BARCELONA NI MWENDO WA SARE, MESSI AFIKISHA MABAO 700
LIONEL Messi, staa ndani ya Klabu ya Barcelona usiku wa kuamika leo alifunga bao moja kwenye sare ya kufungana mabao 2-2 na Atletico Madrid Uwanja wa Nou Camp kwenye La Liga na kufikisha jumla ya mabao 700. Raia huyo wa Argentina anayekipiga pia kwenye timu ya taifa alifunga bao hilo kwa penalti kwa kupiga penalti ya panenka iliyozama ndani ya nyavu na kumshinda mlinda mlango wa Atletico Madrid, Jan Oblak. Messi ametoka kutoka kwenye jumla ya mabao 699 aliyokuwa nayo kibindoni baada ya kufunga bao mbele ya Leganes wiki mbili zilizopita na alishindwa kufurukuta kwenye mechi tatu zilizopita ikiwa ni mbele ya Sevilla, Athletic Bilbao na Celta Vigo kabla ya kuibuka mbele ya Atletico na kufunga bao hilo. Nyota huyo mwenye miaka 33,anaongoza kwa kutupia ndani ya Barcelona akiwa amefunga jumla ya mabao 630 kwenye timu yake huku akitupia jumla ya mabao 70 kwenye timu yake ya taifa ya Argentina. Mabao ya Barcelona yalifungwa na Diego Costa aliyejifunga dk 11 na Messi alifunga bao lake la...