AGOSTI 15, 2021 kikosi cha Yanga kiliondoka hapa nchini kuelekea Afrika Kaskazini, kwenye nchi ya Morocco kwa ajili ya kuweka kambi iliyotarajiwa kutumia siku kumi kwa ajili ya maandalizi ya kabla ya msimu ‘Pre season’, ambapo baada ya safari ya siku mbili walitua Jijini Marrakech Agosti 17, ambapo walianza rasmi mazoezi. Kambi hiyo ilihusisha wachezaji wote wa Yanga ambao watatumika msimu ujao wakiwemo nyota wapya kumi ambao wamesajiliwa kwenye dirisha kubwa la usajili ambalo litafungwa rasmi Agosti 31, mwaka huu. Leo ifikapo saa sita usiku, dirisha la usajili litafungwa kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF). Baada ya siku sita za programu ya mazoezi hayo ambayo yalikuwa yakiwasilishwa kwa wapenzi na wadau wa Yanga kupitia mitandao ya kijamii ya klabu hiyo, ghafla kambi hiyo ilivunjwa. Taarifa rasmi kutoka kwenye Uongozi wa Yanga zilieleza kuwa kutokana na sababu mbalimbali na kwa maslahi mapana ya klabu hiyo uongozi uliamua kusitisha kambi hiyo na...