NYOTA WA SIMBA CHAMA MIKONONI MWA YANGA
MEFAHAMIKA kuwa, Yanga imemalizana kwa siri na kiungo mchezeshaji wa Simba, Mzambia, Clatous Chama huku ikimfanyia kufuru kubwa nyota huyo. Mzambia huyo ambaye ni kipenzi cha Simba, kama kila kitu kitaenda sawa, basi atatua kuichezea Yanga kuanzia msimu ujao ikiwa ni baada ya mkataba wake wa miaka miwili ndani ya Simba kumalizika. Kiungo huyo alikuwa kwenye mipango ya muda mrefu ya kusajiliwa na Yanga ikiwemo katika usajili mkubwa msimu huu, lakini mkataba wake ndiyo ulizuia mipango hiyo kukamilika. Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, Kampuni ya GSM ambao ndiyo wanaofanikisha usajili Yanga, wamefanya kufuru kubwa Chama ya kumjenga nyumba ya kisasa na kifahari nyumbani kwao Zambia. Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, GSM imemjengea nyumba kiungo huyo katika sehemu ya masharti aliyowapa matajiri hao huku akiomba dau kubwa la usajili ambalo huenda likaweka rekodi. Aliongeza kuwa, pia kiungo huyo ameahidiwa gari la kutembelea la kifahari atakalolit...