NAMUNGO FC YAIPIGIA HESABU MWADUI FC

 


UONGOZI wa Namungo FC umesema kuwa kwa sasa hesabu zao kubwa ni kwenye mchezo wao wa ligi dhidi ya Mwadui FC ambao utakuwa ni wa raundi ya tano.


Namungo inayonolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery imetoka kushinda mchezo wake uliopita kwa bao 1-0 mbele ya Mbeya City Uwanja wa Sokoine.


Bao la ushindi wa Namungo lilipachikwa na mshambuliaji wao namba moja, Bigirimana Blaise mwenye mabao mawili ndani ya ligi.


Ofisa Habari wa Namungo FC, Kidamba Namlia amesema kuwa ushindi wao kwenye mechi iliyopita unawapa nguvu ya kujipanga kwa mechi zao zijazo ikiwa ni pamoja na ule dhidi ya Mwadui FC.


"Tumefunga hesabu za mzungukuko wa nne kwa ushindi mbele ya Mbeya City kinachofuata ni kusaka pointi tatu mbele ya Mwadui FC.


"Kwa namna ligi inavyokwenda hata ukiwa nyumbani unaweza kufungwa maana maana hata sisi tulishinda ugenini na tulipoteza pia nyumbani tunaamini utakuwa mchezo mgumu," amesema.

Namungo itamenyana na Mwadui FC, Uwanja wa Majaliwa Oktoba 3 ambayo imetoka kushinda kwa mabao 2-0 mbele ya Ihefu FC.



Comments

Popular posts from this blog

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA