi ilianza kwa Mtibwa Sugar kusaka pointi tatu mbele ya Mbeya Kwanza ilikuwa Uwanja wa Mabatini, Kibaha na ngoma ilikamilika kwa ubao kusoma Mtibwa Sugar 0-1 Mbeya Kwanza. Mtupiaji wa kwanza msimu wa 2021/22 ni nyota wa Mbeya Kwanza, Edgar William ambaye alifanya hivyo dakika ya 49 kwa shuti lake la mguu wa kushoto. Katika mchezo mwingine wa pili ulikuwa ni ule uliowakutanisha Namungo na Geita Gold pale Lindi na ubao wa Ilulu ulisoma Namungo 2-0 Geita Gold. Burudani nyingine tamu ilikuwa ni kati ya Coastal Union dhidi ya Azam FC pale Mkwakwani, Tanga na mwisho ubao ulisoma Coastal Union 1-1 Azam FC  na kuwafanya wababe hao kugawana pointi mo

MWAMNYETO:KAZE ATAONGEZA JAMBO NDANI YA YANGA

Image
  NAHODHA wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amebainisha kuwa ujio wa Cedric Kaze ndani ya kikosi hicho utawaongezea jambo la kipekee katika harakati za kusaka ubingwa wa Ligi Kuu Bara. Kaze alikuwa ndani ya Yanga msimu wa 2020/21 alifutwa kazi kutokana na mabosi wa timu hiyo kueleza kuwa mwendo wa timu hiyo ulikuwa ni mbovu ila amerejeshwa msimu huu wa 2021/22 akiwa ni Kocha Msaidizi. Nahodha huyo amesema:”Uwepo wa Kaze ndani ya Yanga una jambo nzuri kwa sababu alishawahi kutufundisha na anatambua namna ligi ya Tanzania ilivyo. “Kwa kuwa hatukuwa na kocha msaidizi na yeye amekuja wakati huu imani yetu ni kuona kwamba tunafanya vizuri na tutapambana ili kupata matokeo chanya. "Jambo la msingi ni mashabiki kuendelea kuwa bega kwa bega nasi katika kazi ambayo tunafanya tunaamini kwamba kila kitu kitakuwa sawa,". Mchezo wa ufunguzi wa ligi, Yanga ilicheza dhidi ya Kagera Sugar na iliibuka na ushindi wa bao 1-0 Uwanja wa Kaitaba ilikuwa ni Septemba 29.

UFALME WA TSHABALALA NA KAPOMBE WATIKISWA

Image
 ISRAEL Mwenda, nyota mpya ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes amefanikiwa kuweza kuuteka ufalme wa Mohamed Hussein, “Tshabalala’ kwa muda kwenye mechi yake ya kwanza ya ushindani ndani ya ligi. Mwenda aliibuka ndani ya Simba akitokea KMC ambapo ujio wake ulikuwa unatajwa kukutana na ushindani mkubwa ndani ya Simba kutokana na uwepo wa mabeki wengine, Shomari Kapombe na Tshabalala. Akiwa na jezi ya Simba, katika mchezo wa kwanza wa ligi mbele ya Biashara United aliweza kuanza moja kwa moja kikosi cha kwanza na kutumia dakika 90 kuonyesha kile ambacho kimejificha kwenye miguu yake. Kipindi cha kwanza alicheza namba tatu huku Kapombe akiwa ni namba mbili na dakika zote hizo aliweza kuwa mwiba kwa Biashara United ambapo aliweza kufanya majaribio manne na yote yaligota kwenye mikono ya kipa wa Biashara United, James Ssetupa. Kipindi cha pili Tshabala alivyoingia akitokea benchi alibadili upande ambapo Tshabalala alicheza namba tatu, Mwenda namba mb

HESABU ZA YANGA NI KUIVUA TAJI LINGINE TENA SIMBA

Image
 MSHAMBULIAJI wa Yanga, Heritier Makambo, amefunguka kuwa baada ya kufanikiwa kuwavua Simba ubingwa wa Ngao ya Jamii, sasa mipango yao ni kuhakikisha wanawavua tena ubingwa wa Ligi Kuu Bara. Jumamosi iliyopita katika mchezo wa Kariakoo Dabi kuwania Ngao ya Jamii uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar, Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba. Taji hilo lilikuwa likishikiliwa na Simba. Akizungumza na Spoti Xtra, Makambo alisema: “Kwanza kabisa kama wachezaji tumefurahishwa sana na matokeo ya mchezo wetu dhidi ya Simba, ushindi lilikuwa jambo muhimu kwa kuwa tulikuwa tumetoka kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. “Jambo zuri ni kuwa tumeshinda ubingwa wetu wa kwanza na sasa macho yetu yote ni kuhakikisha tunaanza vizuri kwenye ligi baada ya kumaliza kazi yetu mbele ya Simba kwa kuwa tumeshatwaa Ngao ya Jamii. “Nina furaha kuwa tumeanza vizuri kwa kuwafunga watani wetu, kwetu huu ni mwanzo mzuri na nina imani tutazidi kufanya vizuri, huu ni mwaka wetu, tunawaahidi mashab

KMC NGUVU ZOTE SASA MKWAKWANI KWA COASTAL UNION

Image
BAADA ya kupoteza pointi tatu kwenye mchezo wao wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara, Klabu ya KMC nguvu zake zote sasa ni kuelekea kwenye mchezo wao ujao dhidi ya Coastal Union. Jana ikiwa Uwanja wa Karatu, ilishuhudia ubao ukisoma Polisi Tanzania 2-0 KMC jambo lililowafanya wapoteze furaha kwa kuziacha pointi tatu mazima. Ni mabao ya Vitalis Mayanga ambaye aliwahi pia kuwa ndani ya KMC aliwatungua dakika ya 3 na 20 kipindi cha kwanza huku kipindi cha pili jitahada za washambuliaji wa KMC kuweka mzani sawa zilikwama pale Uwanja wa Karatu. Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wamepoteza mchezo wao wa kwanza mbele ya Polisi Tanzania hivyo nguvu zao wanazipeleka kwenye mchezo ujao. Itakuwa ni Oktoba 2, pale Uwanja wa Mkwakwani dhidi ya Coastal Union ya Tanga ambayo imetoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wao wa ufunguzi. Ikumbukwe kwamba kabla ya mchezo wa KMC kukamilika kuchezwa Uwanja wa Karatu ulibadilishwa viwanja mara mbili amba

DIRRA AFICHUA KILICHO NYUMA YA UBORA WAKE

Image
 MLINDA mlango wa Yanga raia wa Mali, Djigui Diarra ‘Screen Protector’ amefunguka kuwa siri kubwa ya ubora wake katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Simba, ni kufuata maelekezo ya makocha wake, pamoja na muunganiko mzuri wa safu yao ya ulinzi. Diarra ni miongoni mwa nyota ambao walikuwa kwenye kiwango kikubwa Jumamosi na kuisaidia Yanga kushinda taji la Ngao ya Jamii kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba, kwenye mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam. Katika mchezo wa Jumamosi, Diara alikuwa katika kiwango kikubwa ambapo alifanikiwa kuokoa mashuti matatu ya hatari yaliyolenga lango kati ya mashuti yote 15 ambayo yalipigwa na Simba katika mchezo huo. Akizungumza na Championi Jumatatu, Diara alisema: “Kwanza kabisa nashukuru sana kumaliza mechi salama na kufanikiwa kushinda taji la Ngao ya Jamii tena dhidi ya Simba, ulikuwa mchezo mzuri na ambao kila mmoja alipambana kwa jasho na damu kwa ajili ya timu. “Kuhusiana na kiwango changu naweza kusema siri kubwa

AZAM FC MALENGO YAO YAPO KWENYE TAJI

Image
 KOCHA Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati, ameweka wazi kuwa malengo makubwa ya timu yao msimu huu wa 2021/22 ni kuhakikisha wanashinda ubingwa wa Ligi Kuu Bara kama ilivyokuwa msimu wa 2013/14   Azam FC mchezo wake wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu mpya wa 2021/22 ilianza kwa kugawana pointi mojamoja ugenini. Baada ya dakika 90, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ubao ulisoma Coastal Union 1-1 Azam FC hivyo wameacha pointi mbili sawa na wenyeji wao. Bahati amesema:- “Baada ya kuwa na mwanzo mzuri katika Kombe la Shirikisho Afrika ambapo timu yetu imefanikiwa kufuzu hatua ya kwanza, sasa ni muda wa kurejea kwenye mashindano mengine muhimu ambayo ni Ligi Kuu Bara. “Tumekuwa na maandalizi mazuri ya kabla ya msimu, pia tumefanya usajili bora kwa msimu huu wa 2021/22, malengo yetu makubwa ni kushinda ubingwa wa Ligi Kuu, kwa ubora wa kikosi chetu tunaamini hilo linawezekana.” Mchezo wao ujao kwenye Ligi Kuu Bara ni dhidi ya Polisi Tanzania ambayo ilianza kwa ushindi wa mabao 2-0 d

RONALDO AWATIBULIA MAMBO VILLARREAL USIKU

Image
  DUNIA inamtambua mzee wa kuvunja rekodi Cristiano Ronaldo,  mshambuliaji wa Klabu ya Manchester United baada ya kufunga bao la ushindi katika dakika za lala salama wakati Manchester United ikiitungua mabao 2-1 Villarreal katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.  Mbele ya mashabiki 73,130 waliohudhuria Uwanja wa Old Trafford Ronaldo alivunja rekodi ya kuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi za Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa amefanya hivyo mara 178 na bao lake la dakika ya 90+5 likiipa pointi United katika kundi F. Ni Paco Alcacer alianza kufunga dakika ya 53 kwa mkwaju wa penalti ila lilisawazishwa  na Alex Telles kisha bao la ushindi likawekwa kimiani na mnyama Ronaldo ambaye aliivunja rekodi ya Iker Casillas aliyekuwa anashikilia rekodi ya kuwa nyota ambaye amecheza mechi nyingi za Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kucheza mechi 177 huku mshikaji wake Lionel Messi ambaye yupo PSG amecheza mechi 151 akiwa ni namba tatu. Mvunja rekodi huyo ameifanya United kukusanya pointi tatu kwa

VIDEO:KOCHA YANGA ATAMBA KUWA YEYE NI MTU WA KAZI SIO MANENOMANENO

Image
NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amebainisha kuwa yeye ni mtu wa kazi hasa uwanjani na sio manenomaneno kwa kuwa kati ya vitu ambavyo hapendi ni kuzungumza maneno mengi.   Pia amebainisha kuwa kwa namna ambavyo anakitambua kikosi cha Yanga anauhakika kuwa timu hiyo itakuja kuwa kubwa ndani ya Afrika licha ya kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika.  Kuhusu suala la matokeo uwanjani Nabi amesema kuwa hana uwezo wa kutabiri bali hilo anayejua ni Mungu.   

SIMULIZI YA MCHUUZI ALIYEKUWA AKIPATA TABU KUTOKA POLISI

Image
SIMULIZI ya mchuuzi aliyekuwa akipata tabu kutoka Polisi Ama kwa hakika iwapo huna bahati isiyo nzuri basi  unaweza kuwaza nini kinaweza kuwa suluhisho kamili  kwa yale yanayokukumba kwa wakati wowote ule.  Nilikuwa mchuuzi Nairobi  ambapo nilikuwa nauza vitu kadhaa vya urembo kwenye maeneo yaliyokuwa na watu wengi  yakiwemo maeneo ya magari yaani stendi, vilabu na sehemu nyinginezo. Hii ndio ilikuwa kazi ambayo  ilinilisha mimi na mwanagu kwani nilikuwa naishi bila mume wangu tuliyekosana naye miaka  miwili iliyopita.  Maisha yalikuwa magumu kweli kwenye biashara hii niliyofanya kwani  changamoto zilikuwa ni nyingi sana. Kila wakati nilikuwa kwenye mikono ya polisi hata wakati  mwingine sikujua ni jambo ama ni makosa yapi nilikuwa nimefanya. Nilikuwa nalipa kiasi cha pesa nyingi ili kuachiliwa lakini baada tena ya siku kadhaa nilikuwa tena  kwa mikono ya askari. Suala hili lilinishangaza kwani sikuamini jinsi mambo haya  yalivyokuwa yakitendeka. Ama kwa hakika sikuwa na bahati n

GOMES AKUBALI MUZIKI WA WATANI ZAO WA JADI

Image
 KOCHA wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa Yanga walistahili kushinda mechi ya Ngao ya Jamii kwa sababu walitengeneza nafasi moja na wakaitumia tofauti na wao, huku akisifu usajili wao. Simba walipoteza kwa kuchapwa bao 1-0 na Yanga kwenye mchezo mkali uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam. Yanga walijipatia bao lao kupitia Fiston Mayele dakika ya 11 baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Farid Mussa. Gomes alifunguka kuwa, kwenye mchezo wowote ambao kombe linakuwa mbele ni lazima timu moja ishinde na nyingine ipoteze na bahati mbaya haikuwa siku yao, Yanga wakashinda mchezo. “Nawapongeza wachezaji wangu walicheza vizuri, lakini Yanga walipata nafasi na wakaitumia. “Wamefanya usajili mzuri na wanatimu nzuri sana msimu huu, tunakwenda kujipanga na ligi kwa kuwa tunafahamu kuwa itakuwa ngumu,” alisema kocha huyo. Gomes ameingia kwenye orodha ya makocha ambao wamepoteza mechi mbili kati ya tatu za Simba na Yanga ambazo zimechezwa ndani ya mwaka mmoja akiwa kama kocha

ALIYEIMALIZA SIMBA KWA MKAPA APANIA KUFUNGA SANA

Image
 MSHAMBULIAJI  Fiston Mayele, amesema kuwa anahitaji kufunga sana kwenye mechi zake zote ambazo atacheza kwa kuwa kazi yake ni mpira na anajua furaha ya mashabiki ipo kwenye ushindi. Mayele yupo kwenye kitabu cha kumbukumbu baada ya kuwa mfungaji wa bao pekee la ushindi kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, Septemba 25, Uwanja wa Mkapa ambapo alimtungua Aishi Manula kwa pasi ya Farid Mussa. Nyota huyo amesema ana furaha kubwa kufunga bao katika dabi yake ya kwanza aliyoicheza msimu huu, huku akiahidi kuendelea kufunga katika Ligi Kuu Bara na mashindano mengine. “Kuwafunga Simba siyo kama nimebahatisha, nimezoea kufanya hivyo kwenye dabi kwani nyumbani nikiwa na AS Vita nilishacheza dabi ambayo ni ngumu na yenye ushindani kama hii ya Simba dhidi ya Yanga. “Kikubwa ninafurahia kufunga bao langu la kwanza la mashindano nikiwa na Yanga, ambalo limetupa Ngao ya Jamii. “Niwaahidi mashabiki wa Yanga kwa kuwaambia kuwa furaha kubwa inakuja, ninafahamu ligi ni ngumu lakini nita

BONDIA MANNY PACQUIAO ASTAAFU, NGUVU ZAKE AZIHAMISHIA HUKU

Image
  BONDIA maarufu duniani kutoka nchini Ufilipino, Manny Pacquiao ametangaza kustaafu mchezo huo ili kuangazia kazi yake ya siasa.   Bondia huyo anayeshikilia mataji ya uzani tofauti ni seneta nchini humo na tayari ametangaza nia yake ya kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka 2022.   Katika pigano lake la mwisho bondia huyu mwenye umri wa miaka 42 alishindwa na bondia wa Cuba, Yordenis Ugas mjini Las Vegas mwezi uliopita.  “Nilisikia kengele ya mwisho tu. Mchezo ulikua umeisha,” alisema Pacquiao.   Katika video iliyowekwa kusambaa mitandao ya kijamii, Pacquiao alielezea kustaafu kwake kama “Uamuzi mgumu” katika maisha yake, akiongeza kuwa ndondi ilimpatia “nafasi ya kupigana na umaskini” na “ujasiri wa kubadilisha maisha zaidi”.   Pia aliwashukuru mashabiki wake, marafiki na wale wote waliomuunga mkono katika mchezo huo,hususa ni Mkufunzi wake wa muda mrefu Freddie Roach, ambaye alimtaja kama “familia yangu, kaka na rafiki. Sitasahau kile nilichofanya na kufanikisha maishani

KAZI IMEANZA UPYA, BALAA LIPO HAPA NDANI YA LIGI BONGO

Image
ZILE shangwe za mashabiki ambazo zilikuwa zinazunguka kwenye vichwa vya wachezaji na purukushani za mashabiki kupata burudani sasa zimerejea. Vita kubwa inaendelea pale ambapo iliishia msimu uliopita wa 2020/21 uliokuwa na ushindani mkubwa hivyo ni suala la kusubiri nani atakuwa nani baada ya msimu kukamilika. Hapa Spoti Xtra inakuletea namna vita itakavyoanza upya kwa msimu ndani ya ligi ambayo ilianza kutimua vumbi Septemba 27 baada ya mchezo wa ufunguzi wa ligi ule wa Ngao ya Jamii kuchezwa na ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Simba 0-1 Yanga:- Kiatu cha ufungaji bora Mbio hizi kwa msimu wa 2020/21 zilipamba moto na mwisho wa siku ziliangukia kwenye miguu ya nyota wa Simba, John Bocco ambaye alifunga jumla ya mabao 16. Licha ya kwamba alikuwa ni namba moja bado waliomfuatia ndani ya tatu bora walikuwa sio haba, alikuwa ni Chris Mugalu huyu alitupia mabao 15 yupo Simba na namba tatu ilikuwa kwenye miguu ya Prince Dube yupo zake Azam FC. Nyota wa Simba kwa sasa wote wapo fiti

DULLY HANA TATIZO NA HARMO

Image
 LEGEND wa BongoFleva, Dully Sykes ‘Brotherman’ amesema kuwa Harmonize ni kijana wake kama walivyo vijana wake wengine na hana tatizo naye kama inavyochukuliwa na watu. Nyota huyo ni Mwanapinduzi kwenye suala la muziki wa Tanzania kutokana na kazi zake nyingi kufanya vizuri na amekuwa ni mshauri kwa wasanii wengine kufanya kazi zao kwa ubunifu. Kazi zake zimekuwa zikiishi na hata anapopewa nafasi ya kushirikishwa bado amekuwa akifanya poa jambo linalofanya azidi kuwe kwenye ramani ya muziki. Kazi yake ya Bongo Fleva bado inaishi licha ya kuwa ni ngoma ya muda mrefu pia ile ya Hunifahamu bado inasumbua vichwa vya wengi. Pia ngoma yake ya Dhahabu ni moja ya kazi nzuri na ilimpa mafanikio makubwa Afrika Mashariki na kati na duniani pia.   Dully Sykes ameongeza kusema baadhi ya watu mitaani na mitandaoni ndio wanasababisha maneno na story zinazoendelea ila kwao hawana tatizo lolote na ikitokea kufanya kazi nyingine na Harmonize wataifanya.

VIDEO:HUYU HAPA MO AKIZUNGUMZIA ISHU YA KUJIENGUA SIMBA,SABABU HIZI HAPA

Image
MOHAMED Dewji, 'Mo', Mkurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Klabu ya Simba ameweka wazi kuwa kwa sasa atabaki kuwa Mwanahisa ndani ya timu hiyo baada ya kukubaliana na Bodi kwamba anaweza kustep down, (kukaa pembeni) kwenye nafasi hiyo.    Mo amesema kuwa sababu kubwa ambayo imemfanya akajiengua ni kutokuwa na muda kwa kuwa amekuwa akisafiri mara kwa mara hivyo nafasi hiyo itakuwa mikononi mwa Salim Abdalah, 'Tryagain'.   Mo amebainisha pia mafanikio ambayo wameyapata kwa muda wa miaka minne ikiwa ni ile ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara nne pamoja na kuweza kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika huku akisistiza kwamba bado anaipenda Simba na yupo Simba.  

HII HAPA RATIBA YA LIGI KUU BARA LEO

Image
  LEO Septemba 29, Ligi Kuu Bara inaendelea ambapo ni mzunguko wa kwanza kwa timu kuingia uwanjani kusaka pointi tatu muhimu. Mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu Bara ni Simba ambao walitwaa msimu uliopita na walianza jana kusaka ushindi mbele ya Biashara United, Uwanja wa Karume na ngoma ilikuwa Biashara United 0-0 Simba. Kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi baada ya kutwaa Ngao ya Jamii Septemba 25 kiliposhinda bao 1-0 mbele ya Simba leo saa 10:00 jioni wanaanza mbio za kulisaka taji la 28 la Ligi kuu Tanzania bara kwa kucheza na Kagera Sugar katika Uwanja wa Kaitaba. Pia saa 8:00 mchana Polisi Tanzania wao watamenyana na KMC katika mchezo wa kwanza kwa timu hizo. Mechi zote zitakuwa mubashara Azam TV.

BREAKING:MO DEWJI AJIENGUA SIMBA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI

Image
BREAKING:MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Klabu ya Simba, Mohamed Dewji ameamua kukaa pembeni kwenye nafasi hiyo kutokana na makubaliano ya Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Simba. Taarifa ambayo ameituma Mo amesema kuwa:"Miaka minne tumepata mafanikio makubwa,tumeshinda ligi mara nne kufanya vizuri Champion League,(Ligi ya Mabingwa Afrika). "Bado ninaipenda Simba. Tumefanya mkutano wa bodi tarehe 21,9,2021 tumekubaliana kwamba mimi nitastep down, (kuwa pembeni) kuwa chairman (mwenyekiti) Simba SC. "Ninaomba wanachama wa Simba msifikirie mimi ninaondoka kwenye Simba, mimi bado ni mwanahisa, ninaipenda Simba, tumekubaliana kufanya hivyo kwa sababu mimi nimekuwa ninasafiri sana," .

KAGERA SUGAR YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA YANGA

Image
  FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar ameweka wazi kuwa wanahitaji pointi tatu leo Septemba 29 mbele ya Yanga. Kagera Sugar ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Kaitaba. Baraza amesema kuwa anatambua mchezo wa leo utakuwa mgumu ila watapambana kupata pointi tatu muhimu. "Ni mchezo mgumu na ushindani mkubwa kwa kila timu lakini kikubwa ni kuona kwamba tunapata pointi tatu muhimu. "Wachezaji wapo tayari na wanajua kwamba mchezo hautakuwa mgumu, mashabiki wajitokeze kuwa nasi bega kwa bega kwani mchezo wa mwanzo unahitaji kushinda ili kujenga hali ya kujiamini," amesema. Msimu wa 2020/21 walipokutana Uwanja wa Kaitaba, ubao ulisoma Kagera Sugar 0-1 Yanga na mtupiaji alikuwa ni Tonombe Mukoko ambaye leo ataukosa mchezo kwa kuwa anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopata kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho mbele ya Simba.

YANGA YAZINDUA TAWI JIPYA KAGERA

Image
    UONGOZI wa Yanga umeweza kuzindua tawi jipya huko Kagera ikiwa ni katika hafla fupi iliyofanyika jana, Septemba 28, Ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha ambaye aliongoza na Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara pamoja na mkuu wa msafara, Salim Rupia. Tawi hilo jipya linaitwa Missenyi lipo wilaya ya Missenyi Mkoa wa Kagera. Kikosi hicho ambacho kinanolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi leo kina kazi ya kusaka pointi tatu muhimu mbele ya Kagera Sugar. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa saa 10:00 jioni, Uwanja wa Kaiataba. Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa tawi hilo.

AZAM FC WAWEKA KAMBI KILIMANJARO

Image
  MABOSI wa Dar es Salaam, Azam FC kwa sasa wapo ndani ya ardhi ya Kilimanjaro kwa ajili ya kufanya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania. Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Polisi Tanzania. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumamosi,Oktoba 2,2021 ikiwa ni kwa ajili ya msimu wa 2021/22. Azam FC wanaingia kwenye mchezo wa pili wakiwa na kumbukumbu ya kugawana pointi mbele ya Coastal Union kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja Mkwakwani.  

BAADA YA KICHAPO MBELE YA PSG, CITY KWENDA KULA NA KUPUMZIKA

Image
PEP Guardiola,  Kocha Mkuu wa Manchester City amesema kuwa kupoteza kwao mchezo wa Ligi ya Mabingwa mbele ya PSG ni moja ya vipindi ambavyo vinatokea kwenye mpira hivyo wanakwenda kula vizuri na kupumzika kwa ajili ya mchezo wao ujao dhidi ya Liverpool. City ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya PSG kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya jambo ambalo limewafanya wawe nafasi ya tatu kwenye kundi A na pointi zao ni tatu vinara ni PSG wenye pointi nne wote wakiwa wamecheza mechi mbili. Guardiola amesema kuwa walicheza kwa mbinu za kusaka ushindi ila kilichotokea ni uimara wa kipa wa PSG, Gianluigi Donnaruma ambaye alifanya kazi kubwa kwenye kuokoa hatari za wachezaji wake.  "Tulikuwa tunahitaji ushindi na tumecheza namna hiyo ila ni sehemu ya matokeo na huwa inatokea kwenye mpira lakini yule kipa wa PSG Donnaruma alifanya kazi yake kwa kuokoa hatari nyingi. "Kwa matokeo ambayo yametokea hamna namna tunakwenda kupumzika vizuri, kutafuta chakula na kula vizuri pamoja na

VIDEO: SABABU ZA WACHEZAJI WA YANGA KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA KAGERA SUGAR

Image
LEO Septemba 29, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa Uwanja wa Kaitaba,Kagera. Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Habari Yanga, Hassan Bumbuli amebainisha kuwa wapo nyota ambao watakosekana katika mchezo wa leo kutokana na sababu mbalimbali.   Miongoni mwa nyota hao ni pamoja na Said Ntibanzokiza, Mapinduzi Balama pamoja na Mukoko Tonombe pia ameweka wazi kwamba wanahitaji ushindi mbele ya Kagera Sugar kwa kuwa wana rekodi nzuri wakiwa Kaitaba.  

SIMBA: HAIKUWA BAHATI YETU,WACHEZAJI WALIPAMBANA

Image
  BAADA ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba kubanwa mbavu mbele ya Biashara United wamebainisha kuwa walipambana kusaka ushindi ila haikuwa bahati yao. Katika mchezo wa kwanza wa msimu wa 2021/22 uliochezwa Uwanja wa Karume,Mara, mbele ya mashabiki wengi waliojitokeza ubao ulisoma Biashara United 0-0 Simba. Unakuwa ni mwanzo wa kipekee kwa Simba ambao msimu wa 2020/21 mchezo wao wa kwanza walishinda kwa mabao 2-1 mbele ya Ihefu ambayo kwa sasa inashiriki Championship ila jana Septemba 28 waligawana pointi mojamoja na Biashara United. Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa haikuwa bahati yao kushinda licha ya kupambana kusaka ushindi. "Haikuwa bahati yetu, wachezaji walipambana kwa namna ambavyo wanaweza lakini tumeshindwa kushinda, matokeo tunayachukua tutafanya kazi mchezo ujao kwani ligi inaanza na kila timu inahitaji ushindi,". Kituo kinachofuata kwa Simba ni dhidi ya Dodoma Jiji inayonolewa na mzawa Mbwana Makata.  Mchezo huo unatarajiwa

VIDEO:KOCHA BIASHARA UNITED ABAINISHA WALIKUWA WANAZITAKA POINTI TATU ZA SIMBA

Image
KOCHA wa Biashara United ya Mara ameweka wazi kuwa walikuwa wanahitaji pointi tatu mbele ya Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Karume ila kwa walichokipata wanashukuru Mungu kwani mchezo ulikuwa na ushindani na timu zote zilikuwa zinahitaji ushindi.  

MESSI ATUPIA KWA MARA YA KWANZA PSG

Image
  LIONEL Messi nyota mpya ndani ya kikosi cha Paris Saint-Germain, (PSG) amefunga bao lake la kwanza akiwa na timu hiyo baada ya kuibuka hapo akitokea ndani ya kikosi cha Barcelona. Ilikuwa ni kwenye Uwanja wa Parc des Princes mbele ya mashabiki 37,350 ambao walihudhuria kutazama mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na PSG ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Manchester City. Ni mabao ya Idrissa Gueye dakika ya 8 na Messi aliweza kupachika bao lake la kwanza dakika ya 74 yamewafanya PSG wawe namba moja katika kundi A huku Manchester City wakiwa nafasi ya tatu. Ikumbukwe kwamba Messi alishindwa kufurukuta katika mechi tatu ambazo alicheza ndani ya PSG chini ya Kocha Mkuu, Mauricio Pochettino na bao lake hilo linamfanya afikishe jumla ya mabao 673 katika ngazi ya klabu Kwenye mchezo huo ni Gianluigi Donnaruma kipa wa PSG alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo.Pia inakuwa ni kichapo cha kwanza kwa Manchester City kwa hivi karibuni katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuwa mara ya mwish

VIDEO:BIASHARA UNITED WAWACHAMBUA NYOTA WAPYA WA SIMBA

Image
MASHABIKI wa Biashara United wameweka wazi kuwa walikuwa wanahitaji ushindi mbele ya Simba ila ilikuwa ngumu kwao kwa kuwa waliamua kuwahurumia Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Karume, Mara. Pia wamewachambua nyota wapya wa Simba wakimtaja Yusuph Mhilu kuwa miongoni mwa wachezaji wenye uwezo mkubwa huku wengine ikiwa ni majina tu.  

KUMBE BAO LA MAYELE KWA SIMBA LILIPIKWA NA MATAIFA MATATU

Image
 MATAIFA matatu yalihusika kulipika bao pekee la ushindi lililofungwa na nyota wa Yanga, Fiston Mayele ambaye alizima furaha ya Simba kutetea taji la Ngao ya Jamii. Ilikuwa Septemba 25, Uwanja wa Mkapa ambapo kazi ilianza kwenye miguu ya taifa la Mali ambaye ni kipa Diarra Djigui aliyepiga pasi ndefu iliyokutana na Mtanzania, Farid Mussa. Utundu wa Mussa katika kuwakwepa mabeki wa Simba wakiongozwa na Pascal Wawa ulimfanya shuti lake likutane na Mayele raia wa Congo ambaye alimtungua Aishi Manula. Mbali na shuti hilo kumshinda Manula pia mpira huo uliweka rekodi kwa kuguswa zaidi na mguu wa kulia ambapo kuanzia kwa nahodha Bakari Mwanyeto ambaye alimrudisha kipa wake Diarra aliyepiga pasi ndefu wote walitumia mguu wa kulia, hata mtoa pasi pia na mfungaji wote walitumia mguu wa kulia. Ni bao la kwanza la Mayele kwenye mechi ya ushindani kufunga na alimtungua kipa bora wa msimu uliopita Aishi Manula ambaye alisepa na tuzo ya kipa bora baada ya kukusanya clean sheet 18. Leo Ya

VIDEO:TAZAMA NAMNA KIPA WA BIASHARA UNITED ALIVYOPEWA MKWANJA

Image
BAADA ya kipa namba moja wa Biashara United, James Ssetupa kutimiza majukumu yake kwenye mchezo wa jana Septemba 28 dhidi ya Simba uliochezwa Uwanja wa Karume, Mara alipewa fedha za kutosha kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi.  

VIDEO:KIPA ALIYEIOKOA PENALTI YA BOCCO ATAJA KILICHOMBEBA

Image
JAMES Ssetupa kipa namba moja wa Biashara United amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa kumpa nguvu ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba uliochezwa Uwanja wa Karume, Mara ambapo aliweza kuikoa penalti ya nahodha wa Simba, John Bocco na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.  

VIDEO:SHABIKI YANGA ACHEKELEA SIMBA KULAZIMISHA SARE NA BIASHARA UNITED

Image
SHABIKI wa Yanga amesema kuwa amefurahi kuona timu hiyo imelazimisha sare ya bila kufungana na Biashara United kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa jana Uwanja wa Karume, Mara.  

VIDEO:NYOTA WA BIASHARA UNITED WAFUNGUKA BAADA YA KUGAWANA POINTI MOJAMOJA NA SIMBA

Image
NAHODHA wa Biashara United, Abdulmajid Mangalo amesema kuwa walikuwa na mchezo mgumu katika kazi yao ya kusaka ushindi mbele ya Simba kwenye mchezo uliochezwa Uwanja Karume ,Mara ambapo ulikamilika kwa timu hizo kutofungana na kugawana pointi mojamoja.   

HIZI HAPA REKODI ZA MWANZO LIGI KUU BARA

Image
 SHUGHULI imeanza upya kwa timu za Lifi Kuu Bara kusa ushindi kwenye mechi ambazo wanazicheza ikiwa ni msimu mpya wa 2021/22 na tayari rekodi tamu zimeanza kuandikwa kwenye mechi za ufunguzi. Mechi ya kwanza kwa msimu wa 2021/22 iliwakutanisha mabosi kutoka Morogoro ambao ni Mtibwa Sugar ilikuwa Uwanja wa Mabatini, Kibaha dhidi ya Mbeya Kwanza ambayo ni msimu wake wa kwanza kushiriki ligi baada ya kupanda daraja. Katika mechi hiyo iliandikwa rekodi ya kuwa mechi ya kwanza ambayo ilikusanya bao la kwanza dakika ya 49 kwa shuti kali akiwa ndani ya 18 akitumia mguu wake wa kushoto kupachika bao hilo. Mtupiaji alikuwa ni Willy Edgar na kipa aliyemtungua kwa mara ya kwanza ndani ya ligi ni kipa namba moja wa Mtibwa Sugar ni Aboutwalib Mshery ambaye kwa msimu wa 2020/21 alikusanya jumla ya clean sheet 14. Mbali na rekodi hiyo iliyowekwa ndani ya dakika 90 kwenye mchezo wa kwanza pia kuna rekodi nyingine ambayo iliwekwa na nyota wa Namungo FC, Obrey Chirwa kuwa ni namba moja kwa kutenge