KMKM WATIA TIMU DAR, KIINGILIO BUKU TANO TU

 



TIMU ya KMKM SC ya Zanzibar  imewasili leo Septemba 30 Dar tayari kwa mchezo wa kirafiki leo dhidi ya Yanga utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Mchezo huo wa kirafiki unatarajiwa kupigwa majira ya saa 1:00 usiku ukiwa na malengo ya kukiweka sawa kikosi cha Yanga kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara.

Mechi hiyo kiingilio cha 5,000 mzunguko na 10,000 VIP. 


Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Zlatko Krmpotic ipo kwenye maandalizi ya mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 3, Uwanja wa Mkapa.



Comments

Popular posts from this blog

ISHU YA MORRISON KUHUSU MKATABA WAKE IPO MIKONONI MWA KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI

BREAKING: MASHABIKI RUKSA KWENDA UWANJANI, UTARATIBU WATAJWA

AFRICAN LYON WADAI KUWA WAZO LA VISIT TANZANIA NA LOGO MPYA YA SIMBA IMETOKA KWAO