Posts

Showing posts from July, 2020

BEKI WA KIMATAIFA ASAINI YANGA MIAKA MIWILI, KUTUA BONGO MUDA WOWOTE

Image
BEKI wa kushoto wa kimataifa wa Rwanda anayeichezea Rayon Sports, Eric Rutanga ni mali ya Yanga baada ya kusema kuwa ameshasaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo. Hivi karibuni Yanga kupitia kwa Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Hersi Said alisema kuwa baadhi ya wachezaji wataanza kuwasili nchini hivi karibuni baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu Bara, ishara inayoonyesha kuwa Rutanga atatua nchini siku chache zijazo. Rutanga amesema kuwa tayari ameshamalizana na Yanga baada ya kukubali kusaini mkataba wa miaka miwili ambapo alisema kuwa iliwabidi Yanga wamtumie mkataba kwa njia ya mtandao ‘Email’ kwa kuwa mipaka ya Rwanda haijafunguliwa. “Namshukuru Mungu kila kitu kimeenda sawa kama ambavyo nilikuwa nikitarajia, tayari tumeshamalizana na Yanga na nimesaini mkataba wa kuitumikia kwa miaka miwili, hivyo uongozi wa Yanga umeniambia nisubiri mipaka itakapofunguliwa ya Rwanda watanitumia tiketi ya ndege. “Hapo awali nilikuwa na mashaka kwa kuwa mipaka ilikuwa imefungwa hi

KUMBE PICHA LA MORRISON KUKAMATWA NA POLISI ISHU ILIKUWA BALAA

Image
NYOTA raia wa Ghana, Bernard Morrison ameingia katika sekeseke jingine baada ya kukamatwa na kushikiliwa kwa muda na Polisi wa Kituo cha Oysterbay jijini Dar es Salaam. Morrison alishikiliwa na Polisi ambao waliisimamisha gari aliyokuwa amekodi ya Uber na kumuambia wamesikia harufu ya bangi. Kwa mujibu wa mashuhuda, walieleza Morrison akiwa na dereva wa Uber aliwaruhusu askari hao kuanza kupekua kama kweli wameona au wataona bangi, lakini haikuwa hivyo. "Baadaye wakasema kwamba wanataka simu ya Morrison, jamaa akagoma kuitoa na kucharuka sana akisema hawezi kuwapa na wako tayari wampeleka Polisi. "Basi ukaibuka mzozo na dereva wa Uber akaanza kuwaamua akiwasisitiza kwamba kama wamehisi kuna bangi kwenye gari wakague kwa kuwa yeye havuti “jani” na wala mteja wake hakufanya hivyo. “ Basi wale askari wasisitiza walitaka simu ya Morrison, baadaye wakawachukua wakisema wanawapeleka Kituo cha Oysterbay huku Morrison akisema watu wa Yanga ndiyo wanamfanyia vile,” kiliel

ISHU YA AUBAMEYANG KUTAJWA CHELSEA YAZUA MSHTUKO

Image
PIERRE-Emerick Aubameyang, mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Arsenal anatajwa kuingia anga za Chelsea ambao leo wanakutana nao kwenye Fainali ya FA jambo lililowashtua mabosi wa timu hiyo. Aubameyang mwenye miaka 31, raia wa Gabon amekuwa kwenye mvutano mkubwa juu ya kuongeza dili lake jipya ndani ya timu hiyo huku akigoma kuweka wazi kwamba anaweza kuongeza kandarasi ndani ya timu hiyo. Nyota huyo alimwaga wino ndani ya kikosi cha washika bunduki akitokea Klabu ya Borussia Dortmund kwa thamani ya paundi milioni 56 mwaka 2018 na ametupia zaidi ya mabao 49 ndani ya Ligi Kuu England. Chelsea iliyo chini ya Kocha Mkuu, Frank Lampard inasaka mshambuliaji kwa sasa ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao na Auba anapewa nafasi ya kuwekwa kwenye rada zake. Aubameyang ametupia jumla ya mabao 27 kwa msimu huu kwenye mashindano yote pia anatajwa kuingia anga za Barcelona na AC Milan ambao nao wanahitaji saini ya nyota huyo aliye chini ya Kocha Mkuu, Mikel Arteta.

TUZO ZA MO DEWJI ZAYEYUKA MAZIMA, SABABU YATAJWA

Image
UONGOZI wa Klabu ya Simba umefunguka kuwa safari hii hawatarajii kuwa na Tuzo za Mo kama walivyofanya misimu miwili iliyopita kutokana na muda kutokuwa rafiki kwao. Simba chini ya Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi, Mohamed Dewji ‘Mo’ imekuwa na utaratibu wa kuwapa tuzo wachezaji wa kikosi hicho pamoja na viongozi wa benchi la ufundi katika misimu miwili mfululizo iliyopita kutokana na kutambua mchango wao. Katika msimu uliopita wachezaji kadhaa waliweza kukabidhiwa tuzo akiwemo mshambuliaji bora, Meddie Kagere.  Katibu Mkuu wa Simba, Arnold Kashembe alisema: “Safari hii hatutakuwa na Tuzo za Mo kutokana na kipindi kile cha Corona ligi ilisimama miezi mitatu, baadhi ya wachezaji walibaki hapahapa hawakuondoka, hivyo kwa sasa wanahitaji kupata mapumziko mafupi kabla ya kuanza msimu mpya. “Wachezaji wa kimataifa wanatakiwa wapate mapumziko na kipindi cha maandalizi ya msimu mpya, pia tunahitaji kujipanga kwa ajili ya msimu ujao.” Chanzo: Championi

ISHU YA MAKAZI YA MORRISON WA YANGA NI PASUA KICHWA

Image
KAIMU Katibu Mkuu wa Yanga, Patrick Simon amesema kuwa hawajampa makazi mchezaji wao Bernard Morrison ila wanahusika kwenye kumlipia kodi. Morrison kwa sasa yupo kwenye mvutano na klabu ya Yanga kwenye upande wa mkataba, Morrison anadai kuwa mkataba wake ni wa miezi sita umekwisha huku Yanga wakieleza kuwa ana dili la miaka miwili. “Morrison hatukuwa tumempa makazi ila tulimwambia atafute nyumba sisi tutalipia kwa hiyo nikisema amehama makazi nitakuwa nadanganya kwa watanzania.  "Ambacho tunakifanya sisi kwa sasa tunamlipia kodi na mpaka sasa hivi tunafanya hivyo.”

YANGA WAMEAMUA SASA, WAMALIZANA NA MASHINE YA KAZI YA AS VITA

Image
BAADA ya Yanga kukamilisha dili la winga wa AS Vita, Tuisila Kisinda, hatimaye timu hiyo imekamilisha tena usajili wa kiungo wa timu hiyo, Mukoko Tonombe. Tonombe amekuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha AS Vita akicheza kama kiungo mkabaji pamoja na timu ya taifa ya DR Congo. Chanzo chetu cha kuaminika ndani ya AS Vita, kililiambia Spoti Xtra kuwa, Yanga tayari walishamalizana na wachezaji hao ambao kwa sasa wanasubiri viwanja vya ndege nchini kwao kufunguliwa ili waweze kuwasili Tanzania. Mtoa taarifa huyo aliongeza kuwa, hata kama viwanja vya ndege vitaendelea kufungwa, wachezaji hao wataondoka nchini humo kwa njia ya barabara. “Yanga walianza kumalizana na Tuisila Kisinda na baadae wakaja kumalizana na Mukoko Tonombe, hivyo kinachosubiriwa kwa sasa ni ndege kuruhusiwa kuruka ili wachezaji hao waweze kuja huko Tanzania. “Kwa mujibu wa wachezaji wenyewe walisema kuwa uongozi wa Yanga umewaambia kama viwanja vya ndege vitafunguliwa mapema basi watatumiwa tiketi ya ndege, i

NIYONZIMA ALIYEKUWA ANAWINDWA NA YANGA ANUKIA AZAM FC

Image
INAELEZWA kuwa Yanga imeamua kumpotezea kiungo anayekipiga Rwanda ndani ya Klabu ya Rayon Sports,  Ally Niyonzima baada ya kupata saini ya mbadala wake. Awali Yanga ilikuwa kwenye mazungumzo na nyota huyo anayekipiga timu ya Taifa ya Rwanda na sasa anatajwa kuingia anga za Azam FC.  Habari kutoka ndani ya Yanga zimeeleza kuwa:"Kweli tulishaanza mazungumzo na kiungo Niyonzima ila baada ya kuipata saini ya moja ya viungo tumeamua kuachana naye. "Ni kiungo mzuri ila tuliyempata naye ni bora pia hivyo atafanya kazi ndani ya Yanga kwa kuwa tumeshamalizana naye kila kitu," ilieleza taarifa hiyo.  Kiungo huyo anatajwa kutua Yanga ni Zawadi Mauya ambaye anatajwa kuwa mbadala wa Papy Tshishimbi raia wa Congo ambaye amegomea kuongeza kandarasi nyingine. Ofisa Habari wa Azam FC,  Zakaria Thabit amesema kuwa suala la usajili kwa nyota watakaotua itawekwa wazi.

SIMBA YAJIFUA LEO SUMBAWANGA KUELEKEA MCHEZO WA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO

Image
KIKOSI cha Simba leo kimefanya mazoezi kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa Shule ya  St. Maurus ikiwa ni maandalizi ya kuelekea mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Namungo FC.  Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Agosti 2, Uwanja wa Nelson Mandela unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili. Simba ipo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck na Namungo FC ipo chini ya Kocha Mkuu Hitimana Thiery. Sven amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na anaamini mchezo utakuwa mgumu licha ya wengi kuipa nafasi timu yake kushinda. Thiery amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo licha ya wachezaji wake wengi kusumbuliwa na typhoid na Malaria. Namungo ina tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho kwa kuwa Simba inaiwakilisha nchi Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutwaa taji la Ligi Kuu Bara.

KESHO NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI USIPANGE KUKOSA NAKALA YAKO

Image
Kesho ndani ya Championi Jumamosi usipange kukosa nakala yako 

DILI LA MWAMNYETO YANGA LIMEFIKIA HAPA

Image
BAKARI Mwamnyeto, beki chipukizi anayekipiga ndani ya Coastal Union inaelezwa kuwa ameshatua Dar akitokea Tanga kwa ajili ya kukamilisha dili la kujiunga na Yanga. Habari zinaeleza kuwa wakati wowote kuanzia leo nyota huyo atamalizana na Yanga ambao wamepania kujipanga kwa ajili ya msimu ujao wa 2020/21. "Mwamnyeto ameshatua ndani ya Bongo huenda akamalizana na Yanga muda wowote kuanzia sasa,ila kinachochelewesha ni dau tu la usajili wake. "Anahitaji apewe milion 70, mabosi wanataka waanze na milioni 30 kisha zilizobaki watammalizia baadaye, ninaamini hawatazembea kwani Azam FC nao wanahitaji saini yake hivyo hawatakubali yatokee kama yale ya Awesu," ilieleza taarifa hiyo. Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa hawana presha na usajili wa msimu huu watafanya mambo makubwa kwa kuzingatia utaalamu wa kazi.

SIMBA WANA BALAA KILA KONA WAKIMBIZA KWENYE TUZO ZA MCHEZAJI BORA, ORODHA YA WACHEZAJI 30 HII HAPA

Image
Hii hapa orodha ya wachezaji 30 waliochaguliwa kuingia kwenye mchakato wa kusaka mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara,2019/20 baadaye watapunguzwa kufika 10:- Nico Wadada, Idd Seleman 'Nado' na Obrey Chirwa (Azam FC), Abdulmajid Mangaro, Daniel Mgore, (Biashara United), Ayoub Lyanga na Bakari Mwamnyeto, (Coastal Union),David Luhende, Yusuph Mhilu na Awesu Awesu (Kagera Sugar) Wazir Junior, (Mbao). Lukas Kikoti, Bigirimana Blaise na Relliants Lusajo,(Namungo FC), Shomari Kapombe, Meddie Kagere, Aishi Manula,Clatous Chama,Francis Kahata,John Bocco, Jonas Mkude na Luis Miqussone wa Simba. Mapinduzi Balama, Deus Kaseke, David Molinga, Juma Abdul na Feisal Salum wa Yanga,Martin Kigi wa Alliance, Daruesh Saliboko wa Lipuli FC na Marcel Kaheza wa Polisi Tanzania. 

VIDEO:TARIMBA 'TUNALIPA HADI BILIONI 2 KWA MWEZI, SportPesa

Image

YANGA YAANZA NA JEMBE LA KAGERA SUGAR, INAELEZWA NI MRITHI WA TSHISHIMBI

Image
KIUNGO mkabaji wa Kagera Sugar, Zawadi Peter Mauya,  amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga SC. Mauya amesaini mbele ya  Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM inayoidhamini Yanga,  Injinia Hersi  Said, huku Kaimu Katibu wa Yanga, Wakili Simon Patrick akishuhudia. Usajili wa kiungo huyo unakuja ikiwa ni siku chache baada ya Yanga kumpa siku 14, Papy Tshishimbi za kuamua hatma yake. Inavyoonekana usajili wa kiungo huyo ni maandalizi kwa Yanga kujiandaa kuanza maisha mapya bila ya Tshishimbi ambaye kwa muda mrefu wamekuwa wakivutana katika suala la kusaini mkataba mpya. Huu unakuwa usajili wa kwanza kwa Yanga kuelekea msimu ujao ambapo viongozi pamoja na wadhamini Kampuni ya GSM, wametamba kukisuka upya kikosi chao.

KUMEKUCHA, SIMBA YATAJA MAJEMBE YATAKAYOPIGWA CHINI NDANI YA KIKOSI

Image
UONGOZI wa Simba umetangaza kuwa wachezaji watakaobaki kuendelea kuvaa jezi za timu hiyo msimu ujao ni wale walioonyesha ubora mkubwa msimu huu wa 2019/2020. Kwa maana hiyo, wachezaji ambao huenda Simba ikaachana nao kutokana na kutotoa mchango mkubwa katika timu hiyo ni Yusuph Mlipili, Tairone do Santos, Rashid Juma, Haruna Shamte na Sharraf Eldin Shiboub. Wakati timu hiyo ikipanga kutembeza panga hilo, tayari wapo wachezaji wanaohusishwa kujiunga na timu hiyo kwa msimu ujao ambao ni Michael Sarpong, Bernard Morrison na Bakari Mwamnyeto. Akizungumza na Spoti Xtra, Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa alisema kuwa soka siyo mchezo wa kujificha, wale wachezaji walioonyesha na wasioonyesha ubora wao wameonekana, hivyo benchi la ufundi na uongozi hawatatumia nguvu kuwaondoa kikosini walioshindwa kuendana na kasi ya timu. Senzo alisema kuwa kazi ngumu ipo kwenye usajili wa wachezaji pekee kwa kutumia ripoti ya kocha wao Mbelgiji, Sven Vandenbroeck ili kuhakikisha wanawapata n

YANGA YAGONGANA NA AZAM FC ZAKUTANA KWA KIPA WA KAGERA SUGAR KUSAKA SAINI YAKE

Image
INAELEZWA kuwa mabosi wa Yanga wanamvutia kasi kipa namba moja wa Kagera Sugar, Benedickt Tinoco ili aongeze nguvu katika kikosi chao msimu ujao. Vita yao sasa inaongezewa makali na Azam FC ambao nao pia wameshapaki basi lao ndani ya Kagera Sugar wakianza na Awesu Awesu ambaye ni kiungo aliyekuwa pia kwenye rada za Yanga. Habari kutoka ndani ya Yanga zimeeleza:"Yanga inafanya maboresho ya kikosi kwa sasa inahitaji kuwa na ushindani kwenye namba zote kuanzia kipa mpaka wachezaji wa ndani. "Tinoco wa Kagera Sugar anaweza kuibuka ndani ya Yanga kwani ana uwezo mkubwa na anakubalika hivyo anaweza kuibukia Yanga siku ya Mwanachi akaendeleze kutoa changamto kwa Metacha Mnata, Faroukh Shikhalo na Ramadhan Kabwili," ilieleza taarifa hiyo. Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa hawakuwa na msimu mzuri ndani ya 2019/20 kwa sasa wanajipanga kwa ajili ya msimu ujao. "Kuna mambo mazuri yanakuja kwani hatukuwa na wakati mzuri msimu huu hivyo tunajipanga kw

DUCHU WA LIPULI AMALIZANA NA SIMBA, AJIFUNGA MIAKA MIWILI

Image
DAVID Kameta,'Duchu' beki wa Klabu ya Lipuli FC inaelezwa kuwa amesaini kandarasi ya miaka miwili ndani ya Klabu ya Simba. Beki huyo msimu huu amekuwa kwenye ubora wake ndani ya Lipuli ambapo amefunga mabao matatu na kutoa pasi saba za mabao. Timu yake ya Lipuli imeshuka daraja baada ya kufikisha pointi 44 ikiwa nafasi ya 18 hivyo msimu ujao itashiriki Ligi Daraja la Kwanza.

HIVI DIVYO YANGA ITAKAVYOMTABULISHA JAMES KOTEI AGOSTI 9, NYOTA WENGINE 9 NDANI

Image
YANGA imedhamiria kuimarisha kikosi chao kuelekea msimu ujao ambapo mabosi wa Kamati ya Usajili chini ya udhamini wa GSM wameandaa sapraizi kubwa kwa mashabiki wao itakayofanyika katika kilele cha Tamasha la Wiki ya Mwananchi. Timu hiyo imepanga kukiboresha kikosi chao kwa kusajili wachezaji tisa watakaoingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo msimu ujao. Tayari wapo baadhi ya wachezaji wanaotajwa kwenye usajili wa timu hiyo, kati ya hao ni kiungo Mkongomani,Mukoko Tonombe anayekipiga AS Vita ya DR Congo, Eric Rutanga (Rayon Sports), Tuisila Kisanda (AS Vita), Heritier Makambo (Horoya AC) na Yacouba Songne ambaye ni mchezaji huru. Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, rasmi kilele cha tamasha kubwa la Wiki ya Mwananchi litafanyika Agosti 9, mwaka huu ambapo siku hiyo, Yanga wataitumia kutambulisha wachezaji wao wa msimu ujao wa 2020/21. Kati ya watakaotambulishwa ni kiungo mkabaji wa zamani Simba, Mghana, James Kotei.Mtoa taarifa huyo alisema ku

WATATU WAPIGWA PANGA MAZIMA NDANI YA AZAM FC

YANGA WACHUKUA MAAMUZI MENGINE KUHUSU BERNARD MORISSON

Image
KAIMU Katibu Mkuu wa Yanga, Patrick Simon amesema kutokana na matukio ya Bernard Morrison ya utovu wa nidhamu amepelekwa kwenye Kamati ya Maadili. Morrison hajajiunga na timu kwa sasa ambapo mara ya mwisho kuonekana akiwa na Yanga ilikuwa ni Julai 12, Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba. Baada ya mchezo huo ambapo Morrison alitolewa dakika ya 64 na nafasi yake kuchukuliwa na Patrick Sibomana aliondoka jumla uwanjani na kwa sasa amekuwa akionekana akicheza mechi za mtaani huku akieleza kuwa anahofia kupigwa ikiwa anakwenda mazoezini. “Kwanza nimeshachoka habari za Morrison lakini ni kwamba kuna kamati ya maadili ya Yanga inashughulikia suala lake muda si mrefu watalitolea maamuzi kwa sababu yametokea matendo ya kujirudia, ilibidi tumpeleke kwenye kamati ya maadili ambayo ni huru mimi sipo kwenye hiyo kamati. “Kwa hiyo wanafanya taratibu zao wameshamwalika kumsikiliza na kufanya taratibu zao halafu watatoa uamuzi wao, sisi tunawasubiri wao pamoja

OLIVIER GIROUD YUPO KARIBU KUTIMKIA ITALIA

Image
OLIVIER Giroud, nyota wa Klabu ya Chelsea inaelezwa kuwa yupo kwenye hesabu za kuondoka ndani ya kikosi hicho na kuibukia ndani ya Inter Milan inayoshiriki Serie A, nchini Italia. Kocha Mkuu wa Inter Milan, Antonio Conte ambaye alikuwa ni kocha wa Chelsea inaelezwa kuwa amevutiwa na nyota huyo jambo ambalo limeongeza nafasi ya nyota huyo kuondoka ndani ya Chelsea kwa sasa. Frank Lampard, Kocha Mkuu wa Chelsea bado hajawa tayari kumruhusu mshambuliaji huyo aondoke kwa kuwa bado anaamini ana nafasi ndani ya kikosi hicho cha Chelsea kwa sasa na amekuwa na ushirikiano mkubwa na wachezaji wenzake. Kesho, Agosti Mosi, Chelsea ina kazi ya kumenyana na Chelsea kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Arsenal na Giroud anatarajiwa kuanza kikosi cha kwanza Uwanja wa Wembely.   Nyota huyo mwenye miaka 33 raia wa Ufaransa amekuwa kwenye ubora wake chini ya Lampard, kesho anakutana na Arsenal ambao walikuwa ni mabosi wake wa zamani kwenye fainali.

NAHODHA TSHISHIMBI ATAJA HATMA YAKE NDANI YA YANGA

Image
NAHODHA wa Yanga, Papy Tshishimbi amesema kuwa kuhusu kubaki ndani ya Yanga msimu ujao anamwachia Mungu. Mkataba wa Yanga na Papy Tshishimbi unafika tamati mwezi Agosti ambao kwa sasa umebakiza siku moja kwa kuwa leo ni Julai 31, kesho ni Agosti Mosi kabla ya nyota huyo kufikia siku yake aliyosaini kuwa mchezaji huru. Kumekuwa na mvutano mkubwa wa nyota huyo na Yanga kuhusu suala lake la kuongeza kandarasi mpya hali ambayo imemfanya nyota huyo kutomwaga saini mpaka sasa licha ya kupewa mkataba. "Suala la mimi kubaki ndani ya Yanga kwa msimu ujao ninamuachia Mungu kwani nimekuwa nikiskia habari nyingi ambazo zinanizungumzia mimi lakini hazina ukweli. "Naona viongozi wameanza kufanya mambo ambayo sio mazuri kwa kuzungumza kwamba wamenipa mkataba na kunipa siku za kusaini jambo ambalo sio sawa unapozungumzia mkataba sio jambo la kuzungumza kwenye vyombo vya habari. "Kwa sasa sina furaha ndani ya Yanga kwa kuwa hakuna ambacho tumeweza kufanikiwa hakuna taji tulilochuk

MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA

Image
MUONEKANO wa Ukurasa wa nyuma Gazeti la Championi Ijumaa 

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA

Image
MUONEKANO wa Ukurasa wa mbele Gazeti la Championi Ijumaa 

FEI TOTO AKABIDHIWA TUZO YA KUWA MCHEZAJI BORA KWA MSIMU NA SportPesa

Image
KAMPUNI ya michezo na burudani ambao pia ni wadhamini wakuu wa timu za Simba na Yanga,SportPesa wiki hii waliendesha shindano la kumpata mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa timu wanazozidhamini. Kwa upande wa Yanga mshindi aliibuka Feisal Salum na kwa upande wa Simba mshindi aliibuka Clatous Chama. Shindano hili liliwataka mashabiki wa timu hizi mbili kumpigia kura mchezaji wao bora na aliyefanya vizuri kuanzia mwanzo wa ligi mpaka hitimisho kupitia mtandao wa kijamii ambapo mshindi atakabidhiwa tunzo kama  ishara ya ushindi na fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 1. Akizungumza wakati wa kukabidhiwa tuzo Feitoto alisema,  “Kwanza kabisa napenda kuwashukuru sana wadhamini wetu SportPesa kwa kutukumbuka sisi wachezaji na kutambua zaidi vipaji vyetu kwani hii inatupa motisha ya kufanya vizuri zaidi na zaidi. “Pili niwashukuru mashabiki wa Young Africans kwa kunipigia kura kwa wingi na kuhakikisha naibuka mshindi kwa timu yangu.  Pia napenda kuushukuru uongozi m

YANGA YAPOTEZWA NA AZAM FC KWA KIUNGO FUNDI AWESUAWESU ASAINI MIAKA MIWILI

Image
AWESU Awesu, nyota aliyekuwa anakipiga ndani ya Kagera Sugar ametambulishwa rasmi leo, Julai 30 kuwa mali ya Azam FC hivyo kukipiga ndani ya kikosi cha matajiri wa Dar kwa msimu wa 2020/21. Nyota huyo alikuwa anatajwa kuingia kwenye rada za Yanga ambao walikuwa ni washindani wakubwa wa Azam FC ndani ya ligi hivyo mipango imekwama kwa sasa kuibukia ndani ya Yanga. Awesu amesaini kandarasi ya miaka miwili kuitumikia Azam FC akiwa ni mchezaji huru baada ya dili lake na Kagera Sugar kufika kikomo. Awesu amesema:"Niliwahi kuwa ndani ya Azam na nilisema kuwa nitarudi hivyo ninafurahi kwa kuwa nimerejea kufanya kazi ambayo niliianza. "Hakuna mchezaji ambaye hapendi kuja kucheza ndani ya Azam FC kwa kuwa ni klabu kubwa na yenye mafanikio nina amini nitazidi kupambana ili kuwa bora zaidi."

SABABU ZA MORRISON KUSHIKILIWA NA POLISI DAR HII HAPA

Image
KIUNGO wa Yanga, raia wa Ghana, Bernard Morrison leo alikutana na joto la kukamatwa kwa muda na jeshi la Polisi Tanzania. Jeshi la Polisi Dar limethibitisha kukamatwa kwa muda kwa Morrison katika kituo cha Oysterbay. RPC wa Kinondoni, Rodgers Bukombe amesema kuwa Morrison alikamatwa baada ya kupishana maneno na askari waliotilia shaka gari lake.

SIMBA YALIPIGIA HESABU KOMBE LA FA, KIKOSI CHATIA TIMU SUMBAWANGA LEO

Image
MABINGWA wa Ligi Kuu Bara msimu huu, Simba, wamesema kuwa wataivaa Namungo kwa tahadhari kuhakikisha wanaibuka washindi ili kubeba kombe la tatu msimu huu. Simba na Namungo zitakutana katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam utakaochezwa Agosti 2 Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa. Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, amesema: “Kikosi kipo vizuri, wachezaji wote 22 waliokuwa Tanga na Moshi walifanya mazoezi kwa muda pale Mbeya kabla ya kuondoka kuelekea Sumbawanga kwa ajili ya mchezo wa fainali,". Simba iliweka kambi kwa muda Mbeya baada ya kumaliza ligi kwa kucheza na Polisi Tanzania, Julai 26 leo wamewasili salama Sumbawanga kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo unaosubiriwa kwa shauku na wadau.

ISHU YA MORRISON KUHUSU MKATABA WAKE IPO MIKONONI MWA KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI

Image
HATIMA ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison raia wa Ghana itaamuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji. Morrison ameingia katika mgogoro wa kimkataba na waajiri wake Yanga ambao wanadai ana mkataba wa miaka miwili huku mwenyewe akidai kuwa mkataba wake umefikia tamati hivi karibuni. Uongozi wa Klabu ya Yanga umeamua kuliwasilisha suala hilo katika Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ili kuweza kupatia ufumbuzi wa mwisho. Akizungumza na Championi Jumatano Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo, amesema kuwa, suala la Morrison limefikishwa katika Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ambayo italitolea ufafanuzi muda si mrefu. “Yanga wamelifikisha suala la Morrison katika Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ambayo ndiyo itakayotolea ufafanuzi suala hilo la mkataba wake ndani ya klabu hiyo. “Kamati itakutana na kuamua juu ya suala hilo na itajua lini itatolea maamuzi suala hilo, taasisi ina utaratibu mzuri w

ALIYEFANIKISHA DILI LA SAMATTA KUKIPIGA ASTON VILLA APIGWA CHINI MAZIMA

Image
KLABU ya  Aston Villa  imemfuta kazi mkurugenzi wake wa michezo,  Jesus Garcia Pitarch,  baada ya kukosoa sera za usajili za klabu hiyo. Pitarch aliondoka klabuni hapo siku ya Jumatatu ikiwa ni siku moja baada ya timu hiyo kufanikiwa kusalia katika  Ligi Kuu  ya  England  baada ya kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya  West Ham United. Ilifahamika kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo,  Dean Smith,  alihakikishiwa kibarua chake na kuahidiwa kiasi cha fedha kwa ajili ya usajili ingawa klabu ilishaanza kufanya tathmini ya msimu uliomalizika na mikakati ya msimu ujao. Smith  ndiye aliyependekeza usajili wa  Tyrong Mings  na  Tom Heaton  ambao walikuwa na matokeo chanya katika klabu hiyo. Katika majira ya kiangazi,  Villa  ilitumia kiasi cha pauni milioni 140 katika usajili huku  Pitarch  akiwa ndiye aliyehusika katika kuleta wachezaji wakiwemo  Wesley Moraes  aliyenunuliwa kwa ada ya rekodi ambayo ni pauni milioni 21,  Matt Targett, Douglas Luiz, Marvelous Nakamba  na  Mbwana Samatta. Pitar

VIDEO: UWANJA WA NDONDO ALIOCHEZEA MORRISON, WACHEZAJI, MASHABIKI WAFUNGUKA

Image

YANGA WANA JAMBO LAO, USAJILI WA MAJEMBE YA KAZI NI KAMILI ASILIMIA 90

Image
KAMPUNI ya GSM kwa kushirikiana na Kamati ya Usajili ya Yanga tayari imekamilisha usajili wake kwa asilimia tisini katika kuelekea msimu ujao. Yanga imepania kufanya usajili wa kisasa wenye ubora utakaoendana na hadhi ya timu yao ili kuhakikisha wanawapoka watani wao, Simba ubingwa wa Ligi Kuu Bara waliouchukua mara tatu mfululizo 2017/2018, 2018/2019 na 2019/2020. Mastaa wanaotajwa kuwepo kwenye rada za Yanga ni washambuliaji Tuisila Kisinda (AS Vita), Sogne Yacouba (huru), Heritier Makambo (Horoya AC), Jesse Were, Maric Makwata (Zesco), mabeki wa pembeni, Eric Rutanga (Rayon Sports), Yassin Moustapha (Polisi Tanzania). Wengine ni Kibwana Shomari (Mtibwa Sugar),beki wa kati Abdallah Shaibu ‘Ninja’ (La Galaxy), Ibrahim Ame ‘Varane’ (Coastal Union) na kiungo Ally Niyonzima (Rayon Sports). Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassan Bumbuli, alisema kuwa asilimia 90 ya usajili wa wachezaji wa kimataifa kutoka nje ya nchi na wazawa umekamilika, hivyo watajiunga n