Posts

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA

Image
   IKIWA Simba watakuwa kwenye mwendo huu ndani ya msimu wa 2021/22 kengele ya hatari inawaka kwenye kichwa cha Kocha Mkuu, Didier Gomes kwa kuwa kutakuwa na hatihati ya kuachia ubingwa kwa wapinzani wao pamoja na kushindwa kufurukuta kwenye mechi za kimataifa. Hili linakuja kutokana na rekodi kuonyesha kwamba wachezaji wake wengi muhimu wamekuwa wakikutana na minyoosho ya maana huku Gomes akikiri kwamba ligi ni ngumu na ushindani ni mkubwa. Iliwatokea Liverpool ya Ulaya msimu uliopita baada ya kuwakosa nyota wake muhimu kutokana na kupatwa minyoosho uwanjani miongoni mwao alikuwa ni beki kisiki Virgil van Djik ambaye aligongwa na alikaa nje msimu mzima wa 2020/21 na timu yake ikapoteza ubingwa. Hapa Championi Jumatatu inakuletea orodha ya wachezaji walioanza na majanga 2021/22 huku Simba ikiwa ni namba moja kwa timu yenye wachezaji wengi wenye majanga:- Joash Onyango Beki kisiki wa Simba hana bahati na mechi kubwa kwa kuwa aliwahi kupata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Kaize

AZAM FC KAMILI GADO KUWAVAA PYRAMID YA MISRI

Image
 MATAJIRI wa Dar es Salaam, Klabu ya Azam FC imeweka wazi kuwa ipo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramid FC ya Misri. Mchezo huo wa kukata na shoka utachezwa bila ya uwepo wa mashabiki kutokana na maelekezo kutoka Shirkisho la Soka Afrika, (Caf) kwa sababu ya suala la Corona. Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa matarajio makubwa kwa timu hiyo ni kufanya vizuri kwenye kila mchezo ambao watacheza kutokana na uwepo wa wachezaji wazuri pamoja na benchi la ufundi makini. "Azam FC tupo tayari kwa ajili ya ushindani, baada ya kuweza kushinda mechi zile za awali sasa tupo kwenye hatua nyingine ambayo tunatambua kwamba itakuwa ngumu na ushindani ni mkubwa. "Kikubwa ni kuweza kuona tunapata matokeo kwani ipo wazi kila timu ambayo inaingia uwanjani inahitaji ushindi nasi pia tunahitaji kushinda," amesema. Kikosi cha Azam FC kimeendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo huo kwenye viunga vyao pale Azam

KIUNGO YANGA ABAINISHA SABABU ZA KUCHEZA CHINI YA KIWANGO

Image
 KIUNGO mkabaji mpya wa Yanga, Mganda,  Khalid Aucho,amewaambia mashabiki kuwa  watarajie kuona soka safi la pasi linalochezwa  katika baadhi ya klabu kubwa Ulaya kwenye  michezo ijayo wa Ligi Kuu Bara. Kauli hiyo aliitoa mara baada ya mashabiki wa  timu hiyo kulalamikia kiwango kibovu licha ya  kupata ushindi kwenye mechi ya ufunguzi dhidi ya Kagera Sugar. Kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Kagera Sugar ambao ulikuwa ni wa ufunguzi kwa msimu wa 2021/22 Yanga ilifanikiwa kupata  ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na kiungo mzawa, Feisal Salum ‘Fei Toto’ kwa shuti kali ndani ya  18 Uwanja wa Kaitaba.  Nyota huyo alisema kuwa kwenye mechi yao dhidi ya Kagera Sugar walicheza wakiwa wamechoka baada ya kutumia nguvu mbele ya Simba lakini wana imani ya kuendelea kufanya vizuri kwenye mechi zijazo.  "Mchezo wetu dhidi ya Kagera ulikuwa mgumu, lakini licha ya ugumu tunashukuru kuanza ligi  vizuri kwa ushindi ambao umetuongezea nguvu  katika michezo ijayo. “Mchezo wa mwanzo tulicheza

ORODHA YA NYOTA WANAOMPASUA KICHWA GOMES,KUNA KESI MAALUMU

Image
  LAZIMA kichwa cha Didier Gomes kwa sasa kiwe kinapasuka kwa sababu mastaa wake wote nao ni pasua kichwa kutokana na mwendo wao ulivyo pamoja na mechi ambazo zipo mbele yake. Gomes anakibarua cha kutetea taji la Ligi Kuu Bara ambalo Simba ilitwaa msimu uliopita wa 2020/21 pia ana kazi ya kuhakikisha kikosi hicho kinaweza kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa na zaidi ya hatua hiyo ila sasa mastaa wake wameanza tofauti kabisa msimu huu. Hii ni alama mbaya ikiwa hali itaendelea kuwa namna hii na majanga yakaendelea lazima Gomes achange karata vizuri huku akivuta picha kwamba kwa sasa hana nyota wake wawili ambao ni Clatous Chama na Luis Miquissone waliokuwa ni wachezaji muhimu pia kikosi cha kwanza. Spoti Xtra ilipata nafasi ya kuzungumza na Gomes ili kujua kuhusu hesabu zake pamoja na namna ambavyo anawatazama wachezaji wake hao ilikuwa namna hii:- Sadio Kanoute Nyota huyu ingizo jipya ndani ya kikosi cha Simba mwenye umri wa miaka 24 ni raia wa Mali na alitambuli

JEZI AMBAZO ZILISTAAFISHWA NA SABABU PIA

Image
 KUNA namba za jezi ambazo huwa zinastaafishwa na kuwekwa kabatini mazima huko majuu Kibongobongo huwa inakuja kisha inakataa lakini leo acha tucheki zile za mbele kwanza namba za jezi ambazo zilistaafishwa kutokana na sababu mbalimbali. Kwa timu ya Birmingham City jezi namba 22 iliwekwa kabatini na hakuna mchezaji ambaye atakuja kuitupia tena na sababu ya jezi hiyo kustaafishwa ni baada ya Birmingham kuwapa heshima ya kuvunja rekodi ya uhamisho klabuni hapo wakimuuza kiungo wao Jude Bellingham kwenda Klabu ya Borussia Dortmund kwa pauni milioni 25. Namba 10 2000 Klabu ya Napoli walikubali kuistaafisha jezi namba 10 iliyokuwa ikivaliwa na legend, Diego Maradona na hiyo ilikuwa ni kutokana na mchango wa nyota huyo aliyedumu miaka 7 katika timu hiyo. Aliweza kutimiza majukumu kwa timu yake kutwaa taji la Serie A mara mbili ambayo wanayo mpaka sasa. Timu ya taifa ya Argentina ilitaka kufanya hivyo mwaka 2020 ila Shirikisho la Soka la Kimataifa, (Fifa) liliweka ngumu. Kwa sasa nyo

ORODHA YA MASTAA WANAOPIGIWA HESABU NA NEWCASTLE

Image
KLABU ya Newcastle United inatajwa kuanza kuandaa orodha ya mastaa wakubwa ambao watakuwa ndani ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England. Hivi karibuni klabu hiyo imenunuliwa na matajiri wakubwa akiwemo Mohammed bin Salman na Simon Brothers inaonyesha kuwa inataka kushusha majembe kadhaa ya maana kwenye ligi. Kuna nyota kibao wakubwa wamekuwa wakitajwa kwamba wanaweza kuibuka katika kikosi hicho kutokana na uwepo wa mkwanja wa kutosha kwa mabosi hao wapya. Mastaa ambao wanatajwa kuwekwa kwenye rada za timu hiyo ni pamoja na Gareth Bale, Edinson Cavani, Neymar Jr na Mauro Icard. Pia jina la Steven Gerrad ambaye anaifundisha Rangers ya Scotland linatajwa kuwa kwenye orodha ya makocha ambao wanaweza kuinoa timu hiyo. 

VIDEO:TAZAMA NAMNA WANAJESHI WA MPAKANI WANAVYOWAVUTIA KASI AL AHLY TRIPOL

Image
BIASHARA united wanajiita Wanajeshi wa Mpakani wana kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Ahly Tripol ya Libya unaotarajiwa kuchezwa kesho, Oktoba 15 Uwanja wa Mkapa.  Wachezaji hao wameendelea kuwavutia kasi wapinzani wao kwa kufanya mazoezi Uwanja wa Mkapa.Miongoni mwa nyota hao ni pamoja na Duchu,Redondo,James Ssetuba ambao wapo Dar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo.