ISHU YA MEDDIE KAGERE NA KOCHA MKUU SIMBA IMEKAA HIVI


 KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa hana tatizo na mshambuliaji namba moja wa kikosi hicho Meddie Kagere.

Imekuwa ikielezwa kuwa Sven na Kagere hawaivi chungu kimoja jambo ambalo lilikuwa likimfanya amsotesha benchi nyota huyo ndani ya kikosi cha Simba.

Tayari kwa sasa ameanza kumtumia nyota huyo ambaye ametupia jumla ya mabao saba ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.

Jana, Uwanja wa Mkapa wakati Simba ikishinda mabao 4-0 dhidi ya Ihefu FC alitupia mabao mawili na kutimiza majukumu yake ndani ya uwanja.

Sven amesema:"Sijui haya aneno huwa yanatoka wapi ila ninachojua mimi ni kwamba kila mchezaji ndani ya kikosi cha Simba ni muhimu na wote ninafanya nao mazungumzo.


“Wachezaji wangu kwa asilimia kubwa wanapambana na sitaki kuona kwamba wanakuwa wanakosolewa kwa namna yoyote ile. Lawama zao zote lazima zije kwangu na isiwe kwao.


"Sina ugomvi na mchezaji na siwezi kumhukumu kwa masuala ya nje ya uwanja mimi ninachohitaji ni kuona kwamba kila mmoja anatimiza majukumu ndani ya uwanja," .






Comments

Popular posts from this blog

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA