TIMU YA TAIFA U 23 YAREJEA NA TAJI
KIKOSI cha timu ya taifa chini ya miaka 23 leo Agosti Mosi kimewasili Tanzania kikitokea nchini Ethiopia ambapo kimetwaa taji la Cecafa. Ushindi wa penalti 6-5 mbele ya Burundi uliwapa nafasi ya kutwaaa taji hilo. Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), Wallace Karia amesema kuwa ni jambo la furaha kwa ushindi waliopata. Mbali na Karia pia Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao nao alikuwa miongoni mwa waliokuepo leo Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere. Mashabiki nao walijitokeza kwa ajili ya kuwapokea wachezaji hao ambao wameweza kuipeperusha vema bendera ya Tanzania. Wakiwa na ngoma zao mashabiki walipata pia muda wa kucheza na wachezaji wa U 23 pamoja na kupiga picha na kombe hilo nje ya uwanja kwa muda.