SIMBA YAPANIA KUFANYA MAAJABU KIMATAIFA, KUWAJUA WAPINZANI WAO LEO


 KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Larry Bwalya amesema kuwa timu hiyo ina nafasi kubwa ya kufanya maajabu katika Hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo inatarajiwa kupangwa leo Ijumaa.

 

Bwalya alijiunga na Simba mwanzoni mwa msimu huu amekuwa ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Didier Gomes, raia wa Ufaransa.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa kuelekea kwa droo hiyo ambapo Simba ndiyo itajua mpinzani wake, Bwalya alisema: “Imekuwa heshima kwangu na timu pia kuona tunafanikiwa kutinga hatua ya robo fainali katika michuano ya kimataifa.


“Kwa sasa tunasubiri ratiba na timu ambayo tutacheza nayo katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

“Bado tunayo nafasi ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo kutokana na maandalizi mbalimbali ambayo tunaendelea kufanya, “ alisema Bwalya.

 

Katika droo ya leo Simba inatarajiwa kupangwa na wapinzani kati ya hawa, CR Belouizdad au MC Alger zote za Algeria au Kaizer Chiefs ya Afrika ya Afrika Kusini inatarajiwa kupangwa saa 9:00 alasiri.



Comments

Popular posts from this blog

SIMBA KUBADILI KIKOSI MBELE YA TP MAZEMBE AMBAO WATABADILI MFUMO KESHO

SIMBA YAJIFUA LEO SUMBAWANGA KUELEKEA MCHEZO WA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO

MCHEZO MZIMA WA YANGA KUINYOOSHA AIGLE NOIR KWA MKAPA ULICHEZWA HIVI