ISHU YA KUTOLEWA KWA MKOPO, WATANO SIMBA WAWEKA MGOMO


IMEELEZWA kuwa nyota watano wa Klabu ya Simba ambao wapo kwenye hesabu za kutolewa kwa mkopo wameugomea uongozi kusepa ndani ya kikosi hicho.

Wachezaji wanaotajwa kutolewa kwa mkopo ni Kennedy Juma, Miraji Athumani ‘Sheva’, Charles Ilanfya, Ibrahim Ame na Ibrahim Ajibu ambao wamekosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

 

Simba imepanga kuwatoa wachezaji hao kwa mkopo baada ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji Sven Vandenbroeck, kupendekeza nyota hao kutolewa ili wakalinde vipaji vyao baada ya kukosa nafasi.


Habari zimeeleza kuwa wachezaji hao wamegoma kutolewa kwa mkopo kwa kuhofia kutelekezwa na timu hiyo.


Mtoa taarifa huyo aliwataja baadhi ya wachezaji waliogoma kutolewa kwa mkopo ni Kennedy, Ajibu, Sheva huku Ame akionekana kuwatega viongozi wengine wakipendekeza abakie hapo.


Aliongeza kuwa wachezaji waliobakishwa wakiwa katika hatua za mwisho za kutaka kutolewa kwa mkopo ni kiungo Francis Kahata na David Kameta ‘Duchu’ ambao wataendelea kubaki baada ya uongozi kufurahishwa na viwango vyao katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Majimaji FC.

 

"Simba imepanga kuwatoa wachezaji watano kwa mkopo katika dirisha dogo lililofunguliwa Desemba 16, mwaka huu ambao wote hao wamegoma kuondoka hadi mikataba yao itakapomalizika.

 

“Kati ya hao waligoma kuondoka kwa kuhofia kutelekezwa na viongozi wa timu hiyo, kwani mara wanapowatoa kwa mkopo ndiyo kama wamewaacha jumla, hivyo hawataki kusikia, ni bora wakaendelea kukaa hapo Simba,” alisema mtoa taarifa huyo.


Hivi karibuni Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez aliweka wazi kwamba wapo wachezaji ambao watatolewa kwa mkopo ndani ya kikosi hicho.



Comments

Popular posts from this blog

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA