KIKOSI CHA SIMBA KUIFUATA IHEFU LEO MBEYA

 


KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji, leo Septemba Mosi kinatarajiwa kuanza safari kuelekea Mbeya kuifuata Ihefu FC.


Simba iliweka ngome mkoani Arusha tangu Agosti 28 ambapo ilitia timu siku ya Ijumaa kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Ngao ya Jamii uliochezwa Agosti 30,Uwanja wa Sheikh Amri Abeid. 


Kwenye mchezo huo ambao ulikuwa maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara,  Simba ilishinda mabao 2-0 yaliyofungwa na John Bocco dk ya 7 na Bernard Morrison dk ya 60.


Wanaanza safari ya kutetea taji la Ligi Kuu Bara kwa kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya Ihefu Septemba 6 Uwanja wa Sokoine majira ya saa 10:00 jioni.


Huu unakuwa mchezo wa kwanza kwa timu zote ndani ya msimu mpya wa 2020/21 huku Ihefu ikiwa ni msimu wake wa kwanza pia  kushiriki Ligi Kuu Bara baada ya kupanda kutoka Ligi Daraja la Kwanza.



Comments

Popular posts from this blog

ISHU YA MORRISON KUHUSU MKATABA WAKE IPO MIKONONI MWA KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI

BREAKING: MASHABIKI RUKSA KWENDA UWANJANI, UTARATIBU WATAJWA

AFRICAN LYON WADAI KUWA WAZO LA VISIT TANZANIA NA LOGO MPYA YA SIMBA IMETOKA KWAO