NAMUNGO FC WATOLEWA HATUA YA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO

 


WAWAKILISHI wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Namungo FC wameyaaga mashindano hayo bila kukusanya pointi katika hatua ya makundi ambapo ilikuwa ipo kundi D.


Ikiwa imecheza jumla ya mechi sita, imepoteza zote sita kwa kufungwa jumla ya mabao 9 na safu yao ya ushambuliaji haijapachika bao.


Mchezo wa mwisho  ulikuwa ni dhidi ya Pyramids uliochezwa Uwanja wa 30 June ambao ulisoma Pyramids 1-0 Namungo FC. 


Bao pekee la ushindi kwa Pyramids lilipachikwa na Ibrahim Adel dakika ya 65 na kuwapoteza jumlajumla wawakilishi wa Tanzania wanaonolewa na Hemed Morroco. 


Ni Raja Casablanca yenye pointi 18 na Pyramids yenye pointi 12 zimetinga hatua inayofuata kutoka Kundi D, huku Nkana FC yenye pointi 6 na Namungo FC zikiishia katika hatua ya makundi



Comments

Popular posts from this blog

ISHU YA MORRISON KUHUSU MKATABA WAKE IPO MIKONONI MWA KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI

BREAKING: MASHABIKI RUKSA KWENDA UWANJANI, UTARATIBU WATAJWA

AFRICAN LYON WADAI KUWA WAZO LA VISIT TANZANIA NA LOGO MPYA YA SIMBA IMETOKA KWAO