PETER BANDA AITWA TIMU YA TAIFA YA MALAWI


 BAADA ya kumaliza maandalizi ya kwanza kuelekea msimu mpya wa 2021/22 na kurejea Tanzania, kiungo  wa Simba Peter Banda ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Malawi.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes iliweka kambi kwa muda nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Banda ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Malawi kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka 2022. 

Pia wapo nyota wengine wa Simba ambao wapo kwenye kambi ya timu ya taifa ya Tanzania ambao ni pamoja na Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein pamoja na John Bocco.




Comments

Popular posts from this blog

SIMBA KUBADILI KIKOSI MBELE YA TP MAZEMBE AMBAO WATABADILI MFUMO KESHO

SIMBA YAJIFUA LEO SUMBAWANGA KUELEKEA MCHEZO WA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO

MCHEZO MZIMA WA YANGA KUINYOOSHA AIGLE NOIR KWA MKAPA ULICHEZWA HIVI