OLE GUNANAR ATAMBA KUENDELEZA DOZI


 KOCHA Mkuu wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, amesema kuwa anaamini timu yake inaweza kuifunga timu yoyote kwa sasa.

 

Manchester United wamekuwa wakionesha kiwango cha juu kwa siku za hivi karibuni na sasa wanashika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu England.

 

United ilifanikiwa kuichapa Wolves bao 1-0 na kuendelea kufanya vizuri kwenye michezo ya ligi hiyo ikiwa inaufukuzia ubingwa kwa sasa baada ya kucheza michezo 15.

 

Solskjaer amesema:"Haya matokeo ni bora sana kwetu, Man United kwa sasa ina morali ya hali ya juu na hicho ndicho kinasaidia.


“Kwa sasa tupo tofauti, wachezaji wanaamini wanaweza kumfunga yeyote.

 

"Ni mapema sana kusema kuhusu ubingwa kwa kuwa tumecheza michezo 15 tu, ni jambo ambalo tunaweza kulifikiria kuanzia Machi mwakani,” amesema Solskjaer.


Ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 30 kinara ni Liverpool mwenye pointi 33. Leo United inacheza na Aston Villa, Uwanja wa Old Trafford.



Comments

Popular posts from this blog

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA