Posts

Showing posts from September, 2020

YANGA YAJIPIGIA BAO 2-0 KMKM AZAM COMPLEX

Image
 KIKOSI cha Yanga leo Septemba 30 kimeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya KMKM kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex. Mabao ya Yanga yalifungwa na Tonombe Mukoko dakika 10 kwa kona ya Carols Carinhos kiungo ambaye amepewa jukumu la kupiga mipira iliyokufa ndani ya Yanga. Dakika 20 mbele Mukoko tena alipachika bao la pili na la mwisho wa timu yake baada ya mabeki wa KMKM ya Zanzibar kujichanganya katika harakati za kuokoa hatari. Kipindi cha pili mambo yalikuwa magumu kwa KMKM kuweza kuweka mzani sawa huku Yanga nao pia wakikwama kuongeza bao la pili.   Mchezo wa leo ulikuwa ni wa kirafiki ambapo lengo kubwa ni kukiweka kikosi sawa cha Yanga fiti kwa kuwa hakikuwa na mazoezi ya muda mrefu kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2020/21 kutokana na janga la Virusi vya Corona kutibua ratiba nyingi duniani.  Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema kuwa malengo makubwa ni kukiandaa kikosi kwa ajili ya mechi zao zinazof

KUWAONA STARS WAKIMENYANA NA BURUNDI BUKU TATU TU

Image
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania,(TFF) limeweka wazi viingilio vya mchezo wa kirafiki uliopo kwenye  ya kalenda ya FIFA utakaoikutanisha timu ya Taifa ya Tanzania dhidi ya Burundi. Mchezo huo utakaochezwa Oktoba 11,2020 , Uwanja wa Mkapa unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kasi ya ligi ya Bongo pamoja na ujirani wa nchi hizi za ukanda wa Afrika Mashariki. Bei elekezi kwa mzunguko ambayo itampa ruhusa shabiki wa Taifa Stars kupata uhondo ni shilingi 3,000(buku tatu) huku VIP B ikiwa ni 10,000 na ile ya VIP A ikiwa ni 20,000. Pia ushindani unatarajiwa kuwa mkubwa kwa kuwa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Ettiene Ndayiragije ni raia wa Burundi hivyo atakuwa anacheza na timu ambayo anaijua na wao wanaitambua vema mbinu ya mzawa wao.  Uwepo wa nyota wa Burundi ndani ya ligi ya Bongo ikiwa ni pamoja na Bigirimana Blaise anayekipiga Namungo mwenye mabao mawili msimu huu kwenye ligi Jonathan Nahimana kipa wa Namungo ambaye naye ni imara ndani ya lango vitaongeza

MUANGOLA WA YANGA BALAA LAKE SIO LA MCHEZOMCHEZO

Image
  KIUNGO wa Yanga,  Carlos Carlinhos raia wa Angola amepewa jukumu moja kubwa ndani ya kikosi hicho kwa kupiga mipira iliyokufa ikiwa ni kona pamoja na faulo. Yanga ikiwa imefunga mabao manne ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 amehusika kwenye mabao mawili ambapo alitengeneza pasi za mwisho mbili ambazo zilileta mabao  Mechi yake ya kwanza kuanza kipindi cha kwanza ilikuwa ni dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro wakati Yanga ikishinda bao 1-0. Alitumia dakika 72 uwanjani na dakika ya 61 kwenye mzunguko wa nne alitoa pasi ya bao ya pili kwa Lamine Moro na kumfanya awe kinara wa pasi za mwisho ndani ya Yanga akiwa nazo mbili.   Pasi yake ya kwanza aliitoa Uwanja wa Mkapa wakati Yanga ikishinda bao 1-0 mbele ya Mbeya City ambapo pia alipiga kona iliyokutana na Lamine aliyepachika bao lake la kwanza kwa kichwa. Yanga kwa sasa inajiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 3, Uwanja wa Mkapa. Leo itakuwa na kibarua cha kumenyan

BWALYA APEWA MAJUKUMU MENGINE NDANI YA SIMBA

Image
  BOSI wa benchi la ufundi la Simba, Mbelgiji Sven Vandenbroeck, amembebesha majukumu mazito kiungo wake Mzambia Rarry Bwalya la kuhakikisha anaonyesha kiwango kwenye mechi zao za ugenini baada ya kung’ara kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.   Kocha huyo amempa majukumu Bwalya na wachezaji wengine wa kikosi hicho kuhakikisha wanaonyesha uwezo mkubwa katika mechi zao za mkoani kwa ajili ya kuipa timu hiyo matokeo. Bwalya amekuwa mmoja wa viungo walioonyesha ufundi katika mechi mbili walizocheza dhidi ya Gwambina ambayo alianza na Biashara United Uwanja wa Mkapa, Dar. Simba watacheza mechi ijayo ya Ligi Kuu Bara Oktoba 4, dhidi ya JKT Tanzania katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Mbelgiji huyo amesema kuwa anataka kuwaona wachezaji wake wote wakicheza kwa kiwango kikubwa kutokana na wengi kuwa na uwezo mkubwa.   “Wiki ijayo tunatoka kwenda ugenini dhidi ya JKT Tanzania, natarajia tutacheza hivihivi kwa kiwango kizuri hata kama kiufundi hatutacheza kama mechi iliyopita dhidi ya Gwambin

MITAMBO HII YA MABAO NDANI YA SIMBA YAMPA JEURI SVEN

Image
  KASI ya ufungaji ya mastraika wawili wa Simba, Chris Mugalu na Meddie Kagere imempa kiburi kocha wa timu hiyo, Sven Vandenbroeck kwa kusema kuwa inampa nafasi kubwa ya kutamba kwenye Ligi Kuu Bara na hata wakianza kucheza mechi za kimataifa. Kocha huyo ameongeza kuwa wachezaji wake hao pamoja na wengine wanaocheza eneo la ushambuliaji akiwemo Bernard Morrison wanampa uhakika wa kushinda kwenye mechi yoyote ile kwani nje ya kufunga wanajua kutengeneza nafasi.   Mugalu na Kagere wote kwa sasa wamefunga mabao mawili kwenye ligi wakiwa sawa na kiungo Mzambia Clatous Chama na Mzamiru Yassin.   Sven amesema kuwa uwezo huo wa juu wa kufunga wa mastraika wake hao unampa mwanga wa kuona ana uwezo wa kushinda mechi yoyote bila ya kujalisha ni ya ligi au ya kimataifa.   “Tuna washambuliaji wengi wazuri ambao wanajua kwa kiasi kikubwa kufunga, kitu ambacho ni kizuri kwangu kwa sababu hatutegemei mtu mmoja kwenye hilo. “Wanacheza kitimu na kupeana nafasi ambazo zinatufanya tuwe na uhak

MARCEL KAHEZA AFICHUA KILICHO NYUMA YA MAFANIKIO

Image
 MARCEL Kaheza mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Polisi Tanzania amesema kuwa kikubwa kinachoipa ushindi timu yake ni ushirikiano ambao wanauonyesha wachezaji wakiwa uwanjani pamoja na mbinu za mwalimu. Polisi Tanzania inafundisha na Malale Hamsini ambaye ni Kocha Mkuu, mchezo wake uliopita wa raundi ya nne ilishinda mabao 3-0 mbele ya Dodoma Jiji mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Kaheza anashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi kwenye raundi ya nne ambapo alifunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 3-0 mbele ya Dodoma Jiji. Nyota huyo amesema:"Mwalimu amekuwa akitupa mbinu nyingi kwa ajili ya kutafuta ushindi nasi pia tumekuwa tukizifuata, sapoti kutoka kwa mashabiki na ushirikiano ambao tunaupata ni jambo ambalo linatupa ushindi." Mchezo wao unaofuata kwa Polisi Tanzania ni Oktoba 5, Uwanja wa Uhuru itakuwa dhidi ya KMC ambayo imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar.

AZAM FC YAANZA KUJIWEKA MGUU SAWA KWA AJILI YA KUMENYANA NA KAGERA SUGAR

Image
  KIKOSI cha Azam FC kimeanza maandalizi ya kujiwinda na mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex. Azam FC jana, Septemba 29 ilianza kupiga matizi hayo ili kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo wao wa raundi ya tano ambao unatarajiwa kuchezwa Oktoba 4 majira ya saa 1:00 usiku.  Timu zote mbili zinaingia ndani ya uwanja zikiwa zimetoka kushinda mechi zao za raundi ya nne ambapo Azam FC ilishinda bao 1-0 mbele ya Tanzania Prisons na Kagera Sugar ilishinda bao 1-0 mbele ya KMC. Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa timu zote zinahitaji kuendeleza rekodi zao ambazo wameziweka ndani ya uwanja. Azam inahitaji kuendelea kulinda rekodi yake ya Septemba kwa kucheza mechi nne ndani ya dakika 360 bila kupoteza huku Kagera Sugar ikiwa na hesabu za kurejesha makali yake baada ya kuanza msimu kwa kusuasua. Ikiwa imecheza mechi nne ilipoteza mechi mbili sare moja na ushindi mmoja jambo ambalo halikuwapa furaha wachezaji pamoja na

MWINYI ZAHERA: SIMBA INA KIKOSI BORA MSIMU WA 2020/21

Image
  KOCHA wa zamani wa Yanga ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Gwambina, Mkongomani Mwinyi Zahera, amefunguka kuwa Simba wana kikosi imara kwa msimu huu wa 2020/21.   Zahera aliwahi kuwa kocha wa Yanga kwa kipindi cha msimu mmoja na nusu, aliyasema hayo baada ya kushuhudia kikosi chake kikipoteza baada ya kucheza na Simba kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara.  Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 26 ulikuwa ni wa mzunguko wa nne. Mabao ya Simba yalifungwa na Meddie Kagere, Pascal Wawa na Chris Mugalu.Zahera amesema Simba ina kikosi cha wachezaji wengi ambao wana vipaji vikubwa jambo ambalo linaweza kumuweka kwenye hatari mpinzani yeyote wanayekutana naye.   “Ni jambo lisilopingika kuwa Simba msimu huu imejipanga kufanya mambo makubwa kutokana na ubora wa kikosi chao ulivyo.   “Kabla ya mchezo dhidi yao tulikaa na wachezaji wetu na kuwaambia kuwa tunakwenda kucheza dhidi ya timu bora zaidi ya zile tulizocheza nazo hapo awali hasa kwa kulinganisha uwezo wa mchezaji

KMKM WATIA TIMU DAR, KIINGILIO BUKU TANO TU

Image
  TIMU ya KMKM SC ya Zanzibar  imewasili leo Septemba 30 Dar tayari kwa mchezo wa kirafiki leo dhidi ya Yanga utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex. Mchezo huo wa kirafiki unatarajiwa kupigwa majira ya saa 1:00 usiku ukiwa na malengo ya kukiweka sawa kikosi cha Yanga kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara. Mechi hiyo  kiingilio cha 5,000 mzunguko na 10,000 VIP.  Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Zlatko Krmpotic ipo kwenye maandalizi ya mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 3, Uwanja wa Mkapa.

PRINCE DUBE WA AZAM FC ALA SAHANI MOJA NA MEDDIE KAGERE WA SIMBA

Image
  BAADA ya Prince Dube kuifungia Azam FC bao la ushindi dhidi ya Tanzania Prisons ni wazi nyota huyo anakula sahani moja na washambuliaji kama Meddie Kagere na Chris Mugalu, ambao wamekuwa na uwiano mzuri wa kufunga.   Dube tangia asajiliwe na Azam amekuwa na kiwango kizuri hususani katika michezo ya ligi kuu mara baada ya kufanikiwa kufunga mabao matatu na kutoa pasi ya bao moja katika michezo minne aliyoichezea timu hiyo. Dube katika michezo hiyo minne aliyoichezea Azam alifanikiwa kufunga katika michezo miwili dhidi ya Coastal Union alipofunga mabao mawili kisha akafunga bao moja katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons.   Michezo mingine ni dhidi ya Polisi Tanzania ambapo alitoa pasi ya bao lililofungwa na Obrey Chirwa huku katika mchezo dhidi Mbeya akishindwa kufunga wala kutoa pasi ya bao.   Baada ya kufunga mabao hayo matatu kwenye ligi, Dube ni wazi anakula sahani moja na washambuliaji wengine kama Meddie Kagere na Chris Mugalu wa Simba ambao wamefunga mabao mawili ki

KUPOTEZA MBELE YA SPURS, LAMPARD HATA HAELEWI

Image
  FRANK Lampard, Kocha Mkuu wa Chelsea amesema kuwa kupoteza kwake mbele ya Tottenham Hotspurs kumemvuruga kwa kuwa walianza kushinda ndani ya dakika 45 za mwanzo. Mchezo huo wa Kombe la Carabao hatua ya 16 bora uliochezwa usiku wa kuamkia leo, Uwanja wa Tottenham Hotspur ulikuwa na ushindani mkubwa na dakika 90 zilikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 jambo lililopelekea mshindi kupatikana kwa penalti. Timo Werner dakika ya 19 alianza kufunga kwa Chelsea na lilisawazishwa dakika ya 83 na Erik Lamela ambapo kwenye penalti, Spurs inayonolewa na Jose Mourinho ilishinda penalti 5-4.Mason Mount alikosa penalti kwa upande wa Chelsea. Lampard amesema kuwa wachezaji wake walionekana wamechoka kwenye mchezo huo jambo lililowafanya washindwe kuibuka na ushindi jumlajumla. "Tulikiwa tunahitaji kubaki kwenye ushindani ila inaonekana wachezaji wangu walikuwa wamechoka,kwa hali ile ilikuwa ngumu kupata matokeo chanya na ilikuwa ni ngumu kwetu kupoteza kwa kuwa tulianza kushinda,&quo

SIMBA YAIPOTEZA JUMLAJUMLA YANGA KWA MKAPA

Image
  ZIKIWA zimebaki siku 17 kwa Yanga na Simba kukutana Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, rekodi zinaonyesha kuwa ndani ya dakika 180, Simba imewapoteza  Yanga kwenye mechi zao ambazo wamecheza Uwanja wa Mkapa kwa kufunga mabao mengi. Yanga ambao ni wenyeji wa mchezo huo wameutumia Uwanja wa Mkapa kwenye mechi mbili za ligi, ambapo walianza mchezo wa kwanza mbele ya Tanzania Prisons ambapo ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na mchezo wa pili uliokamilisha dakika 180 ilikuwa ni mbele ya Mbeya City wakati Yanga ikishinda bao 1-0. Ikiwa imecheza mechi mbili Uwanja wa Mkapa, Yanga imefunga mabao mawili na kuruhusu kufungwa bao moja ikipotezwa na Simba ambayo imecheza mechi mbili Uwanja wa Mkapa na kufunga jumla ya mabao saba na nyavu za Aishi Manula hazijatikiswa. Mechi ya kwanza ya Simba, Uwanja wa Mkapa ilikuwa dhidi ya Biashara United wakati ikishinda mabao 4-0 kisha ilishinda mabao 3-0 mbele ya Gwambina FC na kuifanya iwe inaidai Yanga mabao matano kwa mechi zao wa

VITA YA KIATU CHA UFUNGAJI BORA NI MOTO NDANI YA LIGI KUU BARA

Image
  IKIWA kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara ni mzunguko wa nne umekamilika huku zikichezwa jumla ya mechi nne ile vita ya kuwania kiatu bora kwa upande wa ufungaji bora inazidi kupamba moto. Kwa sasa tuzo hiyo ipo mikononi mwa Meddie Kagere ambaye msimu wa 2019/20 alitupia jumla ya mabao 22 na timu yake ya Simba ilitwaa ubingwa wa ligi. Kazi imeanza msimu huu ambapo kwenye vita hiyo mambo yapo namna hii:- Prince Dube wa Azam FC yeye ni namba moja akiwa ametupia mabao matatu, mabao mawili aliwatungua Coastal Union Uwanja wa Azam Complex na bao moja aliwatungua Tanzania Prisons Uwanja wa Nelson Mandela. Meddie Kagere wa Simba yeye ana mabao mawili aliwafunga Biashara United na Gwambina FC ilikuwa Uwanja wa Mkapa. Clatous Chama wa Simba ana mabao mawili aliwafunga Biashara United Uwanja wa Mkapa. Chris Mugalu  wa Simba yeye ana mabao mawili aliwafunga Biashara United na Gwambina FC ilikuwa Uwanja wa Mkapa. Mzamiru Yassin wa Simba ana mabao mawili aliwafunga Mtibwa Sugar Uwanja

DAVID KISSU AMPOTEZA MANULA JUMLAJUMLA

Image
  MLINDA mlango namba moja ndani ya Klabu ya Simba, Aishi Manula amenyooshwa mazima ndani ya dakika 360 alizokaa langoni na kipa namba moja wa Azam FC, David Kissu kwa kupotezwa kulinda lango lake bila kuruhusu bao,’Clean Sheet’. Manula anakibarua cha kutetea tuzo yake ya kipa bora ambayo aliipata msimu uliopita wa 2019/20 baada ya kuanza kwa kuyeyusha ‘cleansheet’ za mwanzoni kabisa. Mechi mbili mfululizo ugenini mbele ya Ihefu wakati Simba ikishinda  2-1 Uwanja wa Sokoine na ule Uwanja wa Jamhuri wakati Simba ikilazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 alitunguliwa na amejikusanyia ‘cleansheet’ mbili Uwanja wa Mkapa ilikuwa mbele ya Biashara United wakati Simba ikishinda mabao 4-0 na mbele ya Gwambina wakati Simba ikishinda mabao 3-0. Kwa upande wa Kissu wa Azam FC amempoteza mazima Manula kwa kuwa mechi zake zote nne alizokaa langoni nyavu zake hazijatikishwa ndani ya dakika 360. Alianza mbele ya Polisi Tanzania wakati Azam ikishinda ba 1-0, mbele ya Coastal Union wakati Az

YANGA KUMENYANA NA KMKM LEO AZAM COMPLEX

Image
  KIKOSI cha Yanga leo Septemba 30 kitacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya KMKM ya Zanzibar,utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex. Mchezo huo wa leo ni maalumu kwa ajili ya kujiweka sawa na mechi za Ligi Kuu Bara zinazoendelea ambapo kwa sasa ligi inaingia mzunguko wa tano. Mchezo wa Yanga kwa mzunguko wa tano itakutana na Coastal Union ya Juma Mgunda Uwanja wa Mkapa, Oktoba 4 unatarajiwa kupigwa majira ya saa 1:00 usiku. Yanga mechi yao iliyopita ndani ya ligi wametoka kushinda bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri Morogoro wanakutana na Coastal Union iliyotoka kushinda bao 1-0 mbele ya JKT Tanzania. Coastal Union ipo nafasi ya 14 na pointi zake nne kibindoni huku Yanga ikiwa nafasi ya tatu na pointi zake 10 kibindoni. Inakuwa ni mechi ya pili ya kimarafiki kwa Yanga kucheza ndani ya Uwanja wa Azam Complex ambapo kabla ya kuvaana na Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba ilimenyana na Mlandege ya Zanzibar. Kwenye mchezo huo Yanga ilishinda mabao 2-0 ambapo yalifungw

MSUVA: CORONA IMECHANGIA KUSHUKA KWA THAMANI YA WACHEZAJI WENGI

Image
  THAMANI ya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva, anayeichezea Difaa El Jadida ya Morocco kwa sasa imeonekana kushuka kutoka Sh.2.4 bilioni hadi Sh.1.5 bilioni kwa mujibu wa mtandao wa Transfermarkt.   Msuva ambaye amekuwa akihusishwa na klabu ya Ligi Daraja la Kwanza nchini Ufaransa ‘Ligue 2’, iitwayo Le Havre anashika nafasi ya pili nyuma ya Samatta kati ya wachezaji wa Kitanzania wenye thamani kubwa zaidi.   Samatta anaongoza orodha hiyo akiwa na thamani ya Sh. 25 bilioni huku kwa mujibu wa mtandao huo, akioneka kushuka kwa Sh.7 bilioni tangu alipojiunga na Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu England.   Nyota huyo wa zamani wa Yanga, ameonekana kutokuwa kwenye kiwango bora msimu huu kama ilivyokuwa katika msimu miwili iliyopita ambapo alikuwa miongoni mwa washambuliaji ambao walikuwa wakiwania kiatu cha ufungaji bora wa Ligi Kuu nchini Morocco.   Hadi sasa ambapo imesalia michezo minne kabla ya msimu huu kumalizika ambayo ni dhidi ya Hassania Agadir, Rapide Ou

SIMBA WAANZA KUPIGA MATIZI LEO KUIWINDA JKT TANZANIA

Image
  SIMBA leo wameanza mazoezi kwa ajili ya kujiwinda na mchezo wao wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Oktoba 4 Uwanja wa Jamhuri Dodoma dhidi ya JKT Tanzania. Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kikosi kipo sawa na kinaendelea na programu za mwalimu ili kuweza kufikia malengo ambayo wamejiwekea. "Leo tumeanza na mazoezi maalumu kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya JKT Tanzania, nina amini kwamba utakuwa mchezo mgumu lakini kwa kuwa sisi ni mabingwa lazima tujipange sawasawa. "Kwa upande wa benchi la ufundi baada ya kutoka kushinda mbele ya Gwambina FC wao pia wapo sawa wanatambua kwamba mchezo wetu dhidi ya JKT Tanzania utakuwa na ushindani mkubwa, mashabiki watupe sapoti," amesema. JKT Tanzania itamenyana na Simba ikiwa imetoka kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 mbele ya Polisi Tanzania Uwanja wa Ushirika, Moshi.

LAMINE MORO AONGEZA MKATABA YANGA

Image
  YANGA SC kupitia kwa Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM, Eng. Hersi Said, wamethibitisha kuwa beki wao wa kimataifa, Mghana Lamine Moro ameongeza mkataba wa kuichezea Yanga hadi 2023. Lamine Moro ameongeza mkataba wa kuwatumikia mabosi wake Yanga hadi mwaka 2023. Lamine, raia wa Ghana hivi karibuni iriripotiwa kuwa mkataba wake unakaribia kufika ukingoni jambo ambalo limewafanya mabosi wake kumpa dili jipya kutokana na uwezo wake kuwa ndani ya uwanja. Lamine amesema:-"Ni kweli nimeona vyema kuongeza mkataba, kwanza itanipa  muda zaidi wa kutekeleza majukumu yangu. "Ninapenda kuwaambia mashabiki kuwa ni muhimu kuendelea kushikamana.Nina furaha kubwa ya kuongeza mkataba ndani ya Yanga pamoja.Kuaminiwa na mashabiki pamoja na uongozi kwangu ni furaha nitazidi kupambana kufanikisha malengo ya timu." Beki huyo kisiki alijiunga Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Bidcom ya Zambia mkataba  wake wa awali unamalizika mwishoni mwa msimu uja mwaka 2021. Hivyokwa kusai

KMC:TUMERUDI, HASIRA ZOTE KWA POLISI TANZANIA

Image
  UONGOZI wa KMC umesema kuwa kupoteza kwao mchezo wao wa kwanza mbele ya Kagera Sugar  kwa kufungwa bao 1-0 hakujawatoa kwenye ramani kwani ni sehemu ya mchezo wanajipanga kwa ajili ya mechi yao dhidi ya Polisi Tanzania. KMC ilifanikiwa kucheza mechi tatu ambazo ni dakika 270 bila kupoteza ambapo iliweza kuongoza raundi ya kwanza mpaka ya tatu kabla ya raundi ya nne kupokewa na Azam FC ambao wana pointi 12 kibindoni huku wao wakibakiwa na pointi tisa wakiwa nafasi ya tatu. Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala  amesema kuwa wanaweka kando matokeo yao yaliyopita na kuanza kuivutia kasi Polisi Tanzania watakayokutana nayo Oktoba 5, Uwanja wa Uhuru. “Tulipoteza mchezo wetu uliopita mbele ya Kagera Sugar, imetuumiza kwa kuwa tulianza bila kupoteza hivyo tunaanza tena kurejea kwenye ule moto wetu ambao tulianza nao kwani kikosi chetu kipo imara na tutapambana kufikia malengo yetu. “Mashabiki tunakila sababu za kuwashukuru kwa kuwa wamekuwa nasi bega kwa

OLE GUNNAR AMWAMBIA SANCHO KABLA DIRISHA LA USAJILI HALIJAFUNGWA ATAIBUKIA UNITED

Image
MANCHESTER United inasemekana wana imani watamsajili Jadon Sancho kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Meneja wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amemwambia nyota wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho kuwa dili lake la kujiunga na United litakamilika kwa mujibu wa ripoti ya Dagbladet. Mpaka sasa United walishindwa kutoa fedha ya pauni milioni 108 ambayo Dortumund wanahitaji ili wamuachie kiungo Sancho mwenye uwezo mkubwa ndani ya uwanja. Dirisha la usajili  litafungwa Oktoba 5  lakini, Solskjaer anaonekana kuwa na ujasiri wa wa kumpata Sancho ambae ndio tageti yake ya kwanza msimu huu. Miongoni mwa dili ambalo limezungumzwa kwa muda wote na halijaonesha mafanikio ndani ya united ni la nyota huyu aliyefunga jumla ya mabao 20 msimu uliopita na kutoa pasi 20 kwenye mashindano yote. 

RUVU SHOOTING YATUMA UJUMBE KWA DODOMA JIJI

Image
  UONGOZI wa Ruvu Shooting umesema kuwa utapambana kusaka pointi tatu mbele ya Dodoma Jiji kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara wa raundi ya tano. Ruvu Shooting imetoka kulazimisha sare mchezo wake uliopita wa raundi ya nne ikiwa nyumbani baada ya kukamilisha dakika 90 bila kufungana na Biashara United, Uwanja wa Uhuru. Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa sare waliyoipata sio mbaya kwao kwani walicheza kwa kiwango kikubwa ambacho mashabiki walioshuhudia waliweza kuona ukweli wa Barcelona ya Bongo. "Wengi wanaisahau Ruvu Shooting kwenye ramani ya soka lakini ni moja ya timu ambayo inawatumia vizuri wazawa na wanacheza ule mpira wa pasi nyingi mithili ya Barcelona. "Tumetoka kupata sare mbele ya Biashara United tunatambua kwamba ilikuwa mchezo mgumu kumalizana nao lakini tupo vizuri kwenye upande wa suala la kucheza mpira mzuri ndani ya uwanja ambao mashabiki wenyewe wanakubali. "Ukiwa ugenini unacheza kwa kujiamini,

YANGA WAFIKIA PAZURI NA WAHISPANIA WA LA LIGA

Image
  KAMPUNI ya La Liga ya nchini Hispania inatarajiwa kukabidhi ripoti ya mwisho ya mapendekezo yao kwa uongozi wa Yanga uliokuwa chini ya Mwenyekiti Mkuu wa timu hiyo, Dr Mshindo Msolla.   La liga ndiyo wamepewa jukumu la kupendekeza mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo baada ya hivi karibuni kuingia makubaliano mazuri ya kushirikiana katika masuala ya kimichezo.   Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alisema kuwa Oktoba, mwaka huu mapema wataipokea ripoti hiyo kutoka La liga kupitia klabu ya Sevilla ya nchini Hispania.   Mwakalebela alisema kuwa mchakato umefikia hatua nzuri na ripoti hiyo ni ya mwisho tayari kuelekea hatua inayofuata katika kukamilisha mchakato huo wa mfumo wa mabadiliko.   Aliongeza kuwa baada ya hatua ya kwanza ya makabidhiano, watapata utaalamu wa ndani, na baadaye watautoa nje kwa kushirikisha matawi yote ya Yanga nchini nzima.   “Baada ya kupata utaalamu huo katika matawi yote ya Yanga kuelimisha na kupata ushauri wa wanachama kutokana na

SIMBA YAANZA KUIPIGIA HESABU JKT TANZANIA

Image
 UONGOZI wa Simba umesema kuwa leo Septemba 28 utaanza mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa kuelekea Kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania.  Simba itakuwa ugenini Oktoba 4, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ambapo itamenyana na JKT Tanzania. Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa leo wataanza na mazoezi ya Gym kisha jioni watafanya mazoezi Uwanja wa Bunju. "Tumetoka kushinda mabao 3-0 mbele ya Gwambina FC,  program ya Kwanza ilikuwa mapumziko jana na leo asubuhi mazoezi ya Gym na jioni tutakuwa Uwanja wa  Bunju. "Kikubwa tunahitaji kuendelea kupata matokeo kwenye mechi zetu na mchezo wetu ujao itakuwa ni dhidi ya JKT Tanzania, mashabiki waendelee kutupa sapoti," amesema.  Simba imetoka kushinda mbele ya Gwambina Uwanja wa Mkapa inakutana na JKT Tanzania ambayo imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

KISSU AWEKA REKODI YA KIBABE NDANI LIGI KUU BARA

NAMUNGO FC YAIPIGIA HESABU MWADUI FC

Image
  UONGOZI wa Namungo FC umesema kuwa kwa sasa hesabu zao kubwa ni kwenye mchezo wao wa ligi dhidi ya Mwadui FC ambao utakuwa ni wa raundi ya tano. Namungo inayonolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery imetoka kushinda mchezo wake uliopita kwa bao 1-0 mbele ya Mbeya City Uwanja wa Sokoine. Bao la ushindi wa Namungo lilipachikwa na mshambuliaji wao namba moja, Bigirimana Blaise mwenye mabao mawili ndani ya ligi. Ofisa Habari wa Namungo FC, Kidamba Namlia amesema kuwa ushindi wao kwenye mechi iliyopita unawapa nguvu ya kujipanga kwa mechi zao zijazo ikiwa ni pamoja na ule dhidi ya Mwadui FC. "Tumefunga hesabu za mzungukuko wa nne kwa ushindi mbele ya Mbeya City kinachofuata ni kusaka pointi tatu mbele ya Mwadui FC. "Kwa namna ligi inavyokwenda hata ukiwa nyumbani unaweza kufungwa maana maana hata sisi tulishinda ugenini na tulipoteza pia nyumbani tunaamini utakuwa mchezo mgumu," amesema. Namungo itamenyana na Mwadui FC, Uwanja wa Majaliwa Oktoba 3 ambayo imetoka

KOCHA WA SIMBA AIBUKIA KWENYE BAO LA WAWA

SABABU YA KISINDA NA TONOMBE KUTOITWA TIMU YA TAIFA HII HAPA

KLOPP ACHEKELEA KUITUNGUA ARSENAL MABAO 3-1

Image
  JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa timu hiyo ina jukumu la kuendelea kushinda kila mechi ndani ya Ligi Kuu England ili kuweza kutetea taji lao. Liverpool ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe hilo usiku wa kuamkia leo waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 mbele ya Arsenal inayonolewa na Mikel Arteta kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Anfield. Arsenal ilianza kuwatungua Liverpool dakika ya 25 kupitia kwa Alexandre Lacazette lilidumu kwa muda wa dakika mbili pekee kwani Liverpool waliweka mzani sawa kupitia kwa Sadio Mane dakika ya 28. Wakati Arsenal inayomtegemea Pierre Emerick Aubameyang kwenye upande wa kutupia mabao ikihaha kutafuta ushindi ilitunguliwa bao la pili dakika ya 34 na Andrew Robertson na dakika ya 88 msumari wa tatu ulipachikwa na Diogo Jota. Klopp amesema kuwa ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kushinda tena taji la Ligi Kuu England kazi yao ni moja kuendelea kushinda mechi zao zote. "Haikuwa rahis

LUIS MIQUSSONE AMESHINDIKANA JUMLAJUMLA

MWINYI ZAHERA: KWA MWENDO WA SIMBA, KIMATAIFA HAWAFIKI POPOTE

Image
  MWINYI Zahera, Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi ndani ya Klabu ya Gwambina FC amesema kuwa Simba hawatafika mbali kwenye michuano ya kimataifa ikiwa watacheza kama walivyocheza na wao. Zahera aliwahi kuwa Kocha Mkuu wa Yanga msimu wa 2018/18 na 2019/20 alipigwa chini kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni timu yake kuboronga michuano ya kimataifa. Simba, Septemba 26 ilicheza na Gwambina mchezo wa Ligi Kuu Bara na kushinda mabao 3-0 ukiwa ni mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku. Zahera amesema kwa namna ambavyo Simba walicheza hamsini kwa hamsini na kama watacheza hivi kwenye mashindano ya kimataifa hawatafika kokote. "Nimeona Simba ikicheza ni inacheza vizuri na inapenda kucheza mpira wa pasi, sasa ukiangalia namna ambavyo walicheza na timu yetu ni kwamba tuliweza kwenda nao sambamba mwanzo mwisho licha ya kwamba tumepoteza. "Wana kazi kubwa ya kufanya kimataifa hasa kwa aina ya mchezo wanaocheza, kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hawatakutana

KUMBE, BOBAN ALIYEMTUNGUA MANULA WA SIMBA MAMBO YALIKUWA MAGUMU MBELE YA YANGA

Image
 ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar aesema kuwa mchezaji wake Boban Zirintusa kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga uliochezwa Septemba 27, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro wakati wakipoteza kwa kufungwa bao 1-0 mpira ulimkataa jambo lilimfanya akamtoa mapema. Zirintusa bado hajasaulika kwa mlinda mlango namba moja wa Simba Aishi Manula baada ya kumtungua bao moja kwenye sare ya kufungana bao 1-1 wakati Simba iipocheza nao Uwanja wa Jamhuri kwenye mchezo wa ligi. Wakati timu yake ya Mtibwa ikipoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Yanga nyota huyo ambaye alitibua 'clean sheet' ya Manula alitumia dakika 36 na nafasi yake kuchukuliwa na Juma Nyangi. Katwila amesema:"Unajua mpira ni mbinu sasa kwa namna ambavyo nilimuona Zirintusa kwenye mchezo wetu dhidi ya Yanga mbinu zangu kwake zilikwaa hasa kwenye mipira ya juu ambayo ilikuwa inapotea kwake. "Nilimuona anapata tabu uwanjani, alikuwa anazungukazunguka kutafuta mipira huku ile ya juu akiwa anapishana nayo jambo a