LAMINE MORO AONGEZA MKATABA YANGA

 


YANGA SC kupitia kwa Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM, Eng. Hersi Said, wamethibitisha kuwa beki wao wa kimataifa, Mghana Lamine Moro ameongeza mkataba wa kuichezea Yanga hadi 2023.
Lamine Moro ameongeza mkataba wa kuwatumikia mabosi wake Yanga hadi mwaka 2023.

Lamine, raia wa Ghana hivi karibuni iriripotiwa kuwa mkataba wake unakaribia kufika ukingoni jambo ambalo limewafanya mabosi wake kumpa dili jipya kutokana na uwezo wake kuwa ndani ya uwanja.

Lamine amesema:-"Ni kweli nimeona vyema kuongeza mkataba, kwanza itanipa  muda zaidi wa kutekeleza majukumu yangu.

"Ninapenda kuwaambia mashabiki kuwa ni muhimu kuendelea kushikamana.Nina furaha kubwa ya kuongeza mkataba ndani ya Yanga pamoja.Kuaminiwa na mashabiki pamoja na uongozi kwangu ni furaha nitazidi kupambana kufanikisha malengo ya timu."

Beki huyo kisiki alijiunga Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Bidcom ya Zambia mkataba  wake wa awali unamalizika mwishoni mwa msimu uja mwaka 2021. Hivyokwa kusaini kwake dili jipya kunamfanya Lamine kuendelea kubaki mitaa ya Jangwani  hadi Julai 2023.

Ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa amecheza mechi tatu msimu wa 2020/21 amefunga mabao mawili akiwa ni kinara wa kutupia mabao ndani ya Yanga iliyofunga mabao manne ikiwa imecheza mechi nne.



Comments

Popular posts from this blog

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA