Posts

Showing posts from April, 2021

WATANO WA SIMBA KUIKOSA KAGERA SUGAR KWA MKAPA

Image
  WAKATI leo kikosi cha Simba kikiwa na kazi ya kusaka mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Kagera Sugar, kikosi hicho kinatarajiwa kuwakosa nyota watano ambao ni Francis Kahata pamoja na Ibrahim Ame. Kahata yeye amesajiliwa na Simba kwa ajili ya mechi za kimataifa ambapo Simba imetinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa imepangiwa na Kaizer Chiefs. Ame atakosekana leo kwa kuwa amefungiwa na Kamati ya Masaa 72 kwa kosa la kumzuia mwamuzi wa pembeni katika mchezo wa ligi dhidi ya Gwambina. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Gwambina Complex na ubao ulisoma Gwambina 0-1 Simba. Wengine ni pamoja na Gadiel Michael, Ally Salim na David Kameta, 'Duchu' hawa hawajawa fiti kwa kuwa wamekosa mechi kwa muda mrefu. Kuhusu maandalizi ya timu hiyo, Meneja Patrick Rweyemamu amesema kuwa hakuna majeruhi ndani ya kikosi hicho na maandalizi yapo sawa.    

TANZANIA PRISONS WALIA NA MWAMUZI WA MCHEZO WAO DHIDI YA YANGA

Image
 BAADA ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho, wachezaji wa Prisons wameonekana kumshushia lawama mwamuzi wa kati wakidai kwamba hakuwasikiliza malalamiko yao. Mwamuzi wa kati wa mchezo huo alikuwa ni Athuman Lazi ambaye alionekana akilalamikiwa na wachezaji wa Prisons wakiongozwa na nahodha Benjamin Asukile. Ni bao pekee la Yacouba Sogne dakika ya 53 lilitosha kuwapaleka Yanga hatua ya robo fainali huku wakisubiri droo ipangwe ndio wajue timu ambayo watacheza nayo hatua ya robo fainali. Asukile amesema kuwa hawakutendewa haki na mwamuzi kwa kuwa walikuwa na uwezo sawa na wapinzani wao ndani ya Uwanja wa Nelson Mandela ila refa hakuwa upande wao. "Kwa upande wa mpira uwezo tulikuwa sawa ila kwa upande wa refa hakuwa upande wetu, wao walituzidi hapo kwa kuwa kila ambapo tulikuwa tukimfuata mwamuzi alikuwa akituambia hajaona, kuna penalti ambayo hatukupewa, bado mwamuzi alisema hajaona. "Ikiwa mwamuzi hajaona basi inamaana ye

VIDEO: SIMBA YAWAITA MASHABIKI KESHO, IKIWA WATAJITOKEZA MEI 8 WAAHIDI MABAO ZAIDI YA MATATU

Image
KUELEKEA kwenye mchezo wa kesho Mei Mosi, ambao ni wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora, Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku dhidi ya Kagera Sugar, uongozi wa Simba umewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi.  Haji Manara, Ofisa Habari wa Simba amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi huku akionesha masikitiko yake kwa mashabiki wa Dar kutojitokeza kwa wingi. Pia ameahidi kuwa ikiwa watajitokeza kwa wingi mchezo wao wa Mei 8( Simba v Yanga) watashinda zaidi ya mabao matatu.   

YANGA YAPENYA 16 BORA MBELE YA TANZANIA PRISONS

Image
 UWANJA wa Nelson Mandela umeshuhudia kikosi cha Yanga kikisepa na ushindi kwa mara ya kwanza mbele ya Tanzania Prisons. Mchezo wa leo ulikuwa ni wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora ambapo baada ya dakika 90, ubao ulisoma Prisons 0-1 Yanga. Ni Yacouba Songne alipachika bao hilo la ushindi kipindi cha pili dakika ya 53 na kuipa kuwanyanyua mashambiki wa timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi. Mchezo wa kwanza ambao ulikuwa wa ligi walipokutana Uwanja wa Nelson Mandela timu zote ziligawana pointi mojamoja kwa kufunngana bao 1-1 zama za Cedric Kaze. Baada ya mchezo huo, kiungo mshambuliaji wa Yanga, Saido Ntibanzokiza amesema kuwa kwao ni furaha kusonga mbele na ni ushindi wa timu nzima kiujumla. "Tumepata ushindi ninafurahi naamini hii ni furaha ya wachezaji kiujumla pamoja na benchi la ufundi," amesema.

FT: KOMBE LA SHIRIKISHO: TANZANIA PRISONS 0-1 YANGA

Image
FT: Tanzania Prisons 0-1 Yanga Kikosi cha Yanga kinatinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Prisons  Zimeongezwa dakika 2 Dakika 90 zimekamilika Dakika ya 88 Deus Kaseke anaingia anatoka Nchimbi Dakika 84 nyota wa Yanga Ninja anapewa huduma ya kwanza Dakika ya 79 Wazir Junior anaingia anatoka Fiston  Dakika ya 78 Lamine anapewa huduma ya kwanza  Dakika ya 72, Lamine anacheza faulo ndani ya 18 kwa Jeremia, mwamuzi anapeta Dakika ya 70 Yanga wanapeleka mashambulizi Prisons  Dakika ya 66, Asukile anafaya jaribio linaokolewa na Metacha  Dakika ya 64, Makapu anaingia anatoka Carinhos  Dakika ya 64, Kimenya na Mohamed Mkopi wanaonyeshwa kadi ya njano Dakika ya 61 Carinhos anapewa huduma ya kwanza Dakika ya 60 Prisons wanapata kona, Lambart Sabiyankana anatoka anaingia Seleman  Dakika ya 53 Goooooal Yacouba Songne  Dakika ya 49, Fiston anachezewa faulo  Dakika ya 48 Ntibanzokiza anapiga faulo inaokolewa Dakika ya 46 Yacouba anajaz

JESSE LINGARD AIGOMEA MAN UNITED

Image
  N YOTA wa West Ham  United, Jesse Lingard  imeelezwa kuwa hana  mpango wa kurejea kwenye  timu yake ya Manchester  United.   Lingard kwa sasa  anakipiga West Ham kwa  mkopo tangu Januari mwaka  huu, akitokea Man United na  akiwa kwenye kiwango kizuri.   Ripoti zinaeleza kuwa  Lingard anampango wa  kuomba kuondoka moja  kwa moja ifikapo mwishoni  mwa msimu huu.   Tangu amejiunga na West  Ham amefanikiwa kufunga  mabao tisa katika mechi 11  na amesaliwa na mkataba  wa mwaka mmoja ndani ya  United.   West Ham wanataka  kumsajili nyota huyo moja  kwa moja huku ada ya  kumng’oa nyota huyo ni kiasi  cha pauni 15m.  Kocha Ole Gunnar  Solskjaer yupo tayari  kumpokea nyota huyo kikosi  kwake ilikuja kupambania  nafasi yake.   Inaelezwa kuwa  Lingard sasa ameamua  kuachana na klabu  yake hiyo ya utotoni,  kutokana na Solskjaer  kutokuwa na imani  naye.   Mbali na West  Ham, klabu kama  Arsenal, Inter Milan  na Paris Saint Germain  zimekuwa zikimtolea  macho Lingard  kuelekea ms

BREAKING: WAPINZANI WA SIMBA ROBO FAINALI NI KAIZER CHIEFS

Image
 DROO ya hatua ya robo fainali imepangwa leo Aprili 30 nchini Misri ambapo tayari wawakilishi wa Tanzania, Simba wametambua watakutana na timu ipi. Ni Kazier Chiefs FC ya Afrika Kusini ambayo itamenyana na Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes, raia wa Ufaransa. Mchezo wa kwanza utachezwa nchini Afrika Kusini kati ya Mei 14 na 15. Mchezo wa pili unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa kati ya Mei 21 ama 22, Uwanja wa Mkapa.

HAWA HAPA SITA WA YANGA KUIKOSA TANZANIA PRISONS LEO

Image
 IKIWA leo Yanga inamenyana na Tanzania Prisons kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora Kombe la Shirikisho ni rasmi itawakosa nyota wake sita kutokana na sababu mbalimbali. Mchezo wa leo unakuwa ni wa pili kwa Kocha Mkuu, Nassredine Nabi kukaa kwenye benchi baada ya ule wa kwanza kuwa dhidi ya Azam FC na ubao ulisoma Yanga 0-1 Azam FC. Hawa hapa nyota sita ambao wataukosa mchezo wa leo:- Dickson Job yeye ni beki wa kati anasumbuliwa na nyama za paja. Tuisila Kisinda yeye anasumbuliwa na bega. Yassin Mustapha Majeruhi Tonombe Mukoko anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano. Michael Sarpong  anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano. Feisal Salum anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

KMC TAYARI KWA MCHEZO WA KESHO, KOMBE LA SHIRIKISHO

Image
KIKOSI cha KMC FC kesho Mei Mosi kitashuka katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kwa ajili ya mchezo wa michuano ya Kombe la Shirikisho ( ASFC) dhidi ya Dodoma Jiji FC mchezo ambao utapigwa saa 10:00 jioni. Kocha msaidizi wa KMC, Habibu Kondo amesema kuwa tayari walishafanya maandalizi ya kutosha tangu wakiwa jijini Dar es Salaam na kwamba hana hofu katika mchezo huo licha ya kwamba michuano hiyo ni migumu lakini anakiamini kikosi chake kitakwenda kufanya vizuri na hivyo kuendelea katika hatua inayofuata ya michuano hiyo ya ASFC. Ameongeza kuwa timu anayokutana nayo kesho ni nzuri na kwamba imekuwa ikifanya vizuri katika michezo yake ya ligi kuu hivyo pamoja na yote bado kama kocha na benchi la ufundi kwa ujumla watahakikisha kuwa Kino Boys inakwenda kufanya vizuri katika mchezo wa kesho. “Michuano hii inafahamika kabisa kwamba ukifungwa unatoka, kwahiyo pamoja na kwamba tunakutana na timu yenye ushindani mkubwa, lakini KMC FC imejiandaa vizuri kwa sababu tunahitaji kuchukua ko

NYOTA WENGINE SIMBA AMBAO MIKATABA YAO INAKARABIA KUMEGUKA ORODHA HII HAPA

Image
IKIWA tayari imeshamalizana na nyota wake watatu ambao ni nahodha John Bocco, nahodha msaidizi Mohamed Hussein,'Tshabalala' na beki wa pembeni Shomari Kapombe bado nyota wengine mikataba yao inakaribia kufika ukingoni. Simba chini ya Didier Gomes ambaye ni Kocha Mkuu, inakazi ya kusaka ushindi kesho dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Mkapa ambao ni wa Kombe la Shirkisho. Hawa hapa nyota hao ambao mikataba yao inaweza kumeguka msimu ukikamilika ndani ya ligi 2020/21:-   Kiungo mkabaji  Jonas Mkude.  Kipa namba mbili, Beno Kakolanya kiungo mshambuliaji  Ibrahim Ajibu beki wa kushoto  Gadiel Michael. Pia kiungo Francis Kahata wengi wanapenda kumuita kijiko na kiungo mshambuliaji  Miraji Athumani. Mkongwe Erasto Nyoni ambaye ni kiraka beki wa kati Kenedy Juma na Pascal Wawa. Kuhusu wachezaji kuondoka ndani ya Simba, hivi karibuni Ofisa Habari wa Simba Haji Manara alisema kuwa mpango wa Simba ni kuwa na wachezaji makini na haitaweza kumuachia mchezaji yeyote ambaye anatakiwa

YANGA NA JUMA MWAMBUSI KUHUSU KUREJEA KWAKE WAMEFIKIA HAPA

Image
  K WA  kauli ya kiungwana  aliyoitoa ya Kaimu Katibu  Mkuu wa Yanga, Haji  Mfikirwa sasa ni wazi kuwa  aliyekuwa Kaimu Kocha  Mkuu wa Yanga, Juma Mwambusi  atakuwa rasmi ameachana na klabu hiyo  tangu zilipoibuka taarifa zake za kwenda  kwao Mbeya kwa ajili ya kuhani msiba  wa nduguye.   Tangu Mwambusi akabidhiwe mikoba  ya aliyekuwa kocha wao, Cedrick Kaze  amedumu na kikosi hicho kwa takribani  miezi miwili, ambapo ameisaidia timu  kuvuna pointi 7, kwenye michezo mitatu  aliyohudumu kama mkuu wa benchi la  ufundi.   Kwani kabla Yanga haijaruhusu kichapo  cha pili kwenye Ligi Kuu Bara dhidi ya  Azam FC, Jumapili iliyopita timu ikiwa  chini ya Mtunisia Nasreddine Al Nabi,  kwenye mchezo  uliyochezwa Jumapili  iliyopita, Mwambusi  aliiongoza kupata  sare dhidi ya KMC na  baadaye akavuna pointi  tatu dhidi ya Mtibwa  Sugar kisha dhidi ya  Gwambina FC.   Championi Ijumaa  limezungumza na  Kaimu Mwenyekiti wa  Yanga, Haji Mfikirwa  ambaye ameweka wazi  kuwa, wao kama klabu  tayar

SIMBA YAPANIA KUFANYA MAAJABU KIMATAIFA, KUWAJUA WAPINZANI WAO LEO

Image
  K IUNGO  mshambuliaji wa  Simba, Larry Bwalya  amesema kuwa timu  hiyo ina nafasi kubwa ya  kufanya maajabu katika  Hatua ya Robo Fainali ya  Ligi ya Mabingwa Afrika  ambayo inatarajiwa  kupangwa leo Ijumaa.   Bwalya alijiunga na Simba  mwanzoni mwa msimu huu amekuwa ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Didier Gomes, raia wa Ufaransa .   Akizungumza na  Championi Ijumaa  kuelekea kwa droo  hiyo ambapo Simba  ndiyo itajua mpinzani  wake, Bwalya alisema:  “Imekuwa heshima  kwangu na timu pia  kuona tunafanikiwa  kutinga hatua ya robo  fainali katika michuano  ya kimataifa. “Kwa sasa tunasubiri  ratiba na timu ambayo  tutacheza nayo katika  hatua ya robo fainali ya  michuano ya Ligi ya  Mabingwa Afrika.   “Bado tunayo nafasi  ya kutwaa ubingwa  wa michuano hiyo  kutokana na maandalizi  mbalimbali ambayo  tunaendelea kufanya, “  alisema Bwalya.   Katika droo ya leo  Simba inatarajiwa  kupangwa na  wapinzani kati ya  hawa, CR Belouizdad  au MC Alger zote za  Algeria au Kaizer  C

NYOTA HAWA WATATU WA YANGA KUIKOSA TANZANIA PRISONS LEO

Image
  W ACHEZAJI  watatu  tegemeo  hivi sasa wa Yanga  viungo Mukoko  Tonombe, Feisal  Salum ‘Fei Toto’ na  mshambuliaji Michael  Sarpong wanatarajiwa  kuukosa mchezo wa  leo Ijumaa dhidi ya  Tanzania Prisons.   Timu hizo  zinatarajiwa kujitupa  kwenye Uwanja wa  Nelson Mandela,  mkoani  Rukwa katika mchezo  wa Hatua ya 16 Bora  ya Kombe la FA. Kwa mujibu wa  taarifa ambazo  imezipata Championi  Ijumaa, wachezaji hao  wataukosa mchezo huo  kutokana na kutumikia  adhabu ya kadi za njano.   Mtoa taarifa huyo  kutoka ndani ya benchi  hilo la ufundi ameeleza  kuwa nyota hao  wanatumikia adhabu  ya kadi tatu za njano  walizozipata katika  michezo iliyopita. Alisema kuwa Kocha  Mkuu wa Yanga,  Nasreddine Nabi  anawaandaa wachezaji  wengine watakaocheza  nafasi zao katika  kuelekea mchezo huo. “Katika kuelekea  mchezo wetu wa  kesho (leo) tunatarajia  kuwakosa wachezaji  wetu watatu muhimu  ambao ni Tonombe, Fei  Toto na Sarpong. “Wata kosekana  kutokana na  kutumikia ad habu ya ka

MESSI KUSEPA BARCELONA, PSG WAWEKA OFA

Image
  K LABU ya  Paris Saint  Germain  imeelezwa  kwa sasa ipo  kumshawishi  staa wa Barcelona, Lionel  Messi kujiunga na klabu  hiyo, kumpa ofa ya miaka  miwili.   Messi kwa sasa  anaweza kuongea na  timu yoyote kwani  mkataba wake  umesalia wa mwezi mmoja  ndani ya Barcelona.  Ripoti zinaeleza mpaka  sasa haijafahamika kama  Messi atasalia kikosini hapo  au ataondoka.   Taarifa zainaeleza kuwa  PSG imetoa ofa ya miaka  miwili mezani kwa ajili ya  staa huyo kutua kikosini  hapo. Ripoti zinaeleza kuwa  sababu ya PSG kutaka  kumchukua Messi ni kuona  staa huyo anafanikiwa kwa  mara nyingine kutwaa taji  la Ligi ya Mabingwa Ulaya  akiwa na uzi wao.   Imeelezwa kuwa sasa  hakuna kipya ndani  ya Barcelona kwani  kinachosubiriwa ni jibu la  Messi kama anabaki au  anaondoka.   PSG wao wapo tayari  kumsajili staa huyo na  kuongeza nguvu ndani  ya kikosi chao ambacho  kina vijana kibao wenye  ubora.   Kwa upande mwingine,  taarifa zinaeleza kuwa  Rais wa Barcelona Joan  Laporta bado ana

SAUTI: GSM WABAINISHA KWAMBA WANAIPA THAMANI YANGA

Image
SAUTI ya Injinia Hersi Said kutoka Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Klabu ya Yanga akibainisha eneo ambalo wao ni bora kuliko timu nyingine na ameweka wazi kwamba wanaipa thamani Yanga.  

MANCHESTER UNITED YAISHUSHIA KICHAPO ROMA EUROPA LEAGUE

Image
  USHINDI wa mabao 6-2 ambao wameupata Manchester United mbele ya Roma kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza mbele ya Roma unawapa nafasi ya kuweza kutinga fainali. United inayonolewa na Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solksajer iliweza kufanya vizuri usiku wa kuamkia leo kwenye mchezo wa Europa League uliochezwa Uwanja wa Old Trafford. Ni Bruno Fernandes dk 9 na dk 71 alitupia kwa penalti,  Edinson Cavani dakika ya 48 na 64 Paul Pogba dakika ya 75, Mason Greenwood dakika ya 86 hawa walifunga mabao ya United kwa Roma ni Lorenzo Pellegrini dakika ya 15 kwa penalti na Edin Dzeko dakika ya 33. Ole amesema kuwa amefurahishwa na uwezo wa wachezaji wake kwa kuwa walitumia uzoefu wao kusaka ushindi kwenye timu kubwa na mchezo ambao ulikuwa na ushindani muda wote.

MORRISON AWAFANYIA MAZOEZI MAALUMU MABOSI WAKE WA ZAMANI

Image
  Z IKIWA  zimebaki  takribani siku nane  kabla ya Dabi  ya Kariakoo kati ya  Simba na Yanga, Kiungo  Mshambuliaji wa Simba,  Bernard Morrison,  amesema atakuwa  akifanya mazoezi maalum  kwa ajili ya mchezo huo.   Morrison ambaye  amejiunga na Simba msimu  huu akitokea Yanga, kama  akicheza mechi hii, itakuwa  ni mara ya kwanza kucheza  dhidi ya Yanga baada ya  ile ya kwanza iliyochezwa  Novemba 7, 2020,  kukosekana.   Tayari Morrison  amecheza Kariakoo Dabi  mbili akiwa Yanga ambapo  ya kwanza alifunga bao  pekee lililoipa  Yanga  ushindi wa  1-0 kwenye  Ligi Kuu Bara,  kabla ya ile  ya pili Simba  kushinda  4-1 ndani ya  Kombe la FA.   Mei 8,  mwaka huu,  Simba itakuwa  mwenyeji wa  Yanga katika  mchezo wa  Ligi Kuu Bara unaotarajiwa  kuchezwa Uwanja wa  Mkapa, Dar.   Akizungumza na  Spoti  Xtra,  Morrison amesema  kuwa: “Haina  haja ya mimi  kuwazungumzia  Yanga kwani  sioni maana ya  kuizungumzia  maana mimi  mwenyewe  naonekana kama  Simba, kwa hiyo  tusubirie siku 

OGOPA MATAPELI DUBE HAUZWI KABISA

Image
  U ONGOZI  wa Azam  FC, umesema kuwa  hawapo tayari kumuuza  staa wao, Mzimbabwe, Prince  Dube, kwenda Simba na  badala yake ataendelea kubaki  kikosini kwao.   Hiyo ikiwa ni siku chache  tangu ziwepo tetesi za Simba  kuwa kwenye mipango ya  kumnasa mshambuliaji huyo  anayeongoza kwa mabao Ligi  Kuu Bara akiwa amepachika 12.   Taarifa zilizopo kwa sasa  ni kwamba, hivi karibuni  mshambuliaji huyo ameongeza  mkataba wa miaka miwili  kuendelea kuitumikia Azam,  hivyo atakuwa hapo hadi 2024. Akizungumza na  Spoti Xtra,  Mtendaji Mkuu wa Azam,  Abdulkarim Amin ‘Popat’ alisema  Dube hataenda timu yoyote hapa  nchini, bali atabaki Azam. Popat aliongeza kuwa,  mshambuliaji huyo kama  akiondoka Azam, basi atakwenda  kucheza soka nje ya Tanzania. “Kwa kifupi Dube hatakwenda  popote ndani ya nchi hii,  ataendelea kubaki Azam.   “Dube kama akiondoka hapa  Azam, basi atakwenda kucheza  soka nje ya Tanzania na siyo  kwenye klabu za hapa.   “Hizo timu zinazomtaka hata  watoe dau kub

BREAKING: SHOMARI KAPOMBE ASAINI MKATABA MPYA SIMBA

Image
  BREAKING: Beki wa pembeni wa Simba, Shomari Kapombe amesaini dili jipya baada ya kukubaliana na uongozi kuongeza mkataba. Beki huyo mzawa chaguo namba moja la Kocha Mkuu, Didier Gomes mkataba wake ulikuwa unafika ukingoni mwishoni mwa msimu wa 2020/21. Alikuwa anatajwa kuingia rada za FAR Rabat ya Morocco pamoja na timu nyingine nchini Afrika Kusini ambazo zilikuwa zinahitaji saini yake. Baada ya makubaliano mazuri na mabosi wake wa sasa nyota huyo amesaini dili jipya na inaelezwa ni kandarasi ya miaka miwili.

NAMUNGO FC WATOLEWA HATUA YA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO

Image
  WAWAKILISHI wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika. Namungo FC wameyaaga mashindano hayo bila kukusanya pointi katika hatua ya makundi ambapo ilikuwa ipo kundi D. Ikiwa imecheza jumla ya mechi sita, imepoteza zote sita kwa kufungwa jumla ya mabao 9 na safu yao ya ushambuliaji haijapachika bao. Mchezo wa mwisho  ulikuwa ni dhidi ya Pyramids uliochezwa Uwanja wa 30 June ambao ulisoma Pyramids 1-0 Namungo FC.  Bao pekee la ushindi kwa Pyramids lilipachikwa na Ibrahim Adel dakika ya 65 na kuwapoteza jumlajumla wawakilishi wa Tanzania wanaonolewa na Hemed Morroco.  Ni Raja Casablanca yenye pointi 18 na Pyramids yenye pointi 12 zimetinga hatua inayofuata kutoka Kundi D, huku Nkana FC yenye pointi 6 na Namungo FC zikiishia katika hatua ya makundi

SIMBA YAVUJISHA SIRI ZA MFARANSA GOMES

AZAM FC KAZINI LEO HATUA YA 16 BORA MBELE YA POLISI TANZANIA

Image
 KIKOSI cha Azam FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina leo Aprili 28 kina kazi ya kusaka ushindi mbele ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Kombe la Shirikisho utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex. Mchezo huo ni wa hatua ya 16 bora na yule atakayepoteza safari yake ya kulisaka taji hilo itakuwa imefika kikomo. Kwa sasa mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho ni Simba ambao walitwaa taji hilo zama za Sven Vandenbreocek kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC mchezo uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela, Songea na safari hii fainali itapigwa Kigoma. Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa malengo yao ni kuona kwamba wanapata ushindi kwenye mchezo huo ili kuweza kutimiza jambo lao la kutwaa ubingwa. "Tupo imara na tunahitaji kurejea katika mashindano ya kimataifa, ili uweze kurudi huko ni lazima upate ushindi na kutwaa taji tunaamini tutafanya vizuri, mashabiki watupe sapoti," amesema.

MSHAMBULIAJI YACOUBA APITISHWA NA MAKOCHA WA MATAIFA MANNE

WAWILI WA SIMBA KUIKOSA KARIAKOO DABI MAZIMA KWA MKAPA

Image
 BEKI wa kati wa Simba Ibrahim Ame anatarajiwa kuukosa mchezo wa Kariakoo Dabi, kati ya Simba na Yanga unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Mei 8, Uwanja wa Mkapa. Beki huyo ambaye ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Simba akitokea Klabu ya Coastal Union ya Tanga amefungiwa na Kamati ya Masaa 72. Hali hiyo inatokana na kufungiwa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara katika kikao cha Aprili 27,2021 baada ya kupitia matukio na mwendo wa Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili. Ame amefungiwa mechi tatu na faini ya laki tano kwa kosa la kumzuia mwamuzi msaidizi kufanya maamuzi yake ilikuwa ni kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Gwambina FC. Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Gwambina Complex, Aprili 24, ubao ulisoma Gwambina 0-1 Simba na bao la ushindi lilifungwa na Mohamed Hussein kwa shuti kali la guu la kushoto akiwa nje ya 18. Mbali na Ame pia nyota Francis Kahata naye ataukosa mchezo huo kwa sababu yeye jin

NABI AKABIDHIWA DAKIKA 630 ZA MOTO YANGA, CHEKI ILIVYO

GWAMBINA FC YAWEKA WAZI MALENGO YAO MSIMU HUU

Image
  BADRU Mohammed, Kocha Mkuu wa Gwambina FC amesema kuwa hesabu kubwa za timu hiyo kwa sasa ni kuweza kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/21. Kwenye msimamo ipo nafasi ya 12 ikiwa imekusanya jumla ya pointi 30 baada ya kucheza jumla ya mechi 27. Haijawa kwenye mwendo mzuri licha ya kwamba ana tuzo ya kocha bora wa mwezi Machi kwani katika mechi zake nne za hivi karibuni ameambulia kichapo mfululizo. Waliacha pointi tatu mbele ya KMC, Yanga, Simba na ilipoteza pia kwa kufungwa na Mwadui ambayo inapambana kusaka nafasi ya kujinasua kutoka nafasi ya 18 ambayo imedumu nayo kwa muda mrefu. Badru amesema:"Malengo yetu makubwa kwa sasa ni kuona kwamba timu inabaki kwenye ligi msimu ujao, matokeo ambayo tunayapata ni mabaya ila kuna kitu ambacho tunakionyesha. "Wachezaji wamekuwa wakifanya makosa ambayo tunayafanyia kazi hivyo nina amini kwamba wale ambao wanaona wanajua kwamba Gwambina ni hodari," amesema.

HAPA NDIPO WANAPOPATAKA AZAM FC NDANI YA LIGI KUU BARA

YANGA YAWAPIGA MKWARA WAZEE WA PIRA GWARIDE, MASHINE ZAO ZA KAZI HIZI HAPA

Image
 UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa una imani ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa kesho Aprili 30, mbele ya Tanzania Prisons wenye sera ya pira gwaride ambao ni wa Kombe la Shirikisho. Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi umeweka kambi kwa muda Mbeya kabla ya kuibukia Songea kwa ajili ya mchezo huo wa hatua ya 16 bora. Kikosi hicho kilitinga hatua hiyo kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ken Gold katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru na bao pekee la ushindi lilifungwa kwa mkwaju wa penalti na Fiston Abdulazack ambaye kwa sasa yupo na kikosi pia. Nyota wengine ambao wapo kwenye msafara huo ni pamoja na Ramadhan Kabwili, Farouk Shikahlo na Metacha Mnata kwa upande wa makipa. Dickson Job na Abdala Shaibu, 'Ninja' kwa upande wa mabeki pamoja na Paul Godfrey, 'Boxer'. Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wanatambua Tanzania Prisons ni timu ngumu na imara ila watapambana kupata matokeo. "Katika hali ya kawaida, Tanzania Prisons ni timu ima