BERNARD MORRISON NI PASUA KICHWA NDANI YA YANGA, ATIMKA


INAELEZWA kuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison ametoroka kambini jana wakati wachezaji walipokuwa wakijiaandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Kagera Sugar.

Kwenye mchezo huo Morrison hakuwa sehemu ya mchezo ambapo Yanga iliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar.

Morrison amekuwa kwenye mvutano mkubwa na uongozi wa Yanga kwa sasa ambapo ishu kubwa inaeelezwa kuwa ni kuhusu mkataba wake ambao kila mmoja anasema jambo lake.

Uongozi wa Yanga unasema kuwa Morrison ana kandarasi ya miaka miwili huku mchezaji mwenyewe akieleza kuwa ana mkataba wa miezi sita ambao unameguka msimu utakapoisha.

Habari zinaeleza kuwa wakati wachezaji wakiwa kambini huku ulinzi ukiwa ni mkali Morrison alimua kusepa na alipobanwa aliwazidi ujanja walinzi na kusepa zake kuendelea na mipango yake mingine.

 Morrison ametupia jumla ya mabao matatu na ana pasi tatu ndani ya ligi huku kwenye Kombe la Shirikisho akiwa ametupia bao moja.


Comments

Popular posts from this blog

ISHU YA MORRISON KUHUSU MKATABA WAKE IPO MIKONONI MWA KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI

BREAKING: MASHABIKI RUKSA KWENDA UWANJANI, UTARATIBU WATAJWA

AFRICAN LYON WADAI KUWA WAZO LA VISIT TANZANIA NA LOGO MPYA YA SIMBA IMETOKA KWAO