ARTETA AGOMA KUBADILI MPANGO WAKE KWENYE USAJILI

 


MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa ushindi wa mechi mbili mfululizo ndani ya Ligi Kuu England hautabadilisha mpango wa yeye kuhitaji kuboresha kikosi chake.

Arteta ameongoza kikosi hicho kushinda mara mbili baada ya mchezo wake uliopita kushinda mabao 3-1 dhidi ya Chelsea na usiku wa kuamkia leo kushinda bao 1-0 dhidi ya Brighton.

Bao pekee la ushindi lilipachikwa na Alexandre Lacazette dakika ya 66 na kuifanya Arsenal kusepa mazima na pointi tatu Uwanja wa Falmer.

Arteta amesema:-"Matokeo ambayo tunayapata ndani ya ligi hayatabadilisha mpango wangu kwenye suala la usajili hivyo lazima mipango ikamilike.

"Tupo kwenye wakati mgumu kwa sasa ambao tunapitia na ratiba yetu ni ngumu, hivyo kushinda mara mbili haiwezi kubadili mpango wangu kuelekea kwenye dirisha la usajili" .



Comments

Popular posts from this blog

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA