COASTAL UNION KUTAMBULISHA MAJEMBE 19



UONGOZI wa Coastal Union umesema kuwa hauna presha na suala la usajili kwa sasa kwa kuwa umejipanga vema kwa kuwasajili wachezaji wapya 19 ikiwa ni idadi ya wachezaji ambao wameondoka.

Kwa sasa Coastal Union imeuza  wachezaji saba wa kikosi cha kwanza ambao ni Bakari Mwamnyeto aliyekwenda Simba, Ibrahim Ame yupo Yanga, Ayoub Lyanga,Azam FC,Muhsin Malima, Serbia,Andrew Simba,Azam FC,Makiada Franko, Mbao FC na Sudi Dondola KMC huku ikiwaacha jumla wachezaji 12.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Mkuu wa Coastal Union, JJuma Mgunda alisema kuwa mashabiki wa timu hiyo wasiwe na mashaka kwa kuwa utaratibu wa usajili wameshamaliza kilichobaki ni kuwatambulisha wachezaji.

“Tupo kimya lakini mambo yanakwenda, dirisha la usajili linafungwa tarehe 31, sasa tuhangaike na nini katika kuwatangaza wachezaji wetu? Hatuna presha na mashabiki niwatoe mashaka kwamba tumeshasajili sawa na idadi ya wachezaji ambao wameondoka na tutawatambulisha kabla ya dirisha kufungwa,” alisema Mgunda.

 



Comments

Popular posts from this blog

ISHU YA MORRISON KUHUSU MKATABA WAKE IPO MIKONONI MWA KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI

BREAKING: MASHABIKI RUKSA KWENDA UWANJANI, UTARATIBU WATAJWA

AFRICAN LYON WADAI KUWA WAZO LA VISIT TANZANIA NA LOGO MPYA YA SIMBA IMETOKA KWAO