MICHAEL SARPONG WA YANGA APOTEZWA NA KARIHE WA DODOMA JIJI




 SEIF Karihe, nyota wa kikosi cha Dodoma Jiji aliyemtungua Metacha Mnata kipa namba moja kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha amempoteza mshambuliaji wa Yanga, Michael Sarpong kwa idadi ya mabao.


Karihe alimtungua Mnata kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara wakati Yanga ikishinda kwa mabao 3-1 na kusepa na pointi tatu jumlajumla.

Karihe ametupia jumla ya mabao matano ndani ya ligi akimzidi bao moja nyota huyo Sarpong mwili jumba mwenye mabao manne ndani ya ligi.

Karihe ametupia mabao matano huku katika mabao hayo matano hajafunga bao hata moja kwa penalti ilikuwa ni jitihada zake binafsi za kusaka ushindi kwa timu yake.

Sarpong ametupia bao moja kwa mkwaju wa penalti ilikuwa Uwanja wa Mkapa, wakati Yanga ikitoshana nguvu ya kufungana bao 1-1 na Simba.



Comments

Popular posts from this blog

ISHU YA MORRISON KUHUSU MKATABA WAKE IPO MIKONONI MWA KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI

BREAKING: MASHABIKI RUKSA KWENDA UWANJANI, UTARATIBU WATAJWA

AFRICAN LYON WADAI KUWA WAZO LA VISIT TANZANIA NA LOGO MPYA YA SIMBA IMETOKA KWAO