RONALDINHO MZEE WA KUKERA AMBAYE NI BALOZI WA BARCA


 MIONGONI mwa wachezaji ambao rekodi zao ni bora ndani ya uwanja ni pamoja na raia wa Brazil anaitwa Ronaldo de Assis Moreira aliletwa duniani Machi 21,1980 ana umri wa miaka 41.

Jina lake maarufu ni Ronaldinho Gaucho ama kifupi wengi hupenda kumuita Ronaldinho ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na kwa sasa ni balozi wa muda wote wa Klabu ya Barcelona.

Amecheza jumla ya mechi 511 katika timu mbalimbali ambazo aliweza kucheza zama za maisha yake ya soka na alifunga jumla ya mabao 205. 

Rekodi zinaonyesha kwamba alikuwa ndani ya Gremio msimu wa 1998/2001 ambapo alicheza jumla ya mechi 89 na alifunga mabao 47. Ni timu ya Barcelona hapo alicheza mechi nyingi zaidi ambazo ni 145 na alifunga mabao 70.

Ndani ya Klabu ya Fluminens ya Brazil rekodi zinaonyesha kuwa msimu wa 2015 alicheza mechi chache kwa maisha yake ya soka ambazo zilikuwa ni 7 na hakupata bahati ya kutupia bao hata moja.

Katika timu yake ya taifa ya Brazil rekodi zinaonyesha kwamba alicheza jumla ya mechi 154 na alitupia jumla ya mabao 62 ila hii ni jumla ya mechi zile za kuanzia timu ya vijana pamoja na ile ya wakubwa katika mashindano yote pamoja na mechi za kirafiki.

Ni miongoni mwa rekodi ambazo haziwezi kuandikwa wala kusomwa zote kwa wakati mmoja kutokana na nyota huyo kufanya mengi ndani ya uwanja, ikiwa hii ni badhi ya rekodi za nyota huyo aliyekuwa akifanya watu waone mpira ni kitu chepesi.

Nafasi yake ambayo anacheza ni kiungo mshambuliaji lakini pia anaweza kucheza katika nafasi ya winga bila matatizo yupo kwenye rekodi za wachezaji bora wa muda wote.

Mkononi ana tuzo kibao ikiwa ni pamoja na mchezaji bora wa Fifa kwenye Kombe la Dunia pia ana tuzo ya Ballon d'Or ambapo siku aliyopewa alimwaga machozi ya furaha na alieleza kuwa sababu ya kufanya hivyo ni kumbukumbu ya kuambiwa na babayake acheze peku kwa hisia kumbe sababu ilikuwa ni mshua kutokuwa na mkwanja wa kununulia viatu.

  Ni miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa ni mafundi wa kupiga mapigo huru, wazee wa kukera, kuchezea mpira namna anavyotaka pamoja na pasi za maudhi bila kuangalia kule anakopiga na inafika kwa uhakika.






Comments

Popular posts from this blog

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA