Posts

Showing posts from August, 2020

NAMUNGO HESABU ZAO NDANI YA LIGI KUU BARA

Image
  HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa kwa sasa hesabu zake ni kwenye mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Septemba 6. Mchezo huo utakuwa ni wa kwanza kwa Namungo FC kwa msimu mpya wa 2020/21 ambao ulifunguliwa Agosti 30 kwa mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba na Namungo FC uliopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha. Mchezo huo Namungo FC ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 na yalijazwa kimiani na John Bocco kwa penalti dakika ya 7 na Bernard Morrison dakika ya 60. Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa kupoteza mchezo wao uliopita ni kutokana na makosa waliyofanya hivyo watarekebisha ili kuwa imara zaidi. "Mchezo wetu wa Ngao ya Jamii umeshapita hatuwezi kubadili matokeo.  Tunachofanya kwa sasa ni kuongeza nguvu kuelekea mechi zetu za Ligi Kuu Bara hakuna jambo jingine, " amesema. Msimu wa 2019/20, Namungo FC iliamaliza ikiwa nafasi ya nne kibindoni ilikuwa na pointi 64 baada ya kucheza mechi 38.

KIKOSI CHA SIMBA KUIFUATA IHEFU LEO MBEYA

Image
  KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji, leo Septemba Mosi kinatarajiwa kuanza safari kuelekea Mbeya kuifuata Ihefu FC. Simba iliweka ngome mkoani Arusha tangu Agosti 28 ambapo ilitia timu siku ya Ijumaa kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Ngao ya Jamii uliochezwa Agosti 30,Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.  Kwenye mchezo huo ambao ulikuwa maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara,  Simba ilishinda mabao 2-0 yaliyofungwa na John Bocco dk ya 7 na Bernard Morrison dk ya 60. Wanaanza safari ya kutetea taji la Ligi Kuu Bara kwa kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya Ihefu Septemba 6 Uwanja wa Sokoine majira ya saa 10:00 jioni. Huu unakuwa mchezo wa kwanza kwa timu zote ndani ya msimu mpya wa 2020/21 huku Ihefu ikiwa ni msimu wake wa kwanza pia  kushiriki Ligi Kuu Bara baada ya kupanda kutoka Ligi Daraja la Kwanza.

KOCHA MPYA YANGA,:WACHEZAJI WAPO VIZURI, WANAHITAJI MUDA

Image
  ZLATKO Krmpotic,  Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga amesema kuwa amewaona wachezaji wake wakionyesha kiwango bora kwa kila mmoja ila wanahitaji muda wa kuzoeana zaidi. Zlatko, raia wa Serbia amesaini dili la miaka miwili kuinoa Yanga akichukua mikoba ya Luc Eymael raia wa Ubelgiji ambaye alifutwa kazi mazima Julai 27,2020. Alikishuhudia kikosi chake Agosti 30 kwenye kilele cha wiki ya Mwanachi ambapo Yanga ilishinda mabao 2-0 mbele ya Aigle Noir ya Burundi kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki. Mabao ya Yanga yalifungwa na Tuisila Kisinda dakika ya 38 kwa pasi ya Fei Toto na Michael Sarpong dakika ya 52 kwa pasi ya Ditram Nchimbi.  Kocha huyo amesema:"Nimewaona wachezaji kila mmoja ana kitu chake ila kwa kuwa ni mara yangu ya kwanza bado nina amini wanahitaji muda ili kuwa bora zaidi." Yanga itafungua pazia la mechi ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21 dhidi ya Tanzania Prisons,  Uwanja wa Mkapa, majira ya saa 1:00 usiku  Septemba 6.

MTIBWA SUGAR YAFUNGA KAZI NA MAJEMBE NANE

Image
  UONGOZI wa Mtibwa Sugar umefunga pazia la usajili kwa kusajili majembe mapya ya kazi nane kwa ajili ya msimu mpya wa 2020/21. Dirisha la Usajili lilifunguliwa rasmi Agosti Mosi na limefungwa Agosti 31. Limedumu kwa muda wa mwezi mmoja kutokana na janga la Virusi vya Corona kutibua mipango mingi. Hesabu kubwa za Klabu ya Mtibwa Sugar ni kuifuta rekodi mbovu ya msimu wa 2019/20 ambapo ilimaliza Ligi Kuu Bara ikiwa  nafasi ya 14 na pointi 45 jambo ambalo halikuwahi kuwakuta ndani ya misimu 10 mfululizo.  Nyota ambao imemalizana nao ni pamoja na beki wa kati Geoffrey Luseke na kiungo Juma Nyangi waliokuwa Alliance FC, Baraka Majogoro kiungo kutoka Polisi Tanzania, George Makanga kutoka Namungo. Abal Kassim kutoka Azam FC yeye ni kiungo, Hassan Kessy kutoka Nkana FC ya Zambia yeye ni beki wa kulia, Abubakari Ame yeye ni beki kutoka Klabu ya Malindi ya Zanzibar na Ibrahim Hamadi yeye ni mshambuliaji kutoka Klabu ya Zimamoto ya Zanzibar.

BIASHARA UNITED KUJA NA MOTO MKALI MSIMU WA 2020/21

Image
  FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Klabu ya Biashara United ya Mara amesema kuwa atahakikisha timu yake inakuwa moto wa kuotea mbali kwa msimu mpya wa 2020/21. Pazia la Ligi Kuu Bara linatarajiwa kuanza kutimua vumbi rasmi Septemba 6,2020 ambapo timu ya Biashara United itaanza kumenyana na Gwambina FC. Mchezo huo wa kwanza kwa Biashara United utawakutanisha dhidi ya Gwambina FC ambao wametoka kupanda daraja kwa msimu wa 2020/21. Baraza amesema:"Kuna wachezaji nane wameondoka na tumesajili wachezaji saba ndani ya kikosi hivyo katika hali ya kawaida hawa wanatakiwa kuzoeana ili kwenda na kasi. "Ligi ya msimu huu inatarajiwa kuwa ngumu kutokana na namna timu zinavyojipanga lakini sisi tupo tayari tutakuja kivingine na kasi nyingine." Msimu wa 2019/20, Biashara United ilimaliza ikiwa nafasi ya 9 baada ya kucheza mechi 38 na kibindoni ilikuwa na pointi 50.

BEKI BORA MSIMU WA 2019/20 APEWA TUZO NYINGINE TENA

Image
  UONGOZI wa Azam FC umempa tuzo nyingine tena beki bora wa msimu wa mwaka 2019/20 ndani ya Ligi Kuu Bara Nicolas Wadada.  Tuzo hiyo amepewa na Meneja Masoko wa Azam FC, Tunga Ally ikiwa ni sehemu ya kumpa pongezi kwa kuweza kufanya vizuri ndani ya msimu wa 2019/20. Wadada amekabidhiwa mchoro wa picha yake uliochorwa ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake kwa msimu uliopita. Beki huyo wa kulia aliwapoteza mazima Bakari Mwamnyeto wa Coastal Union na David Luhende wa Kagera Sugar aliotinga nao hatua ya fainali. Aliweza kuhusika kwenye jumla ya mabao 9 kati ya 52 yaliyofungwa na Azam FC msimu uliopita ambapo alifunga bao moja na kutoa pasi nane. Pia Wadada raia wa Uganda kwa msimu wa 2019/20,  alikabidhiwa tuzo nyingine ya kuwepo kwenye kikosi bora cha msimu wa 2019/20.

KOCHA MPYA WA BARCELONA AANZA MAZOEZI BILA YA MESSI

Image
RONALD Koeman, Kocha Mkuu wa Klabu ya Barcelona jana Agosti 31 alianza kukinoa kikosi chake kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2020/21 bila ya uwepo wa nyota wao Lionel Messi. Baada ya kufukuzwa kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo,  Quique Setien, Koeman alikabidhiwa mikoba ya kukinoa kikosi hicho ambacho kilitoka kupokea kichapo cha udhalilishaji cha mabao 8-2 mbele ya Bayern Munich kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.  Picha ambazo zilipigwa na kuwachukua wachezaji ambao walikuwa wameanza mazoezi zilimuonyesha kocha huyo akiwa na baadhi ya wachezaji ambao wanajiandaa na kuanza kwa La Liga huku Messi akiwa hayupo. Wachezaji wa Barcelona walipigwa picha wakiwa mazoezini ambapo winga Ousmane Demebele alionekana akikimbia huku akitumia vifaa vipya vya mazoezi vya timu hiyo.  Pia,  Gerard Pique alionekana akiwa na mpira akichezea kwenye mazoezi hayo ambayo yalifanyika bila ya uwepo wa Messi ambaye inaelezwa kuwa anahitaji kuondoka ndani ya timu hiyo na inatajwa kuwa anahita

AFC YAFUNGWA MABAO 6-0 NA SIMBA, LUIS MIQUSSONE ATUPIA MATATU

Image
  KIKOSI cha Simba, leo Agosti 31 kimeibuka na ushindi wa mabao 6-0 mbele ya AFC kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.  Mabao ya Simba yalifungwa na Meddie Kagere dakika ya nne kwa pasi ya Ibrahim Ajibu ndani ya 18, bao la pili lilifungwa na Larry Bwalya dakika ya 24 kwa pasi ya Ajibu na bao la tatu lilifungwa na Kagere dakika ya 34 kwa pasi ya Gadiel Michael.  Mpaka muda wa mapumziko Simba ilikuwa mbele kwa mabao 3-0 huku AFC ikiwa haijaambulia bao ndani ya dakika 45. Kipindi cha pili Simba ilipachika mabao mengine matatu kupitia kwa kiungo wao Luis Miqussone aliyefunga 'hat trick' ambapo alifunga bao la nne dakika ya 64  kwa shuti la nje ya 18 baada ya kipa wa AFC kutema mpira. Bao la tano lilipachikwa dakika ya 76 kwa pasi ya Said Ndemla na kuzamisha bao kambani na bao la sita lilipachikwa dakika ya 88 baada ya mabeki wa AFC kujichanganya namna ya kukaba. Simba wanajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu unaotarajiwa

UNITED YATAKA SAINI YA BEKI WA RB LEIPZING KUMUONGEZEA NGUVU MAGUIRE

Image
IMEELEZWA kuwa Manchester United ipo kwenye mpango wa kuinasa saini ya beki wa Klabu ya RB Leipzig, Dayot Upamecano kwa ajili ya kuongeza nguvu msimu ujao wa 2020/21. Kocha Mkuu wa United,  Ole Gunnar Solskjaer yupo kwenye mpango wa kuboresha safu yake ya ulinzi ambayo imekuwa kwenye tatizo la umakini kwa msimu wa 2019/20 Lengo la kocha wa United  ni kumuongezea nguvu nahodha wa kikosi hicho, Harry Maguire ambaye ndiye tegemeo kwa upande wa ulinzi ndani ya kikosi hicho. Kwa mujibu wa   ESPN , Solskjaer anaamini kwamba atakamilisha dili hilo mapema kabla ya  Oktoba 5.  Tayari nyota huyo mwenye miaka 21 anayeshiriki Ligi ya Bundesliga amesaini mkataba mpya na timu yake ambayo ilitiga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya kutolewa na PSG ya Ujerumani hivyo italazimika kutoa pauni milioni 53 kwa ajli ya ada ya kumpata nyota huyo .

MSIMU MPYA TUNAHITAJI SOKA LA USHINDANI, MALALAMIKO YAWEKWE KANDO

Image
  LEO Jumatatu saa 5:59 usiku dirisha la usajili litafungwa rasmi kwa hapa nchini ikihitimisha kipindi cha mwezi mzima cha timu kupewa kibali cha kusajili wachezaji wawatakao.   Baada ya kupita kwa kipindi hicho, ligi kuu rasmi sasa inaenda kuanza ambapo timu zote 18 zitakuwa na kibarua cha kugombea ubingwa ambao upo mikononi mwa Simba.   Tumeona Simba ambao jana walikuwa wanacheza mechi ya Ngao ya Jamii na Namungo, wametawala soka la Bongo kwa misimu mitatu mfululizo hii inaonyesha kuwa walijiandaa haswa.   Na msimu ujao pia utaona kama wamepania kuchukua taji la nne kama wapinzani wao wataendelea kuongea zaidi bila kupambana uwanjani.   Ninaamini kila timu imesajili kulingana na upungufu waliouona kupitia michuano mbalimbali ambayo walishiriki msimu uliopita. Hivyo mpaka sasa maana yake kila kitu kiko sawa kwa ajili ya msimu ujao ambao ninaamini utakuwa na ushindani mkubwa haswa kwa kuwa timu zimetoka kujaza ‘mafuta’ hivyo tenki sasa limejaa.   Sasa msimu ujao tunataka k

MANE ANUKIA BARCELONA

Image
 SADIO Mane nyota wa Klabu ya Liverpool anatajwa kuingia anga za Klabu ya Barcelona ili kuziba pengo la mshambuliaji wao namba moja Lionel Messi ambaye anatajwa kutaka kuondoka ndani ya kikosi hicho. Mane raia wa Senegal  amekuwa chachu kubwa ya mafanikio ndani ya Liverpool ambayo msimu wa 2019/20 ilitwaa taji la Ligi Kuu England baada ya kupita miaka 30 pia alikuwa kwenye kikosi kilichotwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Amekuwa akifanya kazi kwa ukaribu na nyota wa Liverpool raia wa Misri, Mohamed Salah pamoja na nyota mwingine Roberto Firmino wakiunda utatu wao matata ndani ya kikosi hicho kinachotumia Uwanja wa Anfield kwa mechi za nyumbani. Ripoti zinaeleza kuwa Mane anataka kwenda Barcelona ili akafanye kazi na kocha mpya wa klabu hiyo Ronald Koeman ambaye kwa sasa yupo ndani ya kikosi hicho kwa kuwa walifanya naye kazi alipokuwa akikinoa kikosi cha Southampton. Alipofanya kazi na kocha huyo Mane alifunga mabao 25 kwenye jumla ya mechi 75 alizocheza anaamini kwamaba akitua

MCHEZO MZIMA WA SIMBA KUTWAA NGAO YA JAMII ULIKUWA NAMNA HII

Image
  KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck jana Agosti 30 kilifanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii kwa kushinda mchezo wa fainali mbele ya Namungo FC kwa ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Timu zote mbili dakika tano za mwanzo zilianza kwa kasi na dakika ya nne, nahodha wa Simba John Bocco alikosa nafasi ya wazi kwa pasi kutoka kwa Hassan Dilunga ndani ya 18 na Clatous Chama naye alipiga shuti liliokolewa na mlinda mlango wa Namungo, Nurdin Barola. IIliwachukua dakika mbili Simba kupata bao la kuongoza lililofungwa dakika ya saba na Bocco kwa mkwaju wa penalti baada ya kiungo mshambuliaji wa Simba Bernard Morrison kuchezewa faulo ndani ya 18 na mchezaji wa Namungo, Steven Duah aliyeonyeshwa kadi ya njano dakika ya saba. Penalti hiyo iliwafanya wachezaji wa Namungo kumfuata mwamuzi wakionekana kumlalamikia ila hakubadili maamuzi yake. Baada ya Simba kupata bao waliacha kushambulia na kuanza kucheza kwa pasi nyingi kipindi ch

MCHEZO MZIMA WA YANGA KUINYOOSHA AIGLE NOIR KWA MKAPA ULICHEZWA HIVI

Image
 YANGA jana Agosti 30 Uwanja wa Mkapa ilihitimisha kilele cha wiki ya  Mwananchi kwa ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Klabu ya Aigle Noir ya Burundi. Mchezo huo ulishuhudiwa na mashabiki wengi waliojitokeza Uwanja wa Mkapa ulikuwa na ushindani mkubwa mwanzo mwisho kwa timu zote kucheza mpira wa darasani na mipango mingi ndani ya uwanja. Yanga ilianza kuandika bao la kwanza dakika ya 38 kupitia kwa ingizo jipya ndani ya kikosi hicho Tuisila Kisinda akimaliza pasi ya nyota mzawa Feisal Salum ambaye alikuwa ni nyota wa mchezo wa jana. Aigle walimaliza wakiwa pungufu baada ya mchezaji wao mmoja Koffi Kuassi kuonyesha kadi nyekundu dakika ya 40 baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano dakika ya 10 na ile ya pili ikamfanya mwamuzi asiwe na chaguzo zaidi ya kumuonyesha kadi nyekundu kutokana na kuwa na kadi mbili za njano. Licha ya wapinzani hao wa Yanga kuwa pungufu bado waliendelea kuwa imara kwa kucheza kwa utulivu huku mipango yao mingi ikiishia miguuni mwa Bakari Mwamnyeto beki mpya wa

DIRISHA LA USAJILI LINAFUNGWA LEO, WACHEZAJI WASIKURUPUKE KUMWAGA SAINI

ANAANDIKA HAJI MANARA AKIWAOMBA WATANZANIA WAMPE JAPO HESHIMA

Image
  OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amewaomba mashabiki na watanzania wampe heshima kabla hajatangulia mbele za haki kwa kuwa amefanya mengi makubwa kwa sasa katika kuutangaza mpira. Haji ameandika namna hii:-Watanzania nipeni heshima yangu walau kidogo, ntaumia sana nikifa mkaja kusoma salaam zenu makaburini kunielezea wasifu na sifa zangu,huku mkinipamba kwa tenzi na shairi nzuri nzuri. "Leo Yanga wametumia washehereshaji watano katika jambo ambalo nalifanya peke yangu always! "Mimi napenda heshima tu ,,msinisifu ila mtambue nimewachangamshia mpira wenu, waliokuwa baridi nimewafanya walau nao wachangamke,japo bado wanafanya uchale tu mbele ya Simba. "Wanasimba wenzangu tujishukuru kwa tulipo na wenzetu walipo,,.hawana chembe ya 'Creativity',(ubunifu),hawajui hata 'wat they want'(nini wanataka). "Hebu nyie na Watanzania wote nipeni japo heshima yangu na management ya Simba pamoja na Bodi ya Klabu chini ya tajiri wa mpira bwana MO kwa haya

MTIBWA SUGAR WAMEAMUA,YAMALIZANA NA MAJEMBE SITA YA KAZI

Image
  JUMA Nyangi, nyota wa zamani wa Klabu ya Alliance FC ya Mwanza anatimiza idadi ya nyota sita waliosajiliwa na Klabu ya Mtibwa Sugar. Nyangi alitambulishwa rasmi jana, Agosti 30 kwa kusaini kandarasi ya miaka miwili ndani ya kikosi cha wakata miwa cha Morogoro. Wachezaji wengine ambao tayari Mtibwa Sugar imemalizana nao ni pamoja na Abal Kassim kutoka Azam FC, Baraka Majogoro kutoka Polisi Tanzania,  George Makanga kutoka Namungo,Hassan Kessy kutoka Nkana FC na Geoffrey Luseke kutoka kutoka Alliance. Mtibwa Sugar ilimtambulisha jana Kessy ambaye ni beki wa kulia kwenda kuziba pengo la Shomari Kibwana aliyeibukia ndani ya Yanga. Nyota hao wataanza kuitumikia Mtibwa Sugar ndani ya msimu wa 2020/21 unaotarajiwa kuanza Septemba 6 kikiwa chini ya Kocha Mkuu,  Zuber Katwila.

SAKATA LA MORRISON KUIBUKA UPYA, SERIKALI YATOA USHAURI HUU YANGA

Image
  ALIYEKUWA Rais wa awamu ya nne wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ameishauri Yanga kuachana na mvutano wa suala la mchezaji, Bernard Morrison kwa kuwa wanapoteza muda na badala yake wawekeze nguvu kuibua vipaji vipya. Kikwete ameyasema hayo jana, Agosti 30 kwenye Kilele cha Wiki ya Mwananchi ampabo yeye alikuwa ni mgeni rasmi Uwanja wa Mkapa. Morrison amekuwa kwenye mvutano na Yanga kuhusu suala la mkataba, Yanga inaeleza kuwa ana mkataba wa miaka miwili huku Morrison akisema dili lake la miezi sita lilikwisha. Shauri hilo lilisikilizwa Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) na Kamati ya Hadhi ya Wachezaji Tanzania kwa muda wa siku tatu mfululizo kuanzia Agosti 10-12 na mwisho Morrison alitangazwa kuwa mshindi kwa kile kilichoelezwa kuwa kulikuwa na mapungufu kwenye mkataba. Kikwete amesema:"Naskika ninyi mwaka huu mmeibiwa mchezaji na majirani zenu,hilo ni jambo la kawaida kwani masuala haya kwa watani wa jadi hayajaanza le

AZAM FC V TANZANIA PRISONS NGOMA 1-1 PALE AZAM COMPLEX

Image
  KLABU ya Azam FC yenye maskani yake Chamazi, nje kidogo ya Dar es Salaam,  jana Agosti 30 ilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 na Klabu ya Tanzania Prisons.  Mchezo huo wa kirafiki ulichezwa Uwanja wa Azam Complex na malengo yake makubwa ni kujiweka fiti kwa ajili ya msimu mpya wa 2020/21. Msimu mpya unatarajiwa kuanza rasmi Septemba 6 baada ya jana Agosti 30 pazia kufunguliwa rasmi baada ya mchezo wa Ngao ya Jamii kuchezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kati ya Simba na Namungo. Kwenye mchezo huo Simba ilishinda mabao 2-0 na kusepa na taji la Ngao ya Jamii mbele ya wapinzani wake Namungo. Azam FC itafungua pazia Septemba 7 kwa mchezo dhidi ya Polisi Tanzania Uwanja wa Azam Complex huku Prisons ikianza na Yanga, Septemba 6,Uwanja wa Mkapa.

NAMNA SIMBA ILIVYOTWAA NGAO YA JAMII MARA NNE MFULULIZO

Image
  Namna Simba ilivyosepa na Ngao ya Jamii mara nne mfululizo:- 2017/18 Simba ilitwaa Ngao ya Jamii kwa kushinda mbele ya Yanga. 2018/19 Simba ilitwaa Ngao ya Jamii kwa ushindi mbele ya Mtibwa Sugar 2019/20 Simba ilishinda Ngao ya Jamii mbele ya Azam FC 2020/21 Simba ilishinda Ngao ya Jamii mbele ya Namungo FC.

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU

Image
  MUONEKANO wa Ukurasa wa mbele Gazeti la Championi 6

JEMBE LA YANGA JIPYA KUTUA LEO

Image
  MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga,Yacouba Sogne raia wa Burkina Faso anatarajiwa kutua nchini leo Agosti 31, akitokea nchini Burkina Faso.   Nyota huyo ilibidi atue nchini Agosti 27 na mashabiki wa Yanga walijitokeza kwa wingi Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere (JINA) ila alishindwa kutua na alikosa tamasha la Wananchi lililofanyika jana Uwanja wa Mkapa ambapo wachezaji wapya na jezi mpya ya Yanga kwa msimu wa 2020/21 ilitambulishwa.    Yacouba alimalizana na Yanga kwa dili la miaka miwili akitokea Asante Kotoko ya Ghana mara baada ya mkataba wake kuisha na anakuja akiwa ni mchezaji huru.   Kwa mujibu wa Mjumbe wa Kamati ya Usajili Yanga na Mkurugenzi Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said alisema kuwa ndege yake ilizuiliwa kutua nchini hivyo amekatiwa tiketi nyingine na atatoka kwao Burkina Faso Agosti 30.   Hersi alisema kuwa mshambuliaji huyo baada ya kutua nchini,  ataungana na kambi ya pamoja kwa ajili ya kuanza mazoezi ya pamoja kujiandaa na msimu mpya wa ligi na t

LIVE:YANGA 1-0 AIGLE NOR

Image
Dakika ya 38 Gooool, Tuisila Kisinda kwa pasi ya Fei Toto Dakika ya 38 Kaseke anakosa bao la wazi Dakika ya 36 mlinda mlango wa Aigle, Erick anapewa huduma ya kwanza Dakika ya 30, nyota wa Aigle, Koffi anaonyeshwa kadi ya pili ya njano na kufanya aonyeshwe kadi nyekudu, Dakika ya 23 Kibwana Shomari anamwaga maji yanakutana na mikono ya kipa wa Aigle  Dakika ya 20,Tuisila ndani ya 18 anampa Yassin Mustapha ambaye anamwaga maji yanakutana na kichwa cha Sarpong hakizai matunda Dakika ya 13 Aigle wanaanzisha mashambulizi kwenda Yanga Dakika ya 10 Koffi Kouassi wa Aigle alionyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea rafu Kisinda Dakika ya 3 Michael Sarpong alisababisha kona ambayo haikuzaa matunda  UWANJA wa Mkapa Mchezo wa kirafiki wa kimataifa Yanga 0-0 Aigle Noir

SIMBA YATWAA NGAO YA JAMII

Image
  KLABU ya simba, leo Agosti 30 imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Namungo FC na kufanikiwa kutwaa taji la Ngao ya Jamii kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha. Mabao ya Simba yalifungwa na nahodha wa timu hiyo, John Bocco kwa mkwaju wa penalti dakika ya saba baada ya Bernard Morrison kuchezewa faulo ndani ya 18. Bao hilo lilidumu mpaka dakika ya 59 ambapo Morrison alipachika bao la pili kipindi cha pili ndani ya 18 kwa pasi ya Clatous Chama. Ushindi huo unaifanya Simba kutwaa taji la Ngao ya Jamii kwa kushinda mbele ya Namungo FC inayonolewa na Hitimana Thiery. Nyota wapya wa Simba, Joash Onyango, Larry Bwalya walifanya kazi kubwa kupambana kwa kuonyesha uwezo wao ndani ya uwanja. Mchezo wa leo ni kifungua pazia kwa Ligi Kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 6. Namungo ilipambana kwa kasi kipindi cha kwanza ambapo ilikuwa ikiwatumia nyota wao ikiwa ni pamoja na Sixtus Sabilo, Stephen Sey na Abdluhum Humud,

SAKATA LA MORRISON LAIBUKA UPYA, YANGA WAMTAMBULISHA UWANJA WA MKAPA

Image
  UONGOZI wa Yanga umesema kuwa bado mchezaji wao wa zamani Bernard Morrison ni mali yao na wamemtambulisha kuwa mchezaji wao wa 28. Leo Agosti 30, Uwanja wa Mkapa ni siku ya kilele cha Wiki ya Mwananchi ambapo wanatambulisha wachezaji wapya na wale waliokuwa na kikosi hicho kwa msimu wa 2019/20 na timu hiyo. Wakati wa utambulisho wa wachezaji hao ambao wametambulishwa na Mtangazaji na Mwadishi wa Wasafi Media ambae pia ni mchambuzi ndani ya Gazeti la Championi, Maulid Kitenge amesema kuwa bado Morrison ni mchezaji wa Yanga. Katika utambulisho huo Kitenge amesema:"Mchezaji wa 28 ndani ya Yanga ni Bernard Morrison ambaye ni mchezaji wetu kwa kuwa kesi ipo CAS hivyo ni mchezaji wa Yanga." Sakata la Morrison lilidumu ndani ya Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) kwa muda wa siku tatu na baadaye maamuzi yalitolewa kuwa Morrison ni mchezaji huru hivyo anaruhusiwa kujiunga na timu yoyote anayohitaji. Agosti 8, alisaini kandarasi ya miaka miwili ndani ya Simb

BREAKING:HASSAN KESSY ASAINI MTIBWA SUGAR

Image
  NYOTA Hassan Khamis Ramadhan Kessy, beki wa kulia amesajiliwa na Mtibwa Sugar akitokea kwa Mabingwa wa  Ligi Kuu ya Zambia msimu 2019/2020 Nkana Red Devils. Kessy alikuwa kwenye rada za Yanga ambao walishindwana naye kwenye masuala ya makubalino jambo lililomfanya aibukie ndani ya Mtibwa Sugar akiwa ni mchezaji huru. Nyota huyo amesaini dili la miaka miwili kutumika ndani ya kikosi cha Mtibwa Sugar wenye maskani yao Morogoro.

LIVE: NGAO YA JAMII, SIMBA 2-0 NAMUNGO

Image
  FT: Simba 2-0 Namungo Zinaongezwa dakika 3 Dakika 90 zimekamilika  Dakika ya 79 Kagere anaingia kuchukua nafasi ya Bocco Dakika ya 77 Dilunga anakosa nafasi nje ya 18 Dakika ya 60 Bernard Morrison anafunga bao la pili kwa pasi Clatous Chama  Kipindi cha pili kimeanza Mapumziko  Dakika 2 zinaongezwa Dakika ya 45 Namungo wanapata faulo baada ya Stephen Sey kuchezewa faulo na Kened Juma  Dakika ya 42 Simba wanapata kona ya Kwanza haizai matunda Dakika ya 38 Namungo inakosa nafasi ya wazi baada ya Simba kujichanganya ndani ya 18 Dakika ya 34 Simba wanapeleka mashambulizi Namungo FC  Dakika ya 20 Morrison anampa pasi Chama ndani ya 18 inaokolewa na Nurdin Barola.  Dakika ya 15 Mzamiru anapewa huduma ya kwanza Dakika ya 9 Namungo wanapiga faulo kuelekea Simba Dakika ya 7 Bocco Goal kwa penalti  Dk 4Bocco anakosa nafasi ndani ya 18 Ngao ya Jamii Uwanja wa Sheikh Amri Abeid  Simba v Namungo FC  Kipindi cha kwanza Simba 0-0

SIMBA V NAMUNGO MOTO KUWAKA NGAO YA JAMII

Image
  JOTO la mtanange wa Ngao ya Jamii kati ya Simba na Namungo, limepanda ambapo leo Jumapili kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, moto utawaka wakati timu hizo zikipambana.   Simba na Namungo zinatarajia kufungua pazia la msimu wa 2020/21 kwa kucheza mechi hiyo ambapo baada ya hapo, Ligi Kuu Bara inatarajiwa kuanza Septemba 6, mwaka huu. Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba, juzi Ijumaa usiku walifika jijini Arusha wakitokea Dar kwa ajili ya mchezo huo, huku Namungo nayo ikifika siku hiyohiyo.   Akizungumzia mchezo huo, Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, alisema: “Tupo tayari na kila mchezaji yupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu wa Ngao ya Jamii. Kocha wa  Namungo, Hitimana Thiery, amesema: “Tumejipanga kwa ajili ya mchezo huo, tumefika huku kwa kuchelewa sana, tuliingia jana (juzi) usiku, sehemu tuliyofikia haikuwa yenye mazingira mazuri, ikabidi tuhame na kutafuta sehemu bora. “Kwa namna ninavyoona, siwezi kusema moja kwa moja kwamba tunaweza kushin

KIKOSI CHA SIMBA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA NAMUNGO FC NGAO YA JAMII

Image
  KIKOSI cha Simba kinachoongozwa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck kitakachoanza leo Agosti 30, dhidi ya Namungo FC mchezo wa Ngao ya Jamii, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha. 

JEMBE LA KAZI YANGA LAANZA SAFARI KUJA BONGO

Image
  MCHEZAJI mpya wa Yanga ambaye ni mshambuliaji kutoka Burkina Faso, anatarajiwa kutua kesho Agosti 31 ameanza leo safari ili kuibuka ndani ya ardhi ya Tanzania. Yacouba Sogne yeye ni mshambuliaji ambaya ilipaswa awasili nchini Agosti 27 ila kutokana na kubadilisha ratiba ya ndege alikwama kusafiri na mashabiki wa Yanga walijitokeza kwa wingi Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere kumpokea na kuambulia patupu. Leo Agosti 30 atakosa tamasha la Mwananchi ndani ya Uwanja wa Mkapa ambalo ni maalumu kwa ajili ya kutambulisha wachezaji wapya pamoja na jezi mpya za Yanga kwa msimu wa 2020/21. 

MANCHESTER CITY KUTOA WACHEZAJI WATATU KUMPATA MESSI

Image
  MAN City imeripotiwa kuwa ipo tayari kuipa Barcelona pauni milioni 89.5 pamoja na wachezaji watatu; Bernardo Silva, Gabriel Jesus na Eric Garcia ili kumpata supastaa Lionel Messi.   City wanamatumaini makubwa ya kufikia makubaliano na Barcelona baada ya Messi kutangaza hivi karibuni juu ya nia yake ya kuondoka Camp Nou katika kipindi hiki cha usajili.   Kama Messi akikubaliana na City, ataungana tena na kocha wake wa zamani Pep Guardiola baada ya miaka yake ya mafanikio Nou Camp akifunga mabao 634 na kutoa asisti 285 kwenye mechi 731 alizoicheza. Sportsmail inaelewa kuwa Messi na Guardiola wamekuwa wakiwasiliana kupitia simu juu ya kutua kwake Etihad, hata kujadili jinsi Messi atakavyozoea England na kujifunza Kiingereza baada ya miaka 20 Hispania.   Wazo la kumsajili Messi kwa muda mrefu lilionekana kama ndoto isiyowezekana lakini dau la pauni milioni 89.5 kujumlisha Silva, Jesus na Garcia linaweza kufanya usajili huo utimie.

SIMBA:TUPO TAYARI KWA AJILI YA NGAO YA JAMII

Image
  SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wachezaji wake wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Namungo FC. Mchezo wa leo, Agosti 30 utakaopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ni maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza Septemba 6. Sven amesema:"Wachezaji 20 wapo tayari kwa mchezo.Maandalizi ya msimu hayajawa marefu lakini tulikuwa na mechi nzuri za kirafiki ambazo zimekuwa na faida kwetu. "Nitakosa huduma ya wachezaji wanne kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Luis (Miqussone), Pascal (Wawa),Chriss (Mugalu) na Gerson (Fraga)," amesema Sven.  Hitimana Thiery,  Kocha Mkuu wa Namungo amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo wana imani watapata matokeo.

COASTAL UNION KUTAMBULISHA MAJEMBE 19

Image
UONGOZI wa Coastal Union umesema kuwa hauna presha na suala la usajili kwa sasa kwa kuwa umejipanga vema kwa kuwasajili wachezaji wapya 19 ikiwa ni idadi ya wachezaji ambao wameondoka. Kwa sasa Coastal Union imeuza  wachezaji saba wa kikosi cha kwanza ambao ni Bakari Mwamnyeto aliyekwenda Simba, Ibrahim Ame yupo Yanga, Ayoub Lyanga,Azam FC,Muhsin Malima, Serbia,Andrew Simba,Azam FC,Makiada Franko, Mbao FC na Sudi Dondola KMC huku ikiwaacha jumla wachezaji 12. Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Mkuu wa Coastal Union, JJuma Mgunda alisema kuwa mashabiki wa timu hiyo wasiwe na mashaka kwa kuwa utaratibu wa usajili wameshamaliza kilichobaki ni kuwatambulisha wachezaji. “Tupo kimya lakini mambo yanakwenda, dirisha la usajili linafungwa tarehe 31, sasa tuhangaike na nini katika kuwatangaza wachezaji wetu? Hatuna presha na mashabiki niwatoe mashaka kwamba tumeshasajili sawa na idadi ya wachezaji ambao wameondoka na tutawatambulisha kabla ya dirisha kufungwa,” alisema Mgunda.  

MASHABIKI WAJISHINDIA TIKETI KUTOKA SPOTI XTRA UWANJA WA MKAPA

Image
  Mapema leo Agosti 30, 2020 Mkuu wa kitengo cha Masoko Global Publishers, Adam Antony ameongoza zoezi la kuwakabihi tiketi za kuingilia uwanjani kushuhudia sherehe za  Kilele cha Wiki ya Mwananchi ambapo mashabiki wamejitokeza kwa wingi.   Walikabidhi mashabiki ambao walikutwa wakilisoma gazeti hilo katika viunga vya Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.