SENZO AWA C.E.O YANGA

 


MAKAMU Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela leo Agosti 31, 2021 amemtangaza, Senzo Mbatha kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu (C.E.O) wa Klabu hiyo.

Kwa majukumu hayo ana jukumu la kusimamia mchakato wa mabadiliko kufikia mwisho na aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, Hajji Mfikirwa atakuwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala.
Fredrick Mwakalebela ametangaza hayo baada ya Katiba ya Yanga kubadilishwa baada ya wanachama wa Klabu hiyo kupitisha mchakato wa mabadiliko kwa asimia mia.


Mbata awali alikuwa mshauri mkuu wa Yanga kuelekea kwenye mabadiliko baada ya kubwaga manyanga ndani ya Simba ambapo alikuwa kwenye nafasi hiyo.

Ndani ya Yanga anakuwa ni Mtendaji Mkuu wa mpito, (Interm CEO) wa Klabu ya Yanga kufuatia utekelezwaji wa mfumo wa uendeshaji wa klabu.


Comments

Popular posts from this blog

SIMBA KUBADILI KIKOSI MBELE YA TP MAZEMBE AMBAO WATABADILI MFUMO KESHO

SIMBA YAJIFUA LEO SUMBAWANGA KUELEKEA MCHEZO WA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO

MCHEZO MZIMA WA YANGA KUINYOOSHA AIGLE NOIR KWA MKAPA ULICHEZWA HIVI