SIMBA YALIPIGIA HESABU KOMBE LA FA, KIKOSI CHATIA TIMU SUMBAWANGA LEO


MABINGWA wa Ligi Kuu Bara msimu huu, Simba, wamesema kuwa wataivaa Namungo kwa tahadhari kuhakikisha wanaibuka washindi ili kubeba kombe la tatu msimu huu.

Simba na Namungo zitakutana katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam utakaochezwa Agosti 2 Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, amesema:“Kikosi kipo vizuri, wachezaji wote 22 waliokuwa Tanga na Moshi walifanya mazoezi kwa muda pale Mbeya kabla ya kuondoka kuelekea Sumbawanga kwa ajili ya mchezo wa fainali,".

Simba iliweka kambi kwa muda Mbeya baada ya kumaliza ligi kwa kucheza na Polisi Tanzania, Julai 26 leo wamewasili salama Sumbawanga kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo unaosubiriwa kwa shauku na wadau.


Comments

Popular posts from this blog

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

KOCHA BIASHARA UNITED: WACHEZAJI NIMEWAPA KAZI YA KUPAMBANA NA JEZI YA NJANO

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI