KIUNGO WA AZAM KUIBUKIA KENYA

 


KIUNGO wa kimataifa wa Kenya na Klabu ya Azam, Kenneth Muguna leo ameondoka kwenye kambi ya Azam FC iliyopo Zambia kwa ajili ya kujiunga na timu ya taifa ya Kenya.

 

Azam ipo Ndola, Zambia kwa ajili ya maandalizi ya kabla ya msimu ya takribani wiki moja na nusu, ambapo wakiwa huko wamepanga kucheza michezo minne ya kirafiki kabla ya kurejea Tanzania Septemba 5, mwaka huu.

 

Watakaporejea Azam watakuwa kwenye maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Horseed ya Somalia, unaotarajiwa kuchezwa kati ya Septemba 10 hadi 12, mwaka huu.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ alisema: “Kikosi chetu kinaendelea vizuri na maandalizi ya kabla ya msimu ‘Preseason’ hapa Ndola Zambia.

 

“Tunatarajia kuwa kiungo wetu wa kimataifa wa Kenya Kenneth Muguna ataondoka kambini kwa ajili ya kujiunga na timu ya taifa ya nchi yao.”


Mchezo wa pili Azam FC ilicheza na Kabwe Warriors ambapo ilishinda kwa bao 1-0 lilifungwa na Prince Dube hivyo kiungo.



Comments

Popular posts from this blog

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA